Kigugumizi (Stuttering): Chanzo na Tiba kwa watu wazima na watoto

Usiwe na shaka sana ndugu hali hiyo inawezakwisha automatically, nami ni muathirka wa hili... Nakumbuka nikiwa mdogo binamu yangu wa kike alikuwa ni mzuri kwa umbo pia alikuwa na kigugumizi na aliongea kwa mkato mkato. Mie kwa akili za utoto nikavutiwa sana na hali ile. Nikaiga kila alivyokuwa anaongea, baadae nami nikawa na kigugumizi kikubwa(cha kujitakia kabisa).

ATHARI:
1. Hujenga hali ya kutojiamini kwa muathirika hii inatokana na kunyimwa nafasi ya kujieleza ya kutosha kutokana na kutumia muda mwingi katika kutamka maneno.
2. Huwa na asira za mara kwa mara kwa kuhisi kuwa anapuuzwa.
3. Anapokuwa kwenye excitiment yeyote/planning for response(anapotumia muda mwingi kujiandaa kuelezea kitu cha baadae huwa taabu kwelikweli nk)

NOTE: Binafsi hivi sasa naichukia sana hali hii.

MAMBO YA KUFANYA:
1. Mzazi/Mlezi mpe nafasi ya kutosha kijana wako ya kujieleza japo atatumia muda mrefu(hii hutufanya tuhisi tunathaminiwa)
2. Usimkate kilimi anapoongea.
3. Kama inawezekana anapoongea usimpuuze mkazie macho hadi atapomaliza kuongea.
4. Kama itatokea akashindwa kutaja baadhi ya maneno kwa wale wenye kigugumizi kikali na kupiga ngumi ukutani/mguu chini msaidie katika kutamka maneno husika.
5. Mpe muda mrefu sana wa kuongea au kuimba mf: kwaya kanisani/kaswida msikitini nk kuliko kukaa kimya.
Siku zote mshauri kuongea taratibu kwa kupumzika, anapokuwa na hasira/furaha ya ghafla asiongee hadi hasira/furaha ishuke.
6. Asichekwe anapoongea kwani hali hii humfanya kukaa kimya muda mrefu hatimae hali huwa mbaya zaidi.

TAHADHARI:
Kigugumizi ni chepesi kweli kweli kuigika, kama utaona watoto wadogo wanajaribu kumuiga mtu yeyote wa karibu mwenye kigugumizi waeleze kwa upole na mara kwa mara madhara yake.

NINA HUSHUHUDA KWA HILI: Jirani yangu mmoja alikuwa na kigugumizi kikali na wadogo zake wawili wakatokea kumuiga kaka yao, hivi sasa wote watatu wameathirika kwa hilo. Ahsante.
 
for my experience,kigugumizi kinapungua kadri mtoto anavyozidi kukua ikiwa tu hatakutana na mazingira ya kumuharibu kisaikolojia kama kukaripiwa mara kwa mara,kuchekwa au kutengwa kw kifupi huyo mtoto anahitaji upendo wa hali ya juu na automatically kigugumizi kitaisha,usihofu mpendwa mshukuru mungu kigugumizi sio kilema
 
Jinsi ya Kukabiliana na Kigugumizi

"Ninaposhikwa na kigugumizi, mimi huwa na wasiwasi, na hilo hunifanya niwe na kigugumizi hata zaidi. Ni kana kwamba nimo ndani ya shimo refu na siwezi kutoka. Wakati mmoja nilienda kumwona mwanasaikolojia fulani. Aliniambia kwamba ninahitaji kuwa na rafiki wa kike-nifanye ngono ili nijiheshimu zaidi! Bila shaka sikurudi tena kwake. Ninataka tu watu wanikubali jinsi nilivyo."-Rafael, mwenye umri wa miaka 32.

HEBU wazia hali ingekuwaje ikiwa kununua tu tiketi ya basi kungekufanya utokwe na jasho, na unapozungumza mara nyingi unashindwa kukamilisha maneno fulani na unajirudia-rudia. Watu milioni 60 hivi ulimwenguni pote, yaani mtu 1 kati ya watu 100, wanakabili hali hiyo kwa sababu wana kigugumizi. Mara nyingi, wao hudhihakiwa na kubaguliwa. Hata huenda wakaonwa kuwa wajinga kwa sababu wao hubadili maneno magumu na kutumia rahisi ambayo wanaweza kutamka.

Ni nini husababisha kigugumizi? Je, tatizo hilo linaweza kutibiwa? Mtu mwenye kigugumizi anaweza kufanya nini ili kuboresha ufasaha wake?* Watu wengine wanaweza kusaidia jinsi gani?

Je, Tunajua Kisababishi?

