Ibrah, ni kuwapa pole ndugu zetu wa Kigoma... Unajua quality ya life after mwekezaji inategemea pia huyo mwekezaji nyumbani anaishije!!?? Kumbuka kwenye picha za treni/garimoshi India jamaa wanasafiri wakiwa wamekaa mpaka juu ya garimoshi lenyewe, kufika wanafika lakini ni adha tu ndio kidogo inakuwa tatizo!!
Mwekezaji mpya TRL (ndio jina jipya hilo after TRC) ametoka India....... So, we are to learn travelling Indian Style
Personally sitegemei mabadiliko makubwa kwenye hilo shirika letu......
Ibrah ni kweli usafir wa treni una matatitizo makubwa na si kwa Kigoma tu bali kwa wale wote wanaoitegemea reli ya kati hasa kule kusikopitiwa na barabara kuu. Yule mwekezaji wa kihindi tusitegemee miujiza kwani hatuoni lolote la kuvutia kule ambako amekuwa akiendesha reli kwa muda mrefu.Hali ya usafiri wa Treni ambao ndiyo usafiri pekee wa uhakika kwenda mikoa mingine ni mbaya mno na inazidi kuwa mbaya siku hadi siku. Wasafiri wanasafiri bila taa kitu ambacho ni hatari kwa usalama na afya (maana kwenda haja usiku ni noma)
Kwa sasa usafiri wa Daraja la 3 ambao ndiyo unamudiwa na watu wengi ni adha tupu tiketi zinauzwa 8 tu na zimeisha! Ukibahatika kupata tiketi basi namba za siti zimegonganishwa kwa watu wengine wawili (na mtajuana wenyewe)na ni juu yenu kupangiana zamu ya kukaa! Ikiwa unataka kusafiri siku unayotaka inakupasa kulipa shilingi 45,000/- ili uweze pata tiketi ya kwenda Dar es Salaam nauli ambayo walipa wasafiri wa Kanda ya Ziwa kutoka Dar kupitia nchi jirani (Kenya na Uganda).
Ibrah unataka kunitoa machoni.
Pamoja na serikali kuwa wabaguzi wakubwa sana na kuutenga mkoa wa kigoma makusudi lakini kinachochangia matatizo hayo kikubwa ni ukosefu wa wabunge makini.
Kigoma haijapata kuwa na MBUNGE Makini anayewatetea hata siku moja. Hukumbuki miezi kama miwili iliyopita tu iliwalazimu FFU kuingia kuwatoa wasalifiri waliokuwa wamekaliana vichwani.
Kwa kifupi ule sio usafiri.
Harafu angali wabunge wa kigoma siku ile ya ZITO walivyoshambuliana bungeni. Selukamba&Msambya dhidi ya ZITO.
Utafikiri ndicho kilicjhowapeleka bungeni.
Ni aibu sana ndugu zanguni,
Naomba Jambo forum itusaidie kutuokoa watu wa KIGOMA twafa.
Ibrah unataka kunitoa machoni.
Pamoja na serikali kuwa wabaguzi wakubwa sana na kuutenga mkoa wa kigoma makusudi lakini kinachochangia matatizo hayo kikubwa ni ukosefu wa wabunge makini.
Kigoma haijapata kuwa na MBUNGE Makini anayewatetea hata siku moja. Hukumbuki miezi kama miwili iliyopita tu iliwalazimu FFU kuingia kuwatoa wasalifiri waliokuwa wamekaliana vichwani.
Kwa kifupi ule sio usafiri.
Harafu angali wabunge wa kigoma siku ile ya ZITO walivyoshambuliana bungeni. Selukamba&Msambya dhidi ya ZITO.
Utafikiri ndicho kilicjhowapeleka bungeni.
Ni aibu sana ndugu zanguni,
Naomba Jambo forum itusaidie kutuokoa watu wa KIGOMA twafa.
1. Viongozi toka Kigoma pia wamewaangusha wana Kigoma- kusema kweli sijawahi ona msukumo wa kweli toka kwa viongozi wanaotoka Kigoma! Angalia mfano wa 1.4 Bil toka kwa wana kagera!
