Kigugumizi (Stuttering): Chanzo na Tiba kwa watu wazima na watoto

Mimi nilizaliwa bila kigugumizi, nilipofika miaka sita nilikwenda kutembea kijijini ambako mtoto nilieishi nae (humo ndani mwao) alikuwa na kigugumizi!

Nilijiskia raha kumuiga na kumuinjoi! Toba yarabi! Si anirukize! Nilijichukia sana, but niliondoka huko na kurudi home, kadiri siku zilivyosonga kilipotea na kupotea! But till today nikikasirika sana maneno yananipotea!
...
Swali kwako Dr MziziMkavu:
Kwanini kigugumizi hakikunipotea moja kwa moja wakati nimeshaanchana na yule kijana miaka mingi?

Na kwa nini kinitokee wakati wa hasira kali tu?
 
Nina mdogo wangu sasa ana miaka 19.

Toka amezaliwa na mpaka ameanza kuongea, lakini alipofikisha umri wa miaka 5, alianza kuongea akiwa na kigugumizi, hadi sasa amekuwa akisumbuliwa.

NAOMBENI USHAURI / DAWA KWA HUYU DOGO
 
Nina mdogo wangu sasa ana miaka 19.

Toka amezaliwa na mpaka ameanza kuongea, lakini alipofikisha umri wa miaka 5, alianza kuongea akiwa na kigugumizi, hadi sasa amekuwa akisumbuliwa.

NAOMBENI USHAURI / DAWA KWA HUYU DOGO
Dawa ya kigugumizi ipo ukitaka nitafute kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano
 
Salama wanaJF,

Nilikuwa nina maswali mawili kuhusu kigugumizi;

1. Napenda kujua hasa ni nini chanzo cha mtu kuwa na kigugumizi au husababishwa na nini hasa
2. Why wanaume wengi ndio huwa na kigugumizi kuliko wanawake, sababu ni nini hasa?

Ni hayo tu..
 
Mkuu naona tayari umepewa ushauri wa kutosha, kwa kuingezea tu ni kwamba usiiendekeze hiyo hali; mwoneshe mtoto kuwa hiyo si hali ya kawaida, mwambie aongee taratibu na akikwama usimsaidie kumalizia neno alilotaka kusema, mwache amalizie mwenyewe.
asioneshe kukasirika ila mwambie kuwa aongee vizuri asije akalemaa(asijihisi kuwa tayari kalemaa).
 
Kwanza kabisa hii dawa ni ya kiimani zaidi. Mimi nilitumia kwa mwanangu na tatizo likaisha. Tiba yake anapewa mtoto ambaye hajavuka miaka 10. Kwa watu ambao wametokea mkoa wa kilimanjoro na Arusha watakuwa mashahidi.

Dawa yenyewe ni hii. Kila baada ya kupika chakula chochote mpe mtoto mwenye tatizo la kigugumizi mwiko alambe.fanya hivi kila siku.

Kiwe kijiko,mwiko, upawa hata kipekecheo.

Nawatakia matibabu mema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom