Kigwangalla na Hoja ya Kutafuta Umaarufu wa Kisiasa Kupitia Kupanda Bajaj ama Bodaboda!

HKigwangalla wakati unaomba na kuhonga hela ili upate huo ubunge hukujua hayo yote? wakati familia ya JK inakusaidia ili upate ubunge ulijua majukumu yake?
je kupiga picha na kuziweka fb ni moja ya majukumu ya mbunge au ndo huo ugumu huoni kama unajishushia heshima yako na unathibitisha kuwa hukutakiwa kuwepo hapo ulipo?
Juzi Juzi ulisema unautaka uraisi, kama ubunge umekuwa shida kiasi kwamba umeanza usanii wa kupanda bodaboda ili kutafuta huruma ya wananchi baadala ya kupiga picha ukiwa jimboni kwako ukishirikiana na wananchi kutatua kero walizonazo unatuthibitishiaje kuwa ukipata urais hutaenda kubembea au kupanda farasi huko kwenye nchi za watu?
 
Last edited by a moderator:
Its funny unahalalisha kupanda bodaboda eti kwa vile umekulia uswahilini na hapo hapo unakubali kuwa si salama, halafu bado huvai helmet, and yet unapiga picha,halafu unakiri kabisa picha imepigwa makusudi na wewe ndo umeiweka facebook. Nyie viongozi balaa.
I think ile nukuu ya Invisible ''Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!'' itakusaidia sana in your future 'publicity stunts'.
 
Ndg. Mazindu,
Kutwa na gari Arusha ama kutokuwa nalo si ishu sana hapa, kwa sababu ningeweza kupanda taxi.
Kupiga picha na kuiweka FB, kama nilivyoeleza hapo juu, lengo lilikuwa kuanzisha mjadala (kama huu unaoendelea) wa safety promotion - nenda kasome post yangu ya FB utaona maelezo yanayoambatana na picha hiyo.

Re,
HK.

Y hukupiga picha na boda boda za huko kwenu tabora? Kama mantiki ni kupromote safty promotion?
 
"In search of an ATM this evening in dowtown Arusha I boarded 'Kibodaboda'; the following quickly crossed my mind: efficient commuting cheap and affordable to many, income generating to urban as well as rural youth,high risk of deadly accidents - appropriate education and regulation is needed to promote safety!"


Kama hicho ndicho kilichoandikwa na huyu mbunge, basi sidhani kama kuna mjadala tena hapo.

Dawa ya hivyo vyombo mbunge alivyoviita 'vulnerable' ni kuviondoa tu. Sasa ukianza kuviona kwa ni vya bei rahisi na vyanzo vya mapato kwa watu mijini na vijijini, hakika hakuna umakini katika mjadala.

Ndugu Hamisi, katika tembea yako, umeona wapi katika mataifa yenye kujali watu wao (husilete mifano ya India, Vietnam na China hapa) vyombo hivyo vinatumika kama vya kubeba abiria?
Ni katika mataifa yaliyo na ufinyu wa mawazo katika kutatua kero za usafiri, ndiyo uja na masuluhisho kama haya ya kuruhusu bajaj na bodaboda kubeba abiria.

Kama upo makini, peleka mjadala huu bungeni; au pendekeza mjadala wa kitaifa. Maana vyombo hivi ni janga la kitaifa, ambalo linasubiri state declaration kuwa maafa.
 
Ni kweli, ni hatari sana kwa sababu mimi ni mkweli na muwazi, na watu kama wewe wamezoea wanasiasa waongo!

kaka watu wanataka kukutoa kwenye mada nawewe unakubali kirahisi hivi? We ng'ang'ania hoja,wananchi wa jimboni kwako tunafuatilia umakini wako ktk kujbu hoja za wanaJF.
 
umesema utagombea vipindi viwili na ss unafikiria kutogombea hicho cha pili mawazo yangu umeona ngoma ngumu na hakuna ulichofanya na unamuofia na kumuogopa husein bashe aka kamanda wa kisomalia
 
Nzi kutaka vyombo hivi vipigwe marufuku ni jambo lisilo sahihi sana kwa sasa, maana vyombo hivi vinatoa ajira kwa wananchi (vijana waendeshaji na hata wamiliki), pia vinatoa huduma ya usafiri mijini na hata vijijini (ambako kwingine hakupatikani usafiri wa rahisi na wa haraka). Jambo la busara, kwa maoni yangu hapa, rationally na objectively, ni kwamba tuongeze usalama kwenye vyombo hivi kwa kutunga sheria na bylaws zinazoongeza usalama na kupunguza ajali mbaya - na kikubwa zaidi hapa ni law enforcement isiyo na mzaha wala msalie mtume! Nchi nyingi zinazoendelea usafiri wa tuk-tuk na pikipiki umekuwa mainstay kwa watu wenye kipato cha chini na wenye haraka, kulingana na uwepo wa traffic jams na pia kukuwa kwa gharama za mafuta kitu ambacho kimepandisha sana gharama za usafiri mijini.