Watu fulani walioishi nyakati za kale waliamini kwamba kigugumizi kilisababishwa na roho waovu ambao walihitaji kuondolewa. Wakati wa Enzi za Kati, watu walidhani kwamba ulimi ndio uliosababisha kigugumizi. Kwa hiyo, walitumia "dawa" gani? Vyuma vyenye moto na vikolezo! Katika karne zilizofuata, madaktari wapasuaji walikata mishipa na misuli ya ulimi na hata kuondoa tezi za kooni ili kutibu kigugumizi. Lakini njia hizo zote hazikufua dafu.

Utafiti wa kisasa unaonyesha kwamba huenda kigugumizi kikasababishwa na mambo kadhaa. Kisababishi kimoja kinaweza kuwa jinsi mtu anavyotenda anapokuwa chini ya mkazo. Huenda pia mtu akarithi tatizo hilo, kwa kuwa asilimia 60 hivi ya watu walio na kigugumizi wana watu wa ukoo walio na tatizo hilo. Isitoshe, eksirei za mfumo wa neva zinaonyesha kwamba ubongo wa mtu mwenye kigugumizi huchanganua lugha katika njia tofauti. "Huenda watu fulani wakaanza kuzungumza kabla ya ubongo wao kuwaambia jinsi maneno yanavyopaswa kutamkwa," anasema Dakt. Nathan Lavid katika kitabu chakeUnderstanding Stuttering.*

Hivyo, kigugumizi si tatizo la kiakili hasa kama ilivyodhaniwa hapo awali. Kitabu No Miracle Cures kinasema hivi: "Kigugumizi si tatizo linalosababishwa na ukosefu wa ujasiri, na huwezi kumchochea mtu aache kugugumiza." Hata hivyo, watu wenye kigugumizi wanaweza kuwa na matatizo ya kihisia kwa sababu ya hali hiyo. Kwa mfano, huenda wakaogopa hali fulani kama vile, kuzungumza hadharani au kwenye simu.

Msaada kwa Walio na Kigugumizi

Jambo la kushangaza ni kwamba watu wenye kigugumizi wanaweza kuimba, kunong'ona, kujizungumzia au kuzungumza na wanyama wao vipenzi, kuzungumza wakati uleule na wengine, au kuwaiga wengine bila tatizo lolote. Isitoshe, asilimia 80 ya watoto wenye kigugumizi huacha kuwa na tatizo hilo bila kutibiwa. Namna gani hiyo asilimia 20 inayosalia?

Leo kuna matibabu ya kuwafunza watu kuzungumza kwa ufasaha zaidi. Mbinu fulani zinahusisha kulegeza taya, midomo, na ulimi na kupumua kutoka kwenye kiwambo. Pia wagonjwa wanaweza kufundishwa kuvuta pumzi kwa kiasi kidogo kutoka kwenye kiwambo na kisha kupumua polepole wanapozungumza. Pia, wanaweza kutiwa moyo kuvuta vokali na konsonanti fulani wanapozungumza. Mgonjwa huanza kuzungumza haraka kadiri ufasaha wake unavyoboreka.

Mtu anaweza kujifunza ustadi huo kwa saa chache tu. Lakini kutumia mbinu hizo kwa mafanikio chini ya hali zenye mkazo sana huenda kukahusisha kufanya mazoezi kwa saa nyingi sana.

Mazoezi hayo yanapaswa kuanza mtu akiwa na umri gani? Je, inafaa kungoja hadi mtoto aache tatizo hilo bila msaada wowote? Takwimu zinaonyesha kwamba watoto wasiozidi asilimia 20 hupona bila msaada hata ikiwa wamekuwa na kigugumizi kwa miaka mitano. "Kufikia umri wa miaka sita," kinasema kitabu No Miracle Cures, "yaelekea mtoto hawezi kupona tatizo hilo bila msaada."

Hivyo, "watoto walio na kigugumizi wanapaswa kupelekwa kwa mtaalamu wa usemi na lugha haraka iwezekanavyo," kitabu hicho kinaongezea. Kati ya asilimia 20 ya watoto ambao huendelea kuwa na kigugumizi hata wanapokuwa watu wazima, inakadiriwa kwamba asilimia 60 hadi 80 kati yao hupona wanapopata msaada wa kuwasaidia kuzungumza kwa ufasaha.*

Ona Mambo Kihalisi

Mtaalamu wa usemi Robert Quesal, ambaye pia ana kigugumizi, anasema kwamba chini ya hali zozote zile, mtu mwenye kigugumizi hapaswi kujiwekea mradi wa kuzungumza kwa ufasaha kabisa. Rafael, ambaye alitajwa mwanzoni mwa habari hii, hajafaulu kushinda tatizo hilo kabisa, ingawa ameboresha ufasaha wake.

