Ms Judith
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 2,563
- 918
mamamia ametoa mchango mzuri sana na kiresula ufuate huo ushauri utakusaidia sana
mimi binafsi nilikuwa na kigugumizi kikali sana hadi miaka 8. kila nilipokuwa nashindwa kabisa kutamka neno na wenzangu kunicheka nilikuwa nalia sana, nilikuwa najisiakia vibaya na mara nyingi nilikuwa najisikia aibu kuongea mbele ya wenzangu. kwa uzoefu wangu:
1. baadhi ya maneno ni magumu kutamka zaidi ya mengine
2. ukijiandaa kutamka neno huwa kinaongezeka kuliko kutamka bila kujiandaa
3. kutamka pamoja na kuimba (kama alivyofafanua mamamia) kunarahisisha kutamka na kunaweza kufunika kabisa kisionekane
4. mtu akiudhiwa na kukasirika hata kwa kiasi kidogo tu ama akiwa na wasiwasi huongezeka
bahati mbaya sikusoma nursery school na sikuwahi kufundishwa na mwalimu anayejua saikolojia ya watoto wakati wa utoto wangu. namshukuru Mungu nilifanikiwa kufanya mazoezi mawili makubwa na nikakimaliza kabisa hadi leo sina hata kidogo, ooh, glory to God!
mazoezi hayo ni
1. kutamka neno lililokuwa linanitatiza kwa kulirefusha (kulivuta) badala ya kulikata. mfano kutamka neno "mkutano" nilikuwa natamka mkuuuuuutaaaaaano" badala ya "mku mku mku ku ku ta ta ta no" kwa hiyo nilikuwa kama naimba wimbo fulani hivi
2. kuweka kiambishi "a" au "ya" kabla ya neno lenye kutatiza kutamka (na wakati mwingine kukivuta kama nilivyofafanua katika (1) hapo juu kama neno litaendelea kuwa gumu kutamka). mfano neno "mkutano" nilikuwa natamka amkutano" au "yamkutano" au wakati mwingine navuta hivyo viambishi na kutamka aaaamkutano" au "yaaaamkutano"
kwa hiyo mpendwa unaweza kumhsawishi na kumfanyia mazoezi mwanao ajaribu mbinu hii huenda ikamsaidia kama ilivyonisaidia mimi. ila natoa tahadhari kuwa:
1. watu tumetofautiana. kwangu mimi viambishi hivi vya "a" na "ya" vilinirahisishia kutamka neno lolote ambalo lilikuwa linanisumbua. kwa hivyo inawezekana mimi mbinu hii ilinisaidia lakini mwingine isimsaidie.
2. umri wa mtoto waweza kumuwia vigumu kutumia mbinu hii, ila wewe mwenyewe na jamaa zako wengine walio watu wazima mnaweza kujaribu hii mbinu na mnaweza kuondokana na tatiza hili hata huku ukubwani
3. muwe watundu na wadadisi kwa kujaribu viambishi vingine mbalimbali kwani viambishi vilivyonisaidia mimi vinawezaa visiwasaidie nyinyi lakini kukawa na viambishi vingine vyenye msaada kwenu kutegemeana na ndimi zenu. kwa hiyo jaribuni viambishi mbalimbali
kwa haya machache nawaombea faraja na baraka za Mungu
mbarikiwe sana na msife moyo wala kufadhaika,
Mungu anawapenda sana, anawapenda upeo!!