Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,730
- 530
Hali ya usafiri wa Treni ambao ndiyo usafiri pekee wa uhakika kwenda mikoa mingine ni mbaya mno na inazidi kuwa mbaya siku hadi siku. Wasafiri wanasafiri bila taa kitu ambacho ni hatari kwa usalama na afya (maana kwenda haja usiku ni noma)
Kwa sasa usafiri wa Daraja la 3 ambao ndiyo unamudiwa na watu wengi ni adha tupu tiketi zinauzwa 8 