Anasema hivi: "Ninakuwa na kigugumizi zaidi ninaposoma au kuzungumza mbele za watu au ninapokuwa na mtu wa jinsi tofauti ambaye ni mrembo. Nilikuwa mtu mwenye wasiwasi sana kwa sababu watu walinidhihaki. Hata hivyo, siku hizi, nimekubali hali yangu na sijifikirii sana. Sasa neno fulani likinifanya nishikwe na kigugumizi, nyakati nyingine mimi hucheka, kisha ninajaribu kutulia na kuendelea kuzungumza."

Maneno hayo ya Rafael yanapatana na maelezo ya Shirika la Kuzuia na Kutibu Kigugumizi la Marekani kwamba "kushinda tatizo la kigugumizi mara nyingi huhusisha kushinda woga wa kuwa na kigugumizi badala ya kujitahidi sana kuacha kugugumiza."

Watu wengi hawajaruhusu tatizo hilo liwazuie kuwa na maisha yenye kusudi. Hata baadhi yao wamekuwa watu mashuhuri kama vile, mwanafizikia Sir Isaac Newton, mwanasiasa Mwingereza Winston Churchill, na mwigizaji Mmarekani James Stewart.

Wengine wamejifunza ustadi ambao hauhusishi kuzungumza, kama vile kucheza ala fulani, kuchora, au kujifunza lugha ya ishara. Watu wanaozungumza bila kugugumiza wanapaswa kuthamini jitihada nyingi za wale walio na kigugumizi. Hivyo, na tuwatie moyo na kuwategemeza kadiri tunavyoweza.

Zaidi ya asilimia 80 ya watu walio na kigugumizi ni wanaume.

Ingawa maoni mbalimbali kuhusu visababishi na matibabu yanayofaa ya kigugumizi yanafanana, hayapatani nyakati zote. Gazeti Amkeni! halipendekezi maoni au matibabu yoyote hususa.

Katika visa fulani, huenda wataalamu wakapendekeza kifaa fulani cha kuzuia kigugumizi ambacho hufanya sikio lichelewe kusikia.

UNAWEZA KUMSAIDIA JINSI GANI MTU ALIYE NA KIGUGUMIZI?

● Msaidie atulie, na kustarehe. Maisha ya leo yenye hekaheka nyingi na mkazo mara nyingi hufanya tatizo hilo liwe baya zaidi.

● Badala ya kumwambia mtu mwenye kigugumizi azungumze polepole, mwekee mfano kwa kuzungumza polepole. Msikilize kwa subira. Usimkatize. Usimalizie sentensi anazosema. Tua kabla ya kujibu.

● Epuka kumchambua na kumrekebisha. Onyesha kwamba unapendezwa na anachosema kwa maneno yako, kwa kumtazama, na kwa ishara zako za uso na mwili. Usikazie fikira jinsi anavyozungumza.

● Hupaswi kuogopa kuzungumzia tatizo lake. Kutabasamu kwa njia ya kirafiki na kuzungumzia tatizo lake, kutamsaidia mtu mwenye kigugumizi kujihisi huru. Huenda ukasema: "Nyakati nyingine si rahisi kusema tunachotaka kusema."

● Zaidi ya yote, mhakikishie kwamba unamkubali jinsi alivyo.

"POLE KWA POLE NILIACHA KUWA NA KIGUGUMIZI"

Víctor, ambaye amekuwa na kigugumizi kwa miaka mingi wakati familia yao ilipopatwa na mkazo mwingi, alishinda tatizo hilo bila matibabu yoyote. Akiwa Shahidi wa Yehova, alijiandikisha kwenye Shule ya Huduma ya Kitheokrasi, ambayo hufanywa kila juma katika kila kutaniko. Ingawa shule hiyo haijakusudiwa kutoa matibabu ya usemi, imewasaidia wanafunzi kuboresha uwezo wa kuzungumza na kupata ujasiri.

Kitabu Faidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi hutumiwa katika shule hiyo. Chini ya kichwa, "Kukabiliana na Kigugumizi," kitabu hicho kinasema: "Ni muhimu kuendelea kujaribu. . . . Kama una mgawo wa kutoa hotuba, tayarisha vizuri. Fikiria sana jinsi utakavyoitoa. . . . Ukikwama unapoongea, jaribu kwa kadiri unavyoweza kudumisha utulivu wa sauti yako na hali yako. Legeza misuli ya utaya wako. Tumia sentensi fupi-fupi. Epuka kutumia maneno kama ‘mmh' na ‘eeh.'"

