Mwanaume mwenye aibu...

chaukimya

Member
Dec 15, 2023
26
86
Habari?

Wajameni naombeni msaada wa kimawazo. Kuna mwanaume ambaye anaonyesha dalili zote za kunihitaji kwenye mahusiano lakini hawezi kabisa kutamka kuwa ananihitaji anapokuwa hajanywa pombe.
Anapolewa anaweza kuongea chochote na kuahidi kila kitu. Ila pombe zinapomtoka, atabaki kufanya ishara za kawaida, kupiga simu, kutoka out nk ila Hakuna Jambo la kimahusiano mtakaloweza kuongea. Ukimuuliza hata juu ya plan yenu, atatoa ahadi kwamba mtaongea siku ingine ambapo atategemea akilewa ndipo apige sound.
Binafsi nimeshindwa kuelewa. Ninatafsiri kama mtu muongo ndio maana anatafuta confidence kwenye pombe. Ila angekua anatoa majibu toka moyoni, wala asingepata kigugumizi cha kusubiri kuelewa.
Nimeona mambo yasiwe mengi. Nimeamua aachane na Mimi na hadi sasa ameshindwa kuongea lolote. Ila ikitokea amekunywa, anapiga simu na kuanza kujitetea.
Ndugu zangu, mmewahi kukutana na watu wa aina hii? Na je hiki ninachofikiri Mimi kinaweza kikawa tofauti?
Nawasilisha
 
1703624610.png

Muambie atafute hiko kitabu au mnunulie akisome kuanzia mwanzo hadi mwisho, utashangaa matokeo yake, kipo madukani.
Akikisoma akamaliza akashindwa kukupiga mistari ukalainika muuzaji anakurudishia pesa.
 
huyo jamaa nadhani hajakupenda wewe kimapenzi, though anahitaji kampani yako, inawezekana nyie ni marafiki wa muda mrefu hivyo ikapelekea yeye kukuchukulia wewe kama dada yake
Sio kweli. Hao wengi wao ni wale walioluka stage wakati wa kubalehe yaani yale mambo aliyotakiwa kuyafanya hatua za o-level kama kuzoeana na wanawake aliyaluka sasa ndo anakuja kuwa mtu mzima bado muoga wa wanawake hao watu wapo sana sana waliokulia shuleni za bweni za boyz tupu.
 
Uyo mshkaji ni muoga wa wanawake sio kitu kibaya iyo inatokana na namna tulivyolelewa. If you are into him jaribu ku-skip iyo stage ya kutaka akutongoze, tengeneza mazingira ya kuliwa kimasihara. Mkipelekeana moto tayari mahusiano yenu yatakua yameanzia hapo.
 
Habari?

Wajameni naombeni msaada wa kimawazo. Kuna mwanaume ambaye anaonyesha dalili zote za kunihitaji kwenye mahusiano lakini hawezi kabisa kutamka kuwa ananihitaji anapokuwa hajanywa pombe.
Anapolewa anaweza kuongea chochote na kuahidi kila kitu. Ila pombe zinapomtoka, atabaki kufanya ishara za kawaida, kupiga simu, kutoka out nk ila Hakuna Jambo la kimahusiano mtakaloweza kuongea. Ukimuuliza hata juu ya plan yenu, atatoa ahadi kwamba mtaongea siku ingine ambapo atategemea akilewa ndipo apige sound.
Binafsi nimeshindwa kuelewa. Ninatafsiri kama mtu muongo ndio maana anatafuta confidence kwenye pombe. Ila angekua anatoa majibu toka moyoni, wala asingepata kigugumizi cha kusubiri kuelewa.
Nimeona mambo yasiwe mengi. Nimeamua aachane na Mimi na hadi sasa ameshindwa kuongea lolote. Ila ikitokea amekunywa, anapiga simu na kuanza kujitetea.
Ndugu zangu, mmewahi kukutana na watu wa aina hii? Na je hiki ninachofikiri Mimi kinaweza kikawa tofauti?
Nawasilisha
Mwanaume mwenye aibu kwa mwanamke ana vinasaba vya ushoga
 
Back
Top Bottom