2. Sasa utamlaumu nani??? wakti viongozi wamekimbia Kigoma na kujenga Mz na Dar?
3. Jawabu kudumu ni kujenga daraja Malagarasi- na barabara lami na kuwa na usafiri wa uhakika wa barabara- haya ndo mambo ya kutetea kwa nguvu na Wanakigoma kuondoa shilingi ktk budgeti! Ahadi tu za serikali kila siku over daraja na barabara- sasa 46 years! Hamna kitu!
Sasa kama Kigoma wanachagua wabunge wanaotetea mambo ya Kitaifa kama Bugwazi na Zitto kwa nini wanashindwa kutetea infrustructure ya Kigoma?
Pale Mwanza kuna jamaa zangu kibao toka Kigoma, mara nyingi wamekuwa wakilalamikia suala usafiri. Ni vema suala hili sasa likatupiwa japo jicho la huruma...
Mkuu,Asante sana Morani; hawa Wahindi wa TRL ndiyo wanaoendesha zile treni ambazo watu wanakaa hadi juu ya behewa. Duniani kote hakuna mahali penye usafiri duni wa Treni kama kule India.
Nakumbuka kuona picha ya namna hiyo kwenye magazeti yetu kama kuna mtu anazo atubandikie hapa.
Tanzania ina matatizo mengi, na karibia kila sehemu inamatatizo yake,kuna mikoa kama Rukwa ambao wako kimya.
Usafiri wa treni wa india huwezi kulinganisha na nchi zetu za kajambanani, india iko advanced katika usafiri wa terni, na wana grades za treni pia., na wananjia nyingi, siyo kama sisi, treni moja kwa wakati mmoja! Si sahihi kwa ulivyosema kuhusu India.
Wakati Rais anafunga miaka 2 ya utawala kuna mwandishi alimwuliza kuhusu usafiri wa Reli , TRL an uwekezaji Muungwana akadai kuwa wakati wa TRC treni ilichukua hadi siku 8 kwenda Kigoma! Nilimshangaaa, maana haijawahi kutokea katika TRC Wasafiri kukaa siku 5 njiani ati kwa kuwa mabehewa ya mizigo yametokea never, Rais aliwadanganya WaTz! !
Mimi natoka sehemu ambayo miaka nenda miaka rudi, TRC alikuwa partner wangu mkuu katika mambo ya usafiri, tangia enzi zile tunalala chini ya uvungu wa viti! Wakati ule watu walikuwa wanakaliana vichwani na miguuni, ilikuwa inajaza kama vile mabasi ya kwenda mwanza kupitia njia ya kati yanavyojaza! Na ilikuwa inawezekana kukaaa siku kadhaa porini, mvua ikinyesha 'godegode, kidete', treni ya mizigo ikianguka n.k taratibu TRC ikaongeza 'customer care' kwa kuwa inawaleta abiria wake kwa mabasi pindi hali inapokuwa tete.
TRL imeanza kazi, ni budi wadau tupige kelele pale ambako tunaona wanataka kuturudisha miaka ile tulivyokuwa tunasafiri kama mizigo! ni budi tupige kelele kuona haki za wasafir zinalindwa ikiwemo compensation pindi treni inapochelewa kufika kama ilivyokusudiwa!
Kitu ambacho TRC walikuwa wakifanya ni kubadilisha Wasafiri kuhamia treni nyingine (kubadlishana) na ilikuwa sahihi kabis. Sijui Muungwana alipandaga Treni ya TRC lini
Ilikuwa pia inategemea na chanzo cha tatizo! Kama kipindi cha masika, hali ya treni moja kukwama 'Morogoro', nyingine 'Godegode; na nyingine 'Dodoma', ilikuwa jambo la kawaida, hapo huwezi kubadilishana! ni lazima moja ya gode gode iondoke kwanza ifike morogoro, na ya morogoro ifike dodoma ndipo ya dodoma iondoke! piga mahesabu hapo ni siku ngapi njiani! na kufika mapema kwa treni iliyokwama godegode ni majaaliwa ya hali ya mvua ikoje, na ikilzamika kuondoka bila kuangalia miundombinu ikoje, ndio matatizo kama ile ajali ya KIDETE ilivyotokea.
Mikoa hii ( Tanga) inadharauliwa .