Kigwangalla aitwa na kamati ya maadili na maandamano yake kusitishwa na CCM, yeye asisitiza yapo!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigwangalla aitwa na kamati ya maadili na maandamano yake kusitishwa na CCM, yeye asisitiza yapo!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chikakatata, Jun 13, 2012.

 1. c

  chikakatata JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimepata taarifa za kiuchunguzi kwamba Mbunge wa Nzega Hamisi Kigwangallah amepigwa stop na chama chake wilayani Nzega kutokufanya maandamano yake akiambatana na wananchi na viongozi mbalimbali yaliyopangwa kufanyika kule Nzega tarehe 16/06/12.

  Nimewasiliana na mbunge huyo kwenye facebook muda si mrefu na amesema kuwa ataendelea na maandamano kama yalivyopangwa kwa kuwa mpaka sasa polisi hawajamzuia kisheria na kwa kuwa ni ya amani hakuna haja ya chama chake kuwa na mashaka kwa kuwa anafanya kazi waliyomtuma kufanya ya kuwawakilisha wananchi na kudai maslahi yao.

  Mbunge huyo anasema chama hakina sababu ya kumzuia na wala hakina uwezo huo maana kitakuwa kinamuingilia katika utekelezaji wa majukumu yake na hakuna kanuni hata moja ya kimaadili anayovunja kufanya kazi hiyo bega kwa bega na wananchi na viongozi wenzake. anaendelea kusema kwamba katibu wa CCM wilayani pale amekurupuka kuandika barua ile (ambayo nimeiamabatanisha hapa) maana haina nguvu yoyote ile kisheria na wala kikatiba ya CCM.

  Anawaalika wananchi, viongozi na wapenda haki pote nchini kwenda Nzega kuhudhuria maandamano yale. Asema mpaka sasa wabunge wafuatao waahidi kuwepo na kuhutubia mkutano huo unaotarajiwa kuwa mkubwa wa aina yake; mhe. Seleman Zeddy (CCM, Bukene), mhe. Kangi Alphaxard Lugola (CCM, Mwibara), mhe. James Lembeli (CCM, Kahama), mhe. Nyambari Nyangwine (Tarime) na anaendelea kualika wengine.

  Chikaka.

  [​IMG]
  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Anatishia nyau?! Hakuna maandamano,Kigwa ataingia mitini kama kawaida yake!
   
 3. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 602
  Trophy Points: 280
  magamba tu
   
 4. c

  chikakatata JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tusimkatishe tamaa maana inaonyesha safari hii ameamua kufanya kweli nimechat naye kwa muda mrefu na ametoa sababu za msingi sana. anasema anapigwa vita na viongozi wake wa ccm wilayani nzega kwa kuwa wanahofia akifanikisha kupata faida atapata umaarufu kisiasa na itakuwa ngumu kumuondoa kwenye nafasi hiyo 2015
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kigwagallah kasha chuja hafai kabisa bora asipoteze muda kwenye siasa aendelee na phd yake na Hilo jina la mtu analotumia
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  nguvu ya soda?
   
 7. c

  chikakatata JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona una chuki sana na kigwangallah wewe? hii ni mara ya pili na-post hapa habari zinazomhusu huyu jamaa na wewe huibuka na negativity zako, una nini?
   
 8. O

  Original JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakuna haja ya kumvunja nguvu na hasa kama anachodai ni cha msingi na faida kwa Tanzania.
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Wewe kigwagallah nimekushtukia Ngoja ghasia au Mzee Gombe wa wasikie hayo maandamano umkome nyani
   
 10. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kingwalangwala unatakiwa kusimamia maamuzi yako kama unaona yana manufaa kwa wananchi wako na nchi kwa ujumla. Najua unasoma uzi huu na umeona watu hapo juu wasivyokuamini wakiamini wewe ni kunguru mwoga. Sasa kazi kwako kutuonesha kuwa hautushiwi nyau. Nakutakia kilalakheri katika hili suala. Ukishindwa omba msaada kwa CDM
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Number four, I know you heard this before
  Never get high on your own supply

  -Notorious B.I.G- Ten Crack Commandments
   
 12. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hadi hapa ubunge 2015 hana
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Wakuu kigwagallah alitudaganya atakuja na hoja binafsi kuhusu ajira kwa vijana akazunguka kwenye vyombo vya habari akapata umaarufu miongoni mwa vijana halafu akaingia mitini akajidai anakaa upande wa madaktari kwenye mgomo wao ghasia akataka amlambe vibao akafyta Mkia Kama mbwa muoga ikaja issue ya zitto na karatasi la kusaini akapotea akiwa anafikiri ataupata uwaziri sasa kaukosa anatuletea maandamano ambayo siku zote yanapigwa na Chama chake anataka kushare machungu yake ya kukosa uwaziri na sisi. Kwa taarifa yake hatuandamani mpaka apate ridhaa ya Chama chake tena barua iwe imesainiwa na nape au mukama
   
 14. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Wana JF kwani nini hoja za mh.Kigwa kwenye maandamano hayo? Ukiwa ndani ya Ccm unapaswa u-behave na ku-act kama chizi vile, ukiwasikiliza tu basi umekwisha. Unatakiwa uwe na misimamo ya nguvu na kusimamia hoja zenye maana kwa nchi na wananchi hata wakikupiga chini unakuwa na following...ukiwa kinyonga utakosa kwa ccm na kwa wananchi na hata ukienda upinzani utakosa heshima...kazi kwako mh!
   
