BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,377
- 8,121
Mjadala wa kitaifa usingepaswa kuwa Dr. Hamisi Kigwangalla amekosea, atoe ushahidi, ataje, hakupaswa kusema alichosema, ana wivu kwa kuwa yeye yuko benchi etc, bali je alichosema ni uongo ama ukweli; kama ni ukweli tunafanyaje ili kudhibiti?
Badala ya kunyoosheana kidole, ama kutaka umbeya ni nani na nani anamiliki nini na nini, kama ambavyo watanzania tunapenda, ama nani awajibike atolewe cheo, tungefikiria na kutazama mbele zaidi kuwa tufanye nini kudhibiti?
Kama alivyosema Mzee Bagonza, ni kweli mimi siyo mwanasiasa mdogo, na pamoja na kunitukana kwake (najua kwa nia ya kutaka aidha mimi binafsi nitaje ama vyombo vya umma vinilazimishe kutaja) na kuwa kama nilikuwa nafanya mzaha, basi afya yangu ya akili inapaswa kutiliwa shaka! 😀
I won’t yield to his pressure, kwa sababu ya ukubwa wangu kisiasa. Kwa nilipofikia sitafuti umaarufu wa jina langu binafsi kisiasa wala cheo tena, na sina adui wa kumuanzishia vita ya kisiasa! NATAKA TUREKEBISHE MIFUMO NA TAASISI ili tuwaachie watoto wetu nchi salama, yenye usawa, yenye haki, yenye uwazi, yenye mifumo na taasisi imara za kisiasa, za kiuchumi/kifedha na kisheria. Hii ndiyo ndoto yangu kubwa kwa sasa.
Ningekuwa na shida hiyo ningeongea bungeni ambapo najua nina kinga. Ama ningewapa wabunge walipue mabomu bungeni. Ama ningeweza kupeleka umbeya kwenye mitandao.
Vyombo vya kisheria leo hii vinaweza kutumia mamlaka yake kunitaka nitaje la sivyo nichukuliwe hatua; najua nikichagua kutotaja, nitachukuliwa hatua za kisheria, nitawajibika! Lakini haitoondoa ukweli wa udhaifu wa mifumo yetu.
Mengi ya ninayoyajua yamo kwenye taarifa ya CAG, Bungeni etc., kwani hakuna anayeona viashiria vya uwepo wa rushwa, ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi za umma?
Mfano akitokea mtu akaamua kutaja, atakuwa salama? Vyombo vyetu vya uwajibikaji watapata ushahidi? Kuna kitu hakiko sawa, na kwa hakika siyo mimi, ni mfumo/muundo wetu wa kitaasisi! Hautoi fursa ya wabadhirifu kuchukuliwa hatua kirahisi. We need reforms.
#HK #Fighter #NjeYaBox