Je, shule hiyo ilimsaidia Víctor? Anasema hivi: "Kukazia fikira kile ambacho ningesema, na si jinsi ambavyo ningezungumza, kulinifanya nisahau kwamba nina tatizo. Pia, nilifanya mazoezi sana. Pole kwa pole, niliacha kuwa na kigugumizi."
 
Aisee kweli kabisa mie nina kigugumizi ni noma. Napiga watu vibuti kila saa halafu nikikata simu naanza kuhuzunika mwenyewe the the mpaka baby ananiambia ww una majini si bure. Ngoja niicopy hii thread na comment zake nimtumie apate darasa.

Na shule balaa yaani nina miakili noma mpaka chuo namaliza watu hawakuwa wakiamini kama nitamaliza group langu wote walidisco halafu sasa nilikuwa bangi mtu.

The teh likija pepa ninashika namba kama kawa.Vijana wakawa wanajua nanunua paper kumbe mwenzao Financial Account naisoma nusu saa nimeua kila kitu naenda kupuliza ganja nikirudi ni kulalatu naingia kwenye paper wa mwisho natoka wa kwanza kama sijalala kabisa.

Mleta mada nakumbuka when I was young kuongea sijui kabisa mpaka nigonge miguu chini wakawa wananitania kuwa watafunika ungo ili nisiongee kabisa.

Pia mie ni mkorofi noma ngumi nje nje primamry na O level nlikuwa napigana kila siku. Ha ha poor me nlikuwa nadundwa kila siku as nilikuwa sina nguvu.

Sasa hivi ninacho ni kikali balaa japo najitahidi kukicontol si unajua ukubwa dawa
!
 
Heshima Mbele Wadau, nina mtoto wangu anasumbuliwa na kigugumizi kwa muda sasa, tagu azaliwe amekuwa na tatizo hili na anapata shida sana wakati wa kuongea, umri wake ni miaka 3.

naombeni msaada, kama kuna mwana JF anayefahamu namna au dawa ya kutatua tatizo hili.
 
Hilo ni tatizo la kurithi na halina dawa za kutibu ila imeandikwa "wenye vigugumizi watanena barabara" piga maombi hapo kwa imani
 
Jinsi ya Kukabiliana na Kigugumizi

"Ninaposhikwa na kigugumizi, mimi huwa na wasiwasi, na hilo hunifanya niwe na kigugumizi hata zaidi. Ni kana kwamba nimo ndani ya shimo refu na siwezi kutoka. Wakati mmoja nilienda kumwona mwanasaikolojia fulani. Aliniambia kwamba ninahitaji kuwa na rafiki wa kike-nifanye ngono ili nijiheshimu zaidi! Bila shaka sikurudi tena kwake. Ninataka tu watu wanikubali jinsi nilivyo."-Rafael, mwenye umri wa miaka 32.

HEBU wazia hali ingekuwaje ikiwa kununua tu tiketi ya basi kungekufanya utokwe na jasho, na unapozungumza mara nyingi unashindwa kukamilisha maneno fulani na unajirudia-rudia. Watu milioni 60 hivi ulimwenguni pote, yaani mtu 1 kati ya watu 100, wanakabili hali hiyo kwa sababu wana kigugumizi. Mara nyingi, wao hudhihakiwa na kubaguliwa. Hata huenda wakaonwa kuwa wajinga kwa sababu wao hubadili maneno magumu na kutumia rahisi ambayo wanaweza kutamka.

Ni nini husababisha kigugumizi? Je, tatizo hilo linaweza kutibiwa? Mtu mwenye kigugumizi anaweza kufanya nini ili kuboresha ufasaha wake?* Watu wengine wanaweza kusaidia jinsi gani?

Je, Tunajua Kisababishi?

Watu fulani walioishi nyakati za kale waliamini kwamba kigugumizi kilisababishwa na roho waovu ambao walihitaji kuondolewa. Wakati wa Enzi za Kati, watu walidhani kwamba ulimi ndio uliosababisha kigugumizi. Kwa hiyo, walitumia "dawa" gani? Vyuma vyenye moto na vikolezo! Katika karne zilizofuata, madaktari wapasuaji walikata mishipa na misuli ya ulimi na hata kuondoa tezi za kooni ili kutibu kigugumizi. Lakini njia hizo zote hazikufua dafu.