 15. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Unachokisema kipo sahihi sana kwani huyu jamaa bado tunamkumbuka sakata la saini la kumwondoa waziri mkuu. Alifika hapa hapa na kutoa hoja ambazo alipingwa na members wengi tu.Leo anaonekana anataka kugaini popularity, kwani chama chake na wasira wameshasema maandamano si sera yao.Hata huyo katibu tayari anaonesha kugomea maandamano hayo kwa hoja hizo hizo.Simuungi mkono na hayo.
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,450
  Trophy Points: 280
  Mkuu Chikatata, kuna mambo mawili hapo,
  1. Maandamano
  2. Mkutano wa hadhara.

  1.Kwa vile Dr. Kigwa ni mbunge kupitia CCM, jambo lolote atakalofanya jimboni kwake lazima kipate baraka za chama chake. Maadam CCM haijatoa baraka kwa maadamano yale, then maandamamo hayatakuwepo!. Hata kama umechat na Dr kule fb akakuhakikishia maandamano yapo, amekudanganya na kujidanganya!.

  2. Kama ni kweli amekuambia kuwa "chama hakina sababu ya kumzuia na wala hakina uwezo huo" pia atakuwa amekudanganya na kujidanya kwa sababu tayari chama kimeshamzuia na sababu za kumzuia kimezitoa ila ni kweli chama hakina uwezo wa kumzuia, ila chama kimewaandikia jeshi la polisi ambao ndio wenye uwezo wa kumzuia na watatumia uwezo huo kuyazuia maandamano yake, hivyo hayatakuwepo!.

  3. Hilo la kusema kwamba katibu wa ccm wilayani pale amekurupuka kuandika barua ile pia amekudanganya wewe, japo ni kweli barua ile haina nguvu yoyote kisheria, ila imeandikwa kufuatia vikao halali vya ccm wilaya ambavyo Dr. Kigwa ni mjumbe halali wa vikao hivyo!, vinginevyo aseme huyo katibu amejiandikia tuu na vikao hivyo havikuwepo wala havikujadili kuhusu maandamano yake!.

  4. Hata hivyo naomba nikiri wazi Dr. Kigwa ameonyesha ujasiri mkubwa wa kuwatumikia wananchi wake bila kujali chama chake kinataka nini, mgombea ubunge huwa ni mgombea wa chama na anawajibika kwa chama, lakini akishachaguliwa kuwa mbunge ni mtumishi wa wananchi na anawajibika kwa wananchi na sio kwa chama tena, hivyo anachokifanya Dr. Kigwa ndicho sahihi kabisa kinavhopaswa kufanywa na wabunge wote wa kuchaguliwa kwa kuweka mbele maslahi ya wananchi na sio ya chama!.

  5. Kwa mkutano huu, naomba nikiri wazi kuwa Dr. Kigwa anajiunga na timu ya kina Deo Filikunjombe kusimama kuhesabiwa na 2015 ataendelea kuwa mbunge wa Nzega kwa sababu ameweza kuona mbali!. Bashe ndie aliyekuwa kipenzi cha wana Nzega, baada ya kupigwa zengwe, na baadaye kusafishwa, Dr. Kigwa ameshaona picha ya 2015 na kujua there is no way CCM itamsimamisha kwa sababu kipenzi chao Bashe ameshakuwa cleared, hivyo dawa pekee ya kusurvive ni kuachana na CCM na kuivest kwenye wananchi ndio maana barua yake ya maandalizi ya mkutano hakuipitishia CCM I doubt kama hata vikao vya CCM wilaya anahudhuria!.

  Wabunge wenye akili ni wale wanaojua kutazama mbali, 2015 jahazi la CCM linazama, wabunge wa CCM ambao wanaitegemea CCM kuwaokoa, watazama nayo, na wale wenye akili, wana invest on people na ndio watakao waokoa kiukweli, not CCM anymore!.

  Wish you all the best Dr. Kigwa!.

  Paskali
   
 17. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu pasco umesahau kigwagallah ali invest ccm kwenye saini za zitto kwa kutegemea uwaziri huwezi kumlinganisha na deo filikunjombe hata Mara moja na pale ndio dr alikosea vibaya mno sasa hivi kurudisha Imani kwa wananchi lazima bungeni atete vitu vizito na avisimamie kiasi cha kufukuzwaa na bi kiroboto ili ahit tittle za magazeti vinywa vya watu Pamoja na hapa jf
   
 18. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,950
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  mbona unatumia nguvu nyingi, umelipwa? Yeye ni member si aje?
   
 19. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hawezi kufanya maandamano bila baraka za chama chake atakuwa anaudanganya umma.Tusubiri tuone maana naye ni ngamba lililo ng'ang'ania
   
 20. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Anacheza na magamba watamtoa kafara
   
Loading...