Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Katibu Mwenezi wa CCM, Kenani Kihongosi amemwomba Jaji Mstaafu, Joseph Warioba asiwe na chuki kwa viongozi waliopo bali awashauri kwa hekima badala ya kulalamika mtandaoni.
Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma siku ya Jumamosi, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi ameeleza kusikitishwa na hatua ya Jaji Warioba kutoa kauli ambazo chama hicho kinaziona kama zenye chuki na ulalamishi, siku chache tu baada ya kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.
“Warioba amekutana na Rais siku nne hazijapita yupo tena mtandaoni. Sasa inasikitisha kidogo lakini tunachomuomba kwamba astaafu vizuri aendelee kupumzika lakini asiwe na chuki kwa viongozi waliopo kwa sababu ana uwezo wa kushauri na kufika katika mamlaka husika na kuweza kuishauri kwa hekima kuliko kwenda kulalamika kwenye mitandao”, amesema Kihongosi.