Utafiti wa kisasa unaonyesha kwamba huenda kigugumizi kikasababishwa na mambo kadhaa. Kisababishi kimoja kinaweza kuwa jinsi mtu anavyotenda anapokuwa chini ya mkazo. Huenda pia mtu akarithi tatizo hilo, kwa kuwa asilimia 60 hivi ya watu walio na kigugumizi wana watu wa ukoo walio na tatizo hilo. Isitoshe, eksirei za mfumo wa neva zinaonyesha kwamba ubongo wa mtu mwenye kigugumizi huchanganua lugha katika njia tofauti. "Huenda watu fulani wakaanza kuzungumza kabla ya ubongo wao kuwaambia jinsi maneno yanavyopaswa kutamkwa," anasema Dakt. Nathan Lavid katika kitabu chakeUnderstanding Stuttering.*

Hivyo, kigugumizi si tatizo la kiakili hasa kama ilivyodhaniwa hapo awali. Kitabu No Miracle Cures kinasema hivi: "Kigugumizi si tatizo linalosababishwa na ukosefu wa ujasiri, na huwezi kumchochea mtu aache kugugumiza." Hata hivyo, watu wenye kigugumizi wanaweza kuwa na matatizo ya kihisia kwa sababu ya hali hiyo. Kwa mfano, huenda wakaogopa hali fulani kama vile, kuzungumza hadharani au kwenye simu.

Msaada kwa Walio na Kigugumizi

Jambo la kushangaza ni kwamba watu wenye kigugumizi wanaweza kuimba, kunong'ona, kujizungumzia au kuzungumza na wanyama wao vipenzi, kuzungumza wakati uleule na wengine, au kuwaiga wengine bila tatizo lolote. Isitoshe, asilimia 80 ya watoto wenye kigugumizi huacha kuwa na tatizo hilo bila kutibiwa. Namna gani hiyo asilimia 20 inayosalia?

Leo kuna matibabu ya kuwafunza watu kuzungumza kwa ufasaha zaidi. Mbinu fulani zinahusisha kulegeza taya, midomo, na ulimi na kupumua kutoka kwenye kiwambo. Pia wagonjwa wanaweza kufundishwa kuvuta pumzi kwa kiasi kidogo kutoka kwenye kiwambo na kisha kupumua polepole wanapozungumza. Pia, wanaweza kutiwa moyo kuvuta vokali na konsonanti fulani wanapozungumza. Mgonjwa huanza kuzungumza haraka kadiri ufasaha wake unavyoboreka.

Mtu anaweza kujifunza ustadi huo kwa saa chache tu. Lakini kutumia mbinu hizo kwa mafanikio chini ya hali zenye mkazo sana huenda kukahusisha kufanya mazoezi kwa saa nyingi sana.

Mazoezi hayo yanapaswa kuanza mtu akiwa na umri gani? Je, inafaa kungoja hadi mtoto aache tatizo hilo bila msaada wowote? Takwimu zinaonyesha kwamba watoto wasiozidi asilimia 20 hupona bila msaada hata ikiwa wamekuwa na kigugumizi kwa miaka mitano. "Kufikia umri wa miaka sita," kinasema kitabu No Miracle Cures, "yaelekea mtoto hawezi kupona tatizo hilo bila msaada." Hivyo, "watoto walio na kigugumizi wanapaswa kupelekwa kwa mtaalamu wa usemi na lugha haraka iwezekanavyo," kitabu hicho kinaongezea. Kati ya asilimia 20 ya watoto ambao huendelea kuwa na kigugumizi hata wanapokuwa watu wazima, inakadiriwa kwamba asilimia 60 hadi 80 kati yao hupona wanapopata msaada wa kuwasaidia kuzungumza kwa ufasaha.*

Ona Mambo Kihalisi

Mtaalamu wa usemi Robert Quesal, ambaye pia ana kigugumizi, anasema kwamba chini ya hali zozote zile, mtu mwenye kigugumizi hapaswi kujiwekea mradi wa kuzungumza kwa ufasaha kabisa. Rafael, ambaye alitajwa mwanzoni mwa habari hii, hajafaulu kushinda tatizo hilo kabisa, ingawa ameboresha ufasaha wake. Anasema hivi: "Ninakuwa na kigugumizi zaidi ninaposoma au kuzungumza mbele za watu au ninapokuwa na mtu wa jinsi tofauti ambaye ni mrembo. Nilikuwa mtu mwenye wasiwasi sana kwa sababu watu walinidhihaki. Hata hivyo, siku hizi, nimekubali hali yangu na sijifikirii sana. Sasa neno fulani likinifanya nishikwe na kigugumizi, nyakati nyingine mimi hucheka, kisha ninajaribu kutulia na kuendelea kuzungumza."

Maneno hayo ya Rafael yanapatana na maelezo ya Shirika la Kuzuia na Kutibu Kigugumizi la Marekani kwamba "kushinda tatizo la kigugumizi mara nyingi huhusisha kushinda woga wa kuwa na kigugumizi badala ya kujitahidi sana kuacha kugugumiza."

