Kiingereza kinanitesa, nahitaji ushauri

mimi mtakatifu

JF-Expert Member
Oct 11, 2019
207
482
Habari wadau,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, mimi nina tatizo kubwa la kuongea Kiingereza. Nimekuwa nikipoteza fursa nyingi kwa sababu ya kushindwa kuwa fluent kwenye kuongea English.

Mimi ni mwajiriwa kwenye international NGO, nina uwezo mzuri wa kufanya kazi na zinakubalika na kila mtu ila ukinipa nafasi niongee nnachofanya kwa Kingereza nina struggle sana.

Nikiandika vitu vinanyooka ila nikiongea kuna muda mpaka napanic nashindwa kabisa kuongea.

Nimeshashindwa interviews nyingi sababu hiyo.

Nimeshakosa fursa nyingi za kufanya presentation ambazo zingeniuza sababu hiyo.

Kwa mtu asiyenifahamu ni ngumu sana kuamini uwezo wangu kama tukifanya conversation kwa Kiingereza.

Kiasi kwamba sasa nimeona siwezi kuendelea kuishi namna hii naitaji msaada wa mawazo namna gani naweza kuboresha kingereza changu cha kuongea.

Naombeni ushauri.
 
Inatakiwa uweze kujieleza kwa kiswahili kwanza kabla ya kiingereza, kujieleza hakuhusiani na utaalamu wa lugha bali kujiamini. Ukiweza kujiamini kwa kiswahili basi endelea kujifunza lugha ya kiingereza (hasa kwa kusoma vitabu vya simulizi). Siku misamiati ikiwa mingi kichwani utaona unavyotiririka mwenyewe.
 
Hata hivyo unaeza kuwa Rais wa Tanzania siku moja. Hiyo ni dalili nzuri (utani).

Mimi nilikuwa katika hali yako. Ninapenda sana kufanya kazi mashirika ya kimataifa lakini ikija kwenye ngeli, shida. Unajua tena Kiingereza cha kujifunzia ukubwa. Walimu wenyewe wa sekondari na chuo wanafundosha masomo ya Kiingereza kwa kutumia Kiswahili. Walimu ndio hawa hawa akina Magufuli (Sengerema Sekondari).

Nimejitahidi sana kujilazimisha kuongea ongea kama sehemu ya practice. Baadaye nikapata fursa ya kuwa nje ya Tanzania, nikajitahidi sana. Kwa sasa naweza kuwasiliana vizuri tu. Unapojifunza usijali watu kukucheka. Mbona Wachina, Wajapan, Wafaransa hawana aibu wanapovunjavunja Kiingereza? Sisi Waswahili shida yetu ni aibu na kuchekana.

Lakini pia kumbuka kuwa ukijifunzia ukubwani, hata ukiongea hauwezi kuwa kama mtu aliyeanza wakati ni mtoto. Isitoshe public speaking pia ni skill ambayo inaweza isihusiane na uwezo wa lugha.

Kuna watu hata kwa Kiswahili ama kilugha chao hawawezi kusimama mbele za watu na kuongea. Ndio maana Englsih medium/International schools wanafundisha watoto kujieleza tangu madarasa ya mwanzo. Wanasimamishwa kwenye majukwaa mbele ya wenzao na kuimba, kujieleza nk. Wanazoea. Na waliopitia mfumo huu huwa wanashinda tu interview hizo unazosema huwa unashindwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom