TAA na Mussa Mbura tekelezeni maelekezo ya Rais

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,460
1,444
Mimi kama mwananchi Nimekuwa nikifuatilia kwa umakini uboreshaji wa jengo la Abiria la Uwanja wa ndege Mwanza.

Cha kushangaza ahadi na maelezo matamu yamekuwa yakitolewa kila mara kuwa mkataba na kazi itaanza hivi karibuni, lakini imekuwa ni maneno tu bila vitendo mnakwama wapi kiasi cha kumdhalilisha mkuu wa mkoa Amos Makalla kwenye suala hili na Rais,Serikali na wananchi kwa ujumla wake.

Nyinyi ni wataalam hamuoni hali iliyopo Mwanza this is an urgent matter na ni crisis leo hii viwanja muhimu kimkakati vimekamilishwa Mwanza inaonekana kuna kigugumizi,wabunge wamesema sana lakini inaonekana hawasikilizwi.

Mkurugenzi Mussa Mbura hili mbona ni bomu kwako watu wanafanya kuibembeleza TAA kweli. Chukua hatua ulimalize hili uwanja huu ni aibu kwa hadhi ya jiji. Hivi karibuni ulikiri hadharani Rais kuidhisha na kuwaletea bn 30 kwa ajili ya mradi huu achilia mbali bn 4 mlizokabidhiwa na Mkoa sasa tatizo ni nini? Inakera sana.

Rejea kauli yako kwa Mkuu wa Mkoa ukiwa na NSSF hapo Mwanza na pia maagizo ya Waziri Kihenzile.Fanya kweli wacha siasa wewe ni mtendaji mnampa wakati mgumu Rais,msivizie mpaka kipindi cha uchaguzi.
 
Back
Top Bottom