Watu wengi hawajaruhusu tatizo hilo liwazuie kuwa na maisha yenye kusudi. Hata baadhi yao wamekuwa watu mashuhuri kama vile, mwanafizikia Sir Isaac Newton, mwanasiasa Mwingereza Winston Churchill, na mwigizaji Mmarekani James Stewart. Wengine wamejifunza ustadi ambao hauhusishi kuzungumza, kama vile kucheza ala fulani, kuchora, au kujifunza lugha ya ishara. Watu wanaozungumza bila kugugumiza wanapaswa kuthamini jitihada nyingi za wale walio na kigugumizi. Hivyo, na tuwatie moyo na kuwategemeza kadiri tunavyoweza.

Zaidi ya asilimia 80 ya watu walio na kigugumizi ni wanaume.

Ingawa maoni mbalimbali kuhusu visababishi na matibabu yanayofaa ya kigugumizi yanafanana, hayapatani nyakati zote. Gazeti Amkeni! halipendekezi maoni au matibabu yoyote hususa.

Katika visa fulani, huenda wataalamu wakapendekeza kifaa fulani cha kuzuia kigugumizi ambacho hufanya sikio lichelewe kusikia.

UNAWEZA KUMSAIDIA JINSI GANI MTU ALIYE NA KIGUGUMIZI?

● Msaidie atulie, na kustarehe. Maisha ya leo yenye hekaheka nyingi na mkazo mara nyingi hufanya tatizo hilo liwe baya zaidi.

● Badala ya kumwambia mtu mwenye kigugumizi azungumze polepole, mwekee mfano kwa kuzungumza polepole. Msikilize kwa subira. Usimkatize. Usimalizie sentensi anazosema. Tua kabla ya kujibu.

● Epuka kumchambua na kumrekebisha. Onyesha kwamba unapendezwa na anachosema kwa maneno yako, kwa kumtazama, na kwa ishara zako za uso na mwili. Usikazie fikira jinsi anavyozungumza.

● Hupaswi kuogopa kuzungumzia tatizo lake. Kutabasamu kwa njia ya kirafiki na kuzungumzia tatizo lake, kutamsaidia mtu mwenye kigugumizi kujihisi huru. Huenda ukasema: "Nyakati nyingine si rahisi kusema tunachotaka kusema."

● Zaidi ya yote, mhakikishie kwamba unamkubali jinsi alivyo.

"POLE KWA POLE NILIACHA KUWA NA KIGUGUMIZI"

Víctor, ambaye amekuwa na kigugumizi kwa miaka mingi wakati familia yao ilipopatwa na mkazo mwingi, alishinda tatizo hilo bila matibabu yoyote. Akiwa Shahidi wa Yehova, alijiandikisha kwenye Shule ya Huduma ya Kitheokrasi, ambayo hufanywa kila juma katika kila kutaniko. Ingawa shule hiyo haijakusudiwa kutoa matibabu ya usemi, imewasaidia wanafunzi kuboresha uwezo wa kuzungumza na kupata ujasiri.

Kitabu Faidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi hutumiwa katika shule hiyo. Chini ya kichwa, "Kukabiliana na Kigugumizi," kitabu hicho kinasema: "Ni muhimu kuendelea kujaribu. . . . Kama una mgawo wa kutoa hotuba, tayarisha vizuri. Fikiria sana jinsi utakavyoitoa. . . . Ukikwama unapoongea, jaribu kwa kadiri unavyoweza kudumisha utulivu wa sauti yako na hali yako. Legeza misuli ya utaya wako. Tumia sentensi fupi-fupi. Epuka kutumia maneno kama ‘mmh' na ‘eeh.'"

Je, shule hiyo ilimsaidia Víctor? Anasema hivi: "Kukazia fikira kile ambacho ningesema, na si jinsi ambavyo ningezungumza, kulinifanya nisahau kwamba nina tatizo. Pia, nilifanya mazoezi sana. Pole kwa pole, niliacha kuwa na kigugumizi."cc.@Baba JJ
 
Wadau,

Naomba kujua kitu kinachosababisha tatizo la kigugumizi, kwani mwanangu amepatwa na tatizo la kigugumizi ghafla, yeye ana umri wa miaka mitatu na alikuwa anaongea vizuri bila tatizo.

Je kigugumizi ni ugonjwa au ni nini?
 
Mara nyingi kwa jinsi ulivyo eleza husababishwa na ninyi watu mnao mzunguka. Makaripio ya mara kwa mara na kumkatisha sentence wakati anaongea au kumcheka kwa kuwa mtoto ametamka maneno isivyo sahihi. Hii inamsababishia kuto jiamini na hata kigugimizi.

