Kigwangalla adai mkataba wa mgodi anajitakia mema kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigwangalla adai mkataba wa mgodi anajitakia mema kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by engmtolera, Dec 24, 2010.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ndugu wana jf

  MBUNGE wa Jimbo la Nzega [CCM] Dk Hamisi Andrea Kigwangalla ameiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumpatia mkataba wa mgodi wa dhahabu uliopo Nzega wa Golden Pride Project unaoendeshwa na kampuni ya Resolute[T] Limited.


  Kigwangalla alitoa waraka huo baada ya kuona wananchi wa Wilaya ya Nzega kwa ujumla wakikosa faida ya mgodi huo mkubwa wa dhahabu.

  mimi naamini kuwa huo mkataba utakuwa ni wa kifisadi tuuuuuuu na Mh mbunge hawezi pewa mkata kama anavyohitaji

  swali nalojiuliza hapa ni kuwa je Mh amejizatiti kupambana na mafisadi walioingia mkataba huo?

  Je mheshiwa kwa kuomba mkataba huo, anajitakia mema kweli ndani na nje ya chama chake?


  mapinduziiiiiii daimaaaaaaaaa :target::target:
   
 2. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tatizo viongozi wenzake wana mtazamo tofauti (upeo mdogo au 10%) kuhusu suala lenyewe...

  (source:
  Habarileo)

  Uongozi wa mgodi wa Resolute wasifiwa

  Imeandikwa na Lucas Raphael, Nzega; Tarehe: 24th January 2011 @ 23:50 Imesomwa na watu: 17; Jumla ya maoni: 0  MKUU wa Wilaya ya Nzega, Florence Nholombe amesema Serikali ya Wilaya ya Nzega inatambua umuhimu wa mgodi wa madini ya dhahabu wa Resolute kutokana na umuhimu wake kwa wananchi.

  Alisema michango ya mgodi huo imeleta changamoto kubwa chanya zikiwa zinaonekana pande mbalimbali wilayani hapa.

  Nholombe alisema hayo juzi katika sherehe za kumuaga meneja wa mgodi huo, Los Campbell ambaye amemaliza muda wake wa kazi mgodini humo.

  Nholombe alisema mgodi huo ni moja ya taasisi muhimu wilayani hapa ambayo inayochangia maendeleo kwa wingi katika jamii inayozunguka mgodi huo.

  Alitaja sehemu zilizosaidiwa na mgodi huo kuwa ni elimu katika ujenzi wa madarasa, afya katika kutibu magonjwa sugu kama fistula kwa kina mama na kiuchumi katika kutoa ajira kwa vijana pamoja na ulinzi ambapo hivi karibuni kituo cha Polisi kilichojengwa kwa msaada wa mgodi huo kitafunguliwa.

  Mkuu huyo wa wilaya aliutaka uongozi wa mgodi huo ukiongozwa na Les Taylor kupuuza kauli zinazosikika na baadhi ya viongozi juu ya utendaji kazi wa mgodi huo.

  ’’Nawashukuru sana watu wa Resolute kwa kile mnacho kifanya katika uchangiaji maendeleo kwa Wilaya ya Nzega, endeleeni na moyo huo huo ili tujenge Nzega mpya,” alisema mkuu huyo wa wilaya.

  Naye Diwani wa kata ya Nzegandogo, Nasra Ally alikiri kuwepo kwa uhusiano kati ya maendeleo ya nyanja mbalimbali na uwepo wa mgodi huo wa dhahabu.

  Nasra alisema mgodi huo ni chanzo kikubwa cha maendeleo katika maeneo yanayozunguka mgodi, tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya viongozi wilayani hapa.
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Walokupa huo ubunge ndio wamiliki wa hiyo mikataba.... sasa unawavuta sharubu, jiandae kumwagwa wakiona unawazidi kasi :kev:!!!!!!!
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nilikua na wasiwasi sana na hamisi... lakini its a good move!

  Ila wasiwasi wangu ni mmoja tu, watamuita, watamkanya na kumpa kipande cha keki (si ajabu ameshanusa hilo); kesho unaweza usimsikie tena akihoji... tena ukizingatia aliingia kwenye race akiwa wa tatu kura za maoni

  CCM ni balaa
   
 5. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mwambieni hawezi kudai akiwa huko labda aje huku CDM,hawakawii kumpiga zengwe,kama anaendelea kuwepo huko kwenye hicho chama sharti atii wamiliki wa chama na si wananchi
   
 6. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #6
  Jan 29, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kuna mambo mengi sana kuhusiana na huu mgodi wa Golden Pride ambayo wapiga kura wa Nzega wamekuwa wakiyalalamikia kwa zaidi ya miaka kumi na tatu sasa, na haya mambo yanajulikana kila ngazi ya watendaji wa serikali na hakuna jitihada za kuyatatua...mimi Muwakilishi wao nimeamua kuyafuatilia na kwa hakika sintowaangusha wanaNzega wenzangu...nitayafuatilia mpaka pale nitakapoona yanatatuliwa la sivyo hapatatosha Bungeni!

  Hivi juzi, baada ya utafiti wa muda mrefu, nimekabidhi kwa Katibu wa Bunge kusudio la kuliomba Bunge lipitishe azimio la kuufunga mgodi huo kwa kuwa hauna manufaa kwa Taifa, pamoja na mambo mengine mengi!

  Kuleta mapinduzi ya kifikra siyo lazima uwe upinzani; wengine tunaamini katika kuleta mabadiliko 'from within the system' na there is plenty you are yet to see from people like me...naanza na hili na kuna mengi yapo njiani! Na siyo lazima kila mtu mwenye fikra mbadala basi ajiunge na CHADEMA...

  Stay put,
  HK.
   
 7. D

  Deo JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,190
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Tunakutakia kazi njema na Mungu awe pamoja nawe. Tutafuata maneno na matendo yako katika hili.

  Mikataba yote hii ya madini msingi wake ni Mkapa na Chenge, hakuna hata mmoja wenye manufaa. Wajibu wa maendeleo ya jamii siyo makapuni haya bali ni serikali. Vipengele vya hisani ya huduma ya jamii ni wizi tu. Hawa wanatoa msaada mdogo sana na kupiga bigula kwamba wamesaidia.

  Kaza mwendo ndugu yangu, tu pamoja.
   
 8. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,635
  Likes Received: 1,409
  Trophy Points: 280
  huu mkataba si umebakiza miaka miwili uishe au kumbu kumbu zangu zinanidanganya?:coffee:
   
 9. Titans

  Titans JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 867
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 180
  roger that,u can't bring changes within ccm if u are not from the outside it.
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hongera mbunge wetu, fanya kazi kwa ajili ya wananchi wako na taifa...

  Kinachotakiwa ni utekelezaji wa sera za ccm kwa bidii kwa faida ya nchi.
   
 11. m

  mubi JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2011
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Dk, baada ya kuufunga, unaplan gani za kulisaidia Taifa au Wana nzega mgodi huo uwe na faida kwa Wana nzega na Watanzania kwa ujumla?
   
 12. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #12
  Jan 29, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  @Samora10, hawa jamaa wamekuwa na historia ya kurefusha kitu wanachokiita 'mine life' na wamekuwa wakisema kila siku kwamba mgodi utafungwa soon...maybe baada ya miaka miwili...na ikikaribia kufika wanasogeza mbele...kila siku wanafanya utafiti na kugundua mahala kwenye dhahabu nyingi zaidi ya pale pa jana, na mwaka 2006 waliongeza kiwango cha uzalishaji per day ili wavune ndani ya muda mfupi zaidi...hivi ni kweli 6 years later wanaweza kuwa tayari kufunga mgodi?

  Hata hivyo hoja yangu ina options nyingi, moja kubwa ikiwa kuwataka wa-renegotiate mkataba na serikali yetu, watupe share/waongeze mrahaba na walipe kodi ipasavyo...maana katika miaka yote hiyo zaidi ya 13 wameanza kulipa kodi (corporate tax) mwaka 2009............(toka mgodi huo ufunguliwe mwaka 1999!!!!!!!!!!!!) - WAKIMAANISHA NDIPO WALIPOANZA KUTENGENEZA FAIDA KWENYE BIASHARA YAO!
   
 13. christopher t

  christopher t Member

  #13
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aaah jamani,dogo alishinda kwani ndio maana ccm ililiona hilo ikarudisha jina lake na akawapiga chini wapinzani,hivyo yuko fiti.chapa kazi tunaamini mabadiliko sio lazima yatokane na wapinzani tunaweza kufanya na kwa kiasi kikubwa tukiwa ndani ya chama kwani ni rahisi sauti yako kusikika kuliko ya aliyeko nje na siop kila makosa ya kimkataba yana dhana ya ufisadi ndani yake tusiwe na fikra finyu.Nakutakia kila la kheri katika mustakabali ya kuiletea nzega mafanikio ya kutosha naamini unaweza.Mkataba utapatiwa asiwepo wa kukukatisha tamaa awa jamaa wanajiona sasa wao ndio vinara wa siasa za nchi hii hiyo ni ufinyu wa kimtazamo katika siasa na ndio mwanzo wa kushindwa,wasikukatishe tamaa big up mbunge.
   
 14. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Nashukuru sana kusikia mkuu mwenyewe ukitolea ufafanuzi suala hili. Naamini kwamba utalifanyia kazi ili uchimbaji huo uweze kuleta tija kwa wilaya na taifa. Mungu akubariki sana.
   
 15. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  dr,
  sina tatizo na maoni yako ila nina mambo mawili, moja ni swali na jingine angalizo. Swali langu ni kuwa hatuwezi kuchimba wenyewe mpaka tuwape wanyonyaji aka wawekezaji?

  Angalizo langu ni kuwa, huwezi kuibadili sisi em ilipofikia. Aidha wataku silence kwa namna fulani au wataku kolimba ukiwazidi mbinu. Sikutishi ila huwezi ibadili sisi em hii....time will prove my words! Sis em have to die!
   
 16. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #16
  Jan 30, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  dr huwezi kusema unauchukia ukatoliki wakati unaendelea kuubusu msalaba wa papa, wewe,mwakyembe,na sitta, kama kweli niwazalendo muda wenu wa kuondoka ccm ndio huu. Hakuna lingine peoples power inachukua nchi muda si mrefu.
   
 17. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #17
  Jan 30, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mimi nikushukuru Mheshimiwa kwani ni viongozi wachache sana ktk hii nchi wanaotumia forum hii kwa majina yao halisi hongera kwa hilo lakini pia nakubaliana na wewe kuwa kuleta mabadiliko sio lazima uwe ndani ya upinzani hata ndani ya ccm mabadiliko yanawenzekana kuletwa kwani tunasema ukitakata kuleta mapinduzi ya kweli ni lazima uwe imara ktk yale unyafikiayo yawe
  wakati natowa mada hii nilikuwa na wasiwasi juu ya fikra hasi zilizopo ndani ya ccm yetu kuwa mtu safi na mpenda maendeleo daima hapendwi na baada ya kuliona hili nikawa na wasiwasi nawe kuwa labda siku zako zitakuwa zinahesabika baada ya kulianzisha hili

  mimi nikupongeze na nikuombe usikatishwe tamaaaaaaaa na wenyechama
  lakini pia nikupongeze kwa kuwa member wa Jf wa mda mrefu kwani nadhani hapa utapata mambo mengi ambayo yanaendelea,na yatakayokuja mbele yetu na itakuwia raisi kutambuwa nini kitajili baada ya hapa  mapinduziiiiiiii daimaaaaaaaa:clap2::coffee:
   
 18. Masakata

  Masakata JF-Expert Member

  #18
  Jan 30, 2011
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Kwanza nikushukuru Eng Mtolera kwa kuleta hii topic,so interesting,.

  Pili nimpongeze mh dr Hamic kwa kujitokeza jamvin, ila nami nilikuwa na maswali kwake yafuatayo kati yake na DC wake na diwani wake nani MKWELI, mana hawa wanasema ule mgodi una manufaa makubwa kwa jamii ya wananzega, pili kwenye hili, yupo nani nyuma yake, chama, serikali or wananchi

  Tatu anajua hao Resolute walikichangia chama CCM kiac gan kwenye kampen?

  Nne amesema hao jamaa wamekuwa kigeugeu kwenye life span ya mgodi, anajua kwanini, nani anawapa power hiyo?

  Ushauri wangu kwa Hamis: Hiyo vita ni kubwa kuliko unavyofikiri,cha msingi huko bungen ibane govt itekeleze kwa vitendo mapendekezo yote ya judge Bomani, pili ungepata msimamo wa chama hata ngaz ya wilaya juu ya hili suala,..na mwisho mtu kuwa mpinzani sio DHAMBI!
   
 19. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #19
  Jan 30, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  acheni unafiki elingmtore na kupongezana kijinga hakuna mapinduzi ndani ya ccm ni uongo mtupu huyo mbunge anatafuta cheap popularity hapa jf kupitia mgodi,atueleze msimamo wake kuhusu dowans, epa, ndege ya rais, matumizi mabaya ya mkwere, rostam aziz na ufisadi papa wake. Utawadanganya watoto wenzako ila wewe mbunge unapinga kipindupindu wakati unaishi dampo la uchafu CCM. Pumbafu.
   
 20. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #20
  Jan 30, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hili ndilo tatizo tulilonalo baadhi ya wana jf,mda mwingi hatuamini kile kinachofanywa na baadhi ya wanaccm,umefika wakati wa kuweka ushabiki nyuma na kuwapa moyo wale wanaojaribu kudiliki kufanya jambo fulani,najuwa ukitakacho mkuu,unahitaji tumtukane MBUNGE na tusimpe moyo wala kumpa nguvu kwa kile alichokianzisha kwa kuwa ni mbunge wa ccm nasema NO kwa hili

  hata kama huikubali kambi usinyeeeee mlangoni ipo siku utapita ktk huo mlango

  mimi ninatabia tofauti kidogo na wewe mkuu,huwa napenda kumpa mtu moyo na nguvu kwa udiliki wake kwani naelewa ktk ccm ni vigumu sana hata kuanza kuongelea kile ambacho kinawagusa wakubwa,lakini Dr kajaribu mpe sifa yake usiwe ni mtu wa FIKRA MGANDO mda wote hata kwa yale mema wafanyayo wengine hususani wale wasio ktk bega lako la kulia

  KWA MTINDOOOOO HUUUU HATUTAFIKA,HATA CDM IKIWA MADARAKANI,KWANI NI VIGUMU SANA KUWARIDHISHA WATU WA KADA YAKO


  mapinduziiiiii daimaaaa:clap2::first:
   
Loading...