Political interest ya kila mwanasiasa ni kutafuta solution ya matatizo ya wananchi, na Bajaj na bodaboda zinatoa suluhu ya matatizo ya wananchi ya ku-commute, na uwepo wake ni muhimu zaidi ya kutokuwepo kwake. Kama chama chako kina ubavu wa kuondoa njia hizi za usafiri, hebu waambie wajaribu kuleta hoja hiyo Bungeni tuwaone kama wataweza.

Duniani kuna law ya uchumi inayosema demand ikiwepo utashangaa supply imetokea wapi....demand creates its own supply...bajaj, bodaboda hazikuwepo a couple of years back lakini leo zimekuja...nakumbuka mwaka 2004 nilipoenda Bangkok, Thailand kwa mara ya kwanza nilishangaa kuona kuna usafiri wa Bajaj (ambazo huku experience yangu ilikuwa ni kwamba ni tricycles za walemavu) na pikipiki ni za watu binafsi ama watumishi wa umma (kwa usafiri wao private na wala siyo abiria) ---just some few years later na sisi tulipokuwa kiuchumi kufikia hatua fulani zimeanza kuingia...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, mheshimiwa HKigwangalla.

You are going too low in embarking to engage in this kind of discussion.

Know that sometimes to be silent is much wiser than having silly and unproductive debates!

It is a pity that wakubwa wetu siku hizi hamjui vifungo vya itifaki, na kama mnavijua hamvifuati.
 
Maisha ni mzunguko, kuna wakati huwa napaki gari yangu na kupanda daladala, huwa najisikia raha sana kukumbuka maisha yangu haya.
Kuna mazingira ambayo unalazimika kupanda bajaji au pikipiki, na sana sana muda fulani, hasa wa usiku kama uko katika mishe mishe na taxi hakuna, especially kama uko mikoani kikazi.
Kwa hili la Mh. HK nina haya, kama alipenda na alikuwa katika utafiti wake basi siyo mbaya, hilo mosi, pili, kwa kuwa kiongozi, kioo cha jamii, uneyelipwa mafuta kutokana na kodi za wananchi, na nina imani una dereva, inakuwa vigumu watu kukuelewa!
Lakini pia, Nakumbuka kuna wakati hapa JF ilipostiwa picha ya Waziri Mkuu wa Ufaransa nafikiri, alikuwa akienda ofisini kwa bike huku amepiga suti yake, wadau wengi waliisifu hii makitu kweli kweli!
Watanzania sisi ni wanafiki sana, kama Mh. HK alikuwa na lengo zuri ni vibaya kumbeza!
 
Dr. HK pole sana majukumu mazito tulio kukabidhi, kaka unapata wapi muda wa kuyajadili haya? ni kwa nini usije na mjadala kama wa kufufua viwanda vyetu ambavyo chama chako kimevinadi?
 
another quick question, je unaamini uongozi ni utumishi wa uma? kwa nini unang'ang'ania nafasi za uongozi mpaka unatoa bastola kutishia uhai wa mwingine (bashe).

last qn, bastola yako ulirudishiwa na polisi?
 
hivi nzega hakuna mtu mwingine wa kugombea ubunge zaidi ya hawa wachumia tumbo bashe na kigangwala? yule mzee aliefanyiwa mizengwe na kina rostamu yuko wapi?
 
Kigwangala,mnalipwa milioni 11 kwa mwezi,mna mashangingi ya bei ghali mliyokopeshwa na serikali(pesa za kodi za hao hao masikini).

Hiyo picha ni usanii kwasababu kama ni hoja ungeipelekea bungeni badala ya kupiga picha kama January Makamba na kibajaji.

Sioni ni kivipi kupiga picha umepanda bodaboda itasaidia kuleta awareness ama kama itabadilisha chochote,unless kama ulipanda halafu ukapata nayo ajali.Otherwise ni usanii tu kuwahadaa wananchi kwa maslahi yenu.

Umasikini mnajuwa upo,lakini kupambana nao hamtaki,badala yake mnautumia kwa manufaa yenu.Si nasikia uligawa vitumbua ili uchaguliwe?

Sasa kweli hiyo ni haki?
 
Mkuu, mheshimiwa HKigwangalla.

You are going too low in embarking to engage in this kind of discussion.

Know that sometimes to be silent is much wiser than having silly and unproductive debates!

It is a pity that wakubwa wetu siku hizi hamjui vifungo vya itifaki, na kama mnavijua hamvifuati.

Mulize mheshimiwa!

Ana Pr consultant? Au gharama yake haiwezi?

Kakurupuka tu huyo
 
Ndg. Nzi, kutaka vyombo hivi vipigwe marufuku ni jambo lisilo sahihi sana kwa sasa, maana vyombo hivi vinatoa ajira kwa wananchi (vijana waendeshaji na hata wamiliki), pia vinatoa huduma ya usafiri mijini na hata vijijini (ambako kwingine hakupatikani usafiri wa rahisi na wa haraka). Jambo la busara, kwa maoni yangu hapa, rationally na objectively, ni kwamba tuongeze usalama kwenye vyombo hivi kwa kutunga sheria na bylaws zinazoongeza usalama na kupunguza ajali mbaya - na kikubwa zaidi hapa ni law enforcement isiyo na mzaha wala msalie mtume! Nchi nyingi zinazoendelea usafiri wa tuk-tuk na pikipiki umekuwa mainstay kwa watu wenye kipato cha chini na wenye haraka, kulingana na uwepo wa traffic jams na pia kukuwa kwa gharama za mafuta kitu ambacho kimepandisha sana gharama za usafiri mijini.