Hujachelewa, all family members wanapaswa kubadilika na kumfunza mtoto kwa upole na upendo na kwa umri huo mtoto huwa na maswali mengi yajibibiwe kwa ufasaha na ukweli epuka kumdanganya mtoto hata kama ni jambo dogo. Kwa hayo utamuwezesha kujiamini na kigugumizi hakika kitakwisha ndani ya wiki chache tu.
 
Very good piece of advice. Ni kweli kabisa kwamba ni vizuri kuwajengea watoto mazingira ya kuwa huru kujieleza badala ya kumkaripia au kumkatisha anapoongea au anapojieleza. Hali hiyo, ilimkuta mtoto wangu mmoja lakini namshukuru Mungu amepona kabisa.
 
Ni ugonjwa,niliona kipindi kimoja cha therapy ya watu wenye kigugumizi its so amazing….
 
Last edited by a moderator:
Hiyo damage inasabishwa na nini?

Unaweza ukapata ajali au ukaanguka na ubongo sehemu hiyo ya Brocas ikapata damage au pia wakati mtoto anapozaliwa anaweza akapata damage pale pale anapozaliwa au baadae anapoanza kutembea kwasababu huwa wanaanguka sana, na sababu nyingine ni zakitaalamu zaidi.
NB: kuna Brocas aphesia ambayo ni kigugumizi na Wrenickles aphasia unaweza kugoogle ili ukaaelewa zaidi.
 
Kwaiyo Kama Ni Ugonjwa Kinatibika? Ntafurahi Na Bungeni Kupatikane Mwenye Kigugumizi Aingize Miss? Mpaka Bac?
 
man.jpg
-

Kigugumizi chaweza kumkumba yeyote -Watu wengi hupata kigugumizi kwa muda baada ya kuathirika kisaikolojia. Hawa waweza kupata kigugumizi: -Wenye msongo wa mawazo -Waliodhalilishwa ama asiyejiamini

KWA UFUPI

  • Kigugumizi chaweza kumpata yeyote na kumvurugia maisha hata akakosa kazi ama cheo ambacho anakimudu kikamilifu.
Mwanafunzi amechaguliwa na mwalimu kujibu swali. Anafahamu vyema jibu la swali hilo, lakini anapoanza kufafanua, maneno yanampotea; anakwama; anashindwa kumaliza sentensi.

Hali hii inaweza kutokana na baadhi ya alama za herufi katika ufahamu wake kumpotea. Hili linasababisha jibu lake sahihi alilokuwa nalo kichwani kutoeleweka mbele ya mwalimu na wanafunzi wenzake.

Mwanafunzi huyu ana tatizo la kigugumizi ambalo huwaathiri watu wengi wakati wa mazungumzo. Mtu mwenye kigugumizi anaweza kurudia neno au kutamka neno, silabi au kifungu cha neno moja kwa muda mrefu. Huweza pia kusimama ghafla na kupotewa na neno au asitoe sauti kwa baadhi ya silabi.

Ingawa kigugumizi kinaweza kuchukuliwa kuwa tatizo dogo, lisipotafutiwa ufumbuzi linaweza kuharibu vipaji, kuwakosesha watu baadhi ya ajira walizozipenda na hata kuwasababisha wasijiamini na kujisikia kuaibika mbele ya kadamnasi.

Mwanasaikolojia wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Modesta Kimonga anasema kigugumizi ni aina ya ulemavu ambao mtu huweza kuzaliwa nao au kupata ukubwani. “Ni tatizo la kuzaliwa, ni miongoni mwa aina za ulemavu na huweza kumpata mtu katika maisha yake yote,” anasema.

Kwa baadhi ya watu kigugumizi huweza kumpata mtu ukubwani kutokana na matatizo ya kiafya kama kuugua kwa muda mrefu.

“Kigugumizi pia huweza kumpata mtu kwa muda mfupi, kwa mfano kama ana hasira au anahojiwa na watu anaowaheshimu au kuwaogopa,” anasema.

Hata hivyo, Modesta anaeleza kuwa kigugumizi kwa watoto wanaojifunza kuzungumza ni jambo la kawaida kwani wakati huo ubongo wao unakuwa haujashika baadhi ya maneno.

“Watoto wanaweza kutibiwa, lakini kwa watu wazima wenye kigugumizi ni nadra sana kutibiwa,” anasema.

Mfalme mwenye kigugumizi

Mfalme George V1 aliyetawala Uingereza kuanzia mwaka 1895 hadi 1952 alikuwa na kigugumizi. Kutokana na tatizo hilo, alikwepa na alikuwa na hofu kubwa ya kuzungumza mbele ya umma jambo ambalo haliepukiki katika nchi ya kifalme.

Mwaka 1925, kabla ya kuwa mfalme, alitoa hotuba ya kufunga maonyesho ya kitaifa jijini London. Hotuba yake iliwachanganya wengi na kumfedhehesha kiongozi huyo kutokana na kigugumizi na tangu hapo aliamua kumtafuta mtaalamu wa kuzungumza.Wataalamu wa afya wanasema kuwa kigugumizi chaweza kumkumba yeyote endapo atakutana na hali ya msongo wa mawazo au hali ya hofu, kwa mfano kuhojiwa na polisi, kuzungumza na mwanasheria mtundu au unapokuwa shahidi mbele ya mahakama.
Maktaba ya dawa ya Uingereza inaeleza kuwa kigugumizi kinawaathiri mara tatu zaidi wanaume kuliko wanawake.

Mtaalamu wa lugha ya mazungumzo, Anastazia Ayebazibwe wa Chuo Kikuu cha Makerere anasema kuwa mtu mwenye kigugumizi hupatwa na hali ya kushindwa kupumua au kuwa katika wasiwasi wa hali ya juu anapozungumza. Baadhi ya kauli zao hufungwa kabisa wakati wa mazungumzo.

“Pale ambapo midomo yao ipo katika wakati sahihi wa kutamka neno, ghafla neno hilo hufungwa katikati ya mdomo bila kutamkika au kutoa sauti yake. Hali hii inaweza kudumu kwa sekunde kadhaa na kuachia,” anasema.

Wakati mwingine neno linapokwama, mzungumzaji hutafuta neno la kuziba nafasi hiyo kama vile “ammm”, “aaah”, “naaa”, au “eeeeh”.

Aina za vigugumizi

Wengine hushindwa kupumua wakati wa kuzungumza, midomo kutetemeka, taya kutetemeka, kuchanganya maneno, kurudiarudia, maneno kutoka vipande, kusita kabla ya kuzungumza au kushindwa kuanza kutamka neno au sentensi.

Mhadhiri wa taaluma ya mawasiliano wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), David Kiowi anasema kwa asilimia kubwa ya kigugumizi ni tatizo la kurithi.

“Mtu mwenye kigugumizi ni lazima kuna mtu kwenye ukoo ambaye ana tatizo hilo,” anasema.

Anasema ni ulemavu wa kuzungumza na humkumba mtu tangu wakati anapozaliwa na mara chache ukubwani au nyakati fulani katika maisha.

“Kigugumizi ni tatizo la kisaikolojia, pia huhusiana na mawasiliano katika ubongo. Ubongo hutoa tafsiri wakati mtu anapotaka kuzungumza, lakini pia inahusisha pumzi, mdomo na masikio,” anasema.

Anasema lugha ya mazungumzo kwa kawaida huweza kufundishika kulingana na mazingira, lakini kigugumizi si tatizo la kimazingira bali ni urithi, saikolojia na akili. “Ni kwa vile mtu anapozungumza tunaangalia mdomoni tu, lakini wakati mwingine kifua na pumzi huhusika kuchangia kigugumizi,” anasema.
Kuhusu tiba, Kiowi anasema watoto wadogo wanaweza kutibiwa kwa vifaa maalumu ambavyo huwekwa masikioni na huambiwa kutamka maneno kwa kurudia, lakini ni vigumu kutibu tatizo hilo ukubwani.

Sababu za kigugumizi

Wataalamu wa afya wameshindwa kufahamu chanzo hasa cha tatizo hili. Lakini utafiti unaeleza kuwa wengi wenye tatizo hilo wanatoka kwenye familia ambazo zina tatizo la kigugumizi.

Kwa watoto wanaojifunza si jambo la ajabu. Hujikuta wakipata shida kutamka baadhi ya maneno au kurudia neno kwa muda mrefu wakitafuta neno jingine la kuunganisha ili kutunga sentensi. Sababu nyingine ni homa ya uti wa mgongo wakati wa utotoni.

Mishipa ya fahamu

Kigugumizi hutokea wakati taarifa kati ya ubongo, neva za mazungumzo na misuli inaposhindwa kufanya kazi sawasawa. Hali hii huwapata watoto na watu wazima hasa wale ambao wamewahi kupata kiharusi au kuathirika ubongo.

Watu wengi hupata kigugumizi kwa muda baada ya kuathirika kisaikolojia. Kwa mfano mtu mwenye msongo wa mawazo, aliyedhalilishwa, kutojiamini au mwenye wasiwasi huweza kupata kigugumizi.

Kwa mfano watoto wanaotukanwa au kudhalilishwa mara kwa mara hupata kigugumizi wakati wa kuzungumza.

Kwa sababu hiyo, mazingira kama hayo yanapaswa kuepukwa katika jamii.

Chanzo: Mwananchi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom