Kiini cha Tatizo ni hiki...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
Baada ya kufuatilia habari nyingi na majadiliano mengi kuhusu mambo mbalimbali nimegundua kuwa wengi wetu hatuna habari sahihi, na hoja zetu nyingi zinatokana na kushuku na kusikia bila kuwa na habari sahihi za kile kinachozungumzwa. Ni vigumu kupata habari toka serikalini kwani vikwazo ni vingi sana; huwezi kusoma mkataba fulani hadi uwe unahusika katika utekelezaji wa mkataba huo, huwezo kupewa habari kwani "msemaji" hayupo, n.k Ndugu zangu tatizo ni kuwa hatuna sheria inayolazimisha vyombo vya serikali (wizara, idara, mawakala nk) watoe habari kwa raia.

Ni kwa sababu hiyo basi inakuwa vigumu sana kupata habari sahihi na zisizofichwa fichwa. Leo hii ukitaka kuona mikataba ya madini, nishati n.k huwezi kupewa kwani ni ya siri! Kinachoudhi zaidi ni kuwa wabunge wa Upinzani ndio wanaonekana wakisema mambo ya maana bungeni na kuhoji mambo ya msingi!! Hivi wabunge wa CCM wanakilisha watu gani? Hivi haiwaumi wao malalamiko ya wananchi!! Hivi wote ni waoga hakuna wale waenda peke (mavericks)?

Ninachosema ni kuwa wakati umefika Bunge badala ya kuomba taarifa toka serikalini, au kwa viongozi wa serikali litunge na hatimaye sheria ipitishwe yenye kulazimisha vyombo vya serikali kutoa habari kwa uhuru kwa wananchi bila kuficha vingevyo chombo hicho kinatozwa shilingi milioni 10 kwa kila siku inapochelewa kutoa taarifa hiyo, na viongozi wake wanatozwa laki moja kwa kila siku wanachelewa kutoa habari hizo! Sheria hii ijulikane kama "Sheria ya Uhuru wa Habari". Hii italazimisha mikataba kujulikana na kuwekwa wazi, itatufanya tujue nani amefanya nini na wapi, itatusaidia kutambua ni wapi kwenye udhaifu! Ama sivyo tutaendelea kuota, na kuombea watuonee huruma na kutupa habari!!!!
 
Mzeemwanakijiji
Umenichekesha sana japokuwa ume raise a very serious issue .Kama Wabunge wa CCM wanashindwa kuhoji uozo wa Serikali kwa jinan kulinda maslahi ya Chama na si kukibomoa na kama Rais anaweza kumiliki vyombo vya habari hadi sasa vinamwandika yeye na kumwaga sifa je Wabunge wale waoga wa CCM wanaweza kweli kusimama na kudai ajambo ambalo likipita itakuwa ni shida kwa CCM baadaye ?

Hebu waulize waandishi sakata la wagushi vyeti na kuiwa na PhD lilienda kwa DCI kwa mara ya mwisho liko wapi sasa mbona hawa andiki wala kumuuliza DCI kapata nini kwenue Uchunguzi ama wanangoja Tume iundwe ? ????
 
Chifu, ni lazima kuwe na watu wachache ambao wana uchungu na nchi yao. Binafsi nasubiri kikundi cha wananchi kiamue kuifikisha serikali mahakamani ili iweke mikataba yote hadharani na kujua kama kifungu kinachokataza watu kuiona mikataba hiyo hakipingani na katiba ya nchi!
 
Mzeemwanakijiji mimi nilidhani unasema unatafuta watu wa kuunda kikundi kwenda Mahakamani kumbe unangoja watu waanzishe wewe uangalie ? Hili ni gumu wewe sema unatafuta watu uwe mmojawapo wa kwenda Mahakamani hapo nami nitakuwemo lakini watu kwa Tanzania hakuna maana wote wanajua JK anachapa kazi sana sana .
 
Chifu, believe me.. ningekuwa nyumbani... miye si mtu wa maneno matupu...! Lakini hata hivyo tunaendelea kufanya vizuri wana bodi, kwa sisi waandishi silaha kubwa na ya pekee tuliyo nayo ni peni (nowadays the laptop!)

Tutaendelea kupiga kelele... msikose podcast yangu nina swali la kumuuliza Mhe. Kikwete...!
 
Mwanakijiji,
sidhani kuwa umbali ndo tatizo, tatizo ni kupata watu wenye nia nk. Ninachosema ni kuwa kama kweli upo serious unaweza ukaanzisha bila hata kukajaga bongo. Na kama ukuiregister kama charitable organisation popote ulipo, unaweza ukashangaa utakapopata umaarufu na hata kutoka kwenye luninga za majuu. Kwani wengi wa hao wafadhili nao wana kichefuchefu na sirikali yetu.

Ila kwa upande wa pili itabidi uwe ngangari sana kwani mkono wa hiyo sirikali na mashushushu wake hawatakawia kukumulika na sijui wataishia wapi, kwani lengo lao litakuwa kukusambaratisha wewe na hao washirika wako wa hiyo organisation.

Goodluck.
 
When you are doing the right thing Mashushu wataona aibu na hatuwezi kuachia Nchi inaharibika kisa kuogopa mashushu that is very wrong .Again naomba kama kuna watu wako serious tuanze kujipanga sirini tuone cha kufanya .Napatikana kwa mail hii hapa sitaki maneno kama Mzeemwanakijiji ila vitendo
salmamee@yahoo.com
Nangoja kuwasikia
 
Chifu, mimi nataka tuwe na kikundi cha kama watu 20 hivi. Watu ambao wamehamasika kisiasa na wako tayari kuweka rehani heshima, na majina yao. Ni kweli umbali si tatizo, ila ni nia na jitihada za watu.
 
Chifu, mimi nataka tuwe na kikundi cha kama watu 20 hivi. Watu ambao wamehamasika kisiasa na wako tayari kuweka rehani heshima, na majina yao. Ni kweli umbali si tatizo, ila ni nia na jitihada za watu.

Mkuu MM,
hao 20 walipatikana? naona mikataba iliyokuwa siri sasa inapatikana mtaani...lakini visheni yako ni kubwa zaidi ya kudai haki ya kusoma nyaraka za "siri" za serikali
 
Back
Top Bottom