Uzoefu wa nchi hizo unazozisema upoje? Ajali za vyombo hivyo zipo katika kiwango gani licha ya uwepo wa sheria na usimamizi?
Ebu tafuta hii article hapa chini:

www.ncbi.nlm.nih.gov/m/pubmed/21584976/

Soma na hii pia:

www.grsproadsafety.org/our-knowledge/safer-road-users/vulnerable-road-users

Chifu, linapokuja suala la usimamizi wa sheria, serikali ya chama chako haina cha kujivunia. Imeshadhihirisha kushindwa katika hilo.
Sasa katika hili itakuja na lipi jipya?

Kwa hiyo hoja yako ya uwepo wa vyombo hivyo ni utoaji wa ajira na huduma za usafiri? Hivyo, haijalishi kiwango cha watumiaji wa vyombo hivyo wanaopoteza maisha na wanaokuwa walemavu? Hadi sasa kwa mtazamo wa haraka (first impression) cost-benefit analysis ya uwepo wa vyombo hivyo, inadhihirisha vyombo hivyo ni janga kwa watumiaji na taifa kwa ujumla.

Ndiyo tatizo la serikali hii, kutafuta majibu mepesi kwa masuala mazito. Huwezi ukatatua tatizo la ajira kwa kuruhusu vijana waendeshe vyombo vya moto vinavyoharibu maidha yao. Huwezi ukatatua tatizo la usafiri mijini na vijijini kwa kuruhusu pikipiki na bajaj kuwa vyombo vya abiria, vinavyosababisha vifo na ulemavu kwa abiria hao.

Hapa inaonyesha namna gani serikali imeshindwa kutatua kero hizo.

political interest ya kila mwanasiasa ni kutafuta solution ya matatizo ya wananchi, na Bajaj na bodaboda zinatoa suluhu ya matatizo ya wananchi ya ku-commute, na uwepo wake ni muhimu zaidi ya kutokuwepo kwake. Kama chama chako kina ubavu wa kuondoa njia hizi za usafiri, hebu waambie wajaribu kuleta hoja hiyo Bungeni tuwaone kama wataweza.

Vyema.
Kutatua matatizo katika namna isiyoleta matatizo zaidi. Hivi unafahamu ni vijana wangapi wamefariki au kuwa walemavu kutokana na vyombo hivyo? Watu wangapi wamefariki au kuwa walemavu kwa kutumia vyombo hivyo kama vya usafiri? Sasa hizo bodaboda zinatatua tatizo au zinaleta matatizo?

Lakini, kwa sababu nia kuwa ya wanasiasa wengi wa Tanzania ni kutafuta kura kwa namna yoyote ile, uwa hawajali kama namna hizo zina madhara gani kwa wananchi husika.

Sasa chifu, wewe unafahamu chama changu? Au ndiyo ile tabia ya watu wa serikali ya CCM kumchukulia kila anayeikosoa serikali ni mwanachama wa upinzani?!? What a shame!??!

Sasa unataka ni mwambie nani tena wakati wewe umesema unataka kuchochea mjadala. Mimi sijamsikia mwingine, ndiyo maana nimekushauri kwamba,kama unataka mjadala uwe moto zaidi peleka hoja bungeni.

Duniani kuna law ya uchumi inayosema demand ikiwepo utashangaa supply imetokea wapi....demand creates its own supply...bajaj, bodaboda hazikuwepo a couple of years back lakini leo zimekuja...nakumbuka mwaka 2004 nilipoenda Bangkok, Thailand kwa mara ya kwanza nilishangaa kuona kuna usafiri wa Bajaj (ambazo huku experience yangu ilikuwa ni kwamba ni tricycles za walemavu) na pikipiki ni za watu binafsi ama watumishi wa umma (kwa usafiri wao private na wala siyo abiria) ---just some few years later na sisi tulipokuwa kiuchumi kufikia hatua fulani zimeanza kuingia...

Duh! Umewahi kujiuliza nini kilichopelekea demand ya vitu hivyo iwepo??!? Jibu ni udhaifu wa serikali katika kutatua kero ya usafiri. Yaani hata Dar, makao makuu ya serikali, kuna kero ya usafiri. Ukitoka tu nje ya mji, usafiri ni shida. Watunga sera wa serikali hii wakaja na suluhisho, bodaboda.

Duh! Kuwa na bodaboda na bajaj ni alama ya kupiga hatua kiuchumi? Chifu, acha utani bwana.

Hivi watunga sera uwa wanaenda nje kufanya nini? Mbona safari za mafunzo nje haziishi?
 
Yaani huyu jamaa ni beyond belief lol....
Kweli hii nchi sasa ni a 'clown's paradise'....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom