engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,150
- 1,437
- Thread starter
- #21
Kuna mambo mengi sana kuhusiana na huu mgodi wa Golden Pride ambayo wapiga kura wa Nzega wamekuwa wakiyalalamikia kwa zaidi ya miaka kumi na tatu sasa, na haya mambo yanajulikana kila ngazi ya watendaji wa serikali na hakuna jitihada za kuyatatua...mimi Muwakilishi wao nimeamua kuyafuatilia na kwa hakika sintowaangusha wanaNzega wenzangu...nitayafuatilia mpaka pale nitakapoona yanatatuliwa la sivyo hapatatosha Bungeni!
Hivi juzi, baada ya utafiti wa muda mrefu, nimekabidhi kwa Katibu wa Bunge kusudio la kuliomba Bunge lipitishe azimio la kuufunga mgodi huo kwa kuwa hauna manufaa kwa Taifa, pamoja na mambo mengine mengi!
Kuleta mapinduzi ya kifikra siyo lazima uwe upinzani; wengine tunaamini katika kuleta mabadiliko 'from within the system' na there is plenty you are yet to see from people like me...naanza na hili na kuna mengi yapo njiani! Na siyo lazima kila mtu mwenye fikra mbadala basi ajiunge na CHADEMA...
Stay put,
HK.
kama Mwalimu alivyosema kuwa upinzani wa kweli ni lazima utokee ndani ya CCM. Nami naamini huenda ipo siku baadhi ya wana CCM wataona na kuyakataa maovu haya ambayo yanatia aibu taifa letu.
Tatizo kubwa ambalo watanzania tunalo ni kukosa moyo wa uzalendo, utaifa na mawazo ya kujenga future ya nchi kama Tanzania. Kama tungekuwa na moyo huu si rahisi kuingiza nchi mikataba ya kuua kabisa nchi.
mapinduziiii daimaaaaaa:clap2: