Kiingereza hakijakamilika kama kiswahili?

okaoni

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
1,471
1,299
1.Mdogo wa baba, mkubwa wa baba ,kaka yake na mama kiswahili kila moja na jina lake na msikilizaji anajua moja kwa moja anatoka upande gani wa wazazi mfano Baba mdogo, baba mkubwa, na mjomba lakini kwnye luga ya kiingereza wote hao huitwa uncle hivyo kushindwa kumfanya hadhira kujua anatoka upande gani wa wazazi

2. Kadhalika Mkubwa wa mama huitwa mama mkubwa, mdogo wa mama huitwa mama mdogo na dada yake na baba huiywa shangazi lakini kwenye lugha ya kiswahili watu woote hao huitwa unt hivyo hadhira haiwezi kujua muusika anatoka upande gani wa wazazi.

3.kiswahili Gunia ni gunia, mfuko wa rambo au wa plastic yaote huitwa hivyo hivyo na bagi la kuwekea ngua huitwa begi kataika matumizi ya kawaila lakini vitu vyoote hivyo kwenye Lugha ya kiingereza huitwa Bag.

4. mtu akiwa anaumwa kiswahili unamuambia pole, ukitaka kumboamba mtu radhi kiswahili unamwabia samahani lakina maneno yoote hayo kiingereza hutamkwa soory hivyo kuwafanya wazungu wanaojifunza kiswahili kutumia neno samahani wakimaanisha pole.

Yapomabo mengi ambayo kiingereza yanaenda ndivyosivyo unavyo yatafsiri kiswahili na kufanya waandaaji wa filamu tanzania kushindwa kutafsira hisia za maneno ya kiswahili kwenye sub tittles za kiingereza hata kama mtafsiri muhusika atakuwa mtaalamu wa lugha zote mbili
 
Back
Top Bottom