Mkuu Chikatata, kuna mambo mawili hapo,
1. Maandamano
2. Mkutano wa hadhara.
1.Kwa vile Dr. Kigwa ni mbunge kupitia CCM, jambo lolote atakalofanya jimboni kwake lazima kipate baraka za chama chake. Maadam CCM haijatoa baraka kwa maadamano yale, then maandamamo hayatakuwepo!. Hata kama umechat na Dr kule fb akakuhakikishia maandamano yapo, amekudanganya na kujidanganya!.
2. Kama ni kweli amekuambia kuwa "chama hakina sababu ya kumzuia na wala hakina uwezo huo" pia atakuwa amekudanganya na kujidanya kwa sababu tayari chama kimeshamzuia na sababu za kumzuia kimezitoa ila ni kweli chama hakina uwezo wa kumzuia, ila chama kimewaandikia jeshi la polisi ambao ndio wenye uwezo wa kumzuia na watatumia uwezo huo kuyazuia maandamano yake, hivyo hayatakuwepo!.
3. Hilo la kusema kwamba katibu wa ccm wilayani pale amekurupuka kuandika barua ile pia amekudanganya wewe, japo ni kweli barua ile haina nguvu yoyote kisheria, ila imeandikwa kufuatia vikao halali vya ccm wilaya ambavyo Dr. Kigwa ni mjumbe halali wa vikao hivyo!, vinginevyo aseme huyo katibu amejiandikia tuu na vikao hivyo havikuwepo wala havikujadili kuhusu maandamano yake!.
4. Hata hivyo naomba nikiri wazi Dr. Kigwa ameonyesha ujasiri mkubwa wa kuwatumikia wananchi wake bila kujali chama chake kinataka nini, mgombea ubunge huwa ni mgombea wa chama na anawajibika kwa chama, lakini akishachaguliwa kuwa mbunge ni mtumishi wa wananchi na anawajibika kwa wananchi na sio kwa chama tena, hivyo anachokifanya Dr. Kigwa ndicho sahihi kabisa kinavhopaswa kufanywa na wabunge wote wa kuchaguliwa kwa kuweka mbele maslahi ya wananchi na sio ya chama!.
5. Kwa mkutano huu, naomba nikiri wazi kuwa Dr. Kigwa anajiunga na timu ya kina Deo Filikunjombe kusimama kuhesabiwa na 2015 ataendelea kuwa mbunge wa Nzega kwa sababu ameweza kuona mbali!. Bashe ndie aliyekuwa kipenzi cha wana Nzega, baada ya kupigwa zengwe, na baadaye kusafishwa, Dr. Kigwa ameshaona picha ya 2015 na kujua there is no way CCM itamsimamisha kwa sababu kipenzi chao Bashe ameshakuwa cleared, hivyo dawa pekee ya kusurvive ni kuachana na CCM na kuivest kwenye wananchi ndio maana barua yake ya maandalizi ya mkutano hakuipitishia CCM I doubt kama hata vikao vya CCM wilaya anahudhuria!.
Wabunge wenye akili ni wale wanaojua kutazama mbali, 2015 jahazi la CCM linazama, wabunge wa CCM ambao wanaitegemea CCM kuwaokoa, watazama nayo, na wale wenye akili, wana invest on people na ndio watakao waokoa kiukweli, not CCM anymore!.
Wish you all the best Dr. Kigwa!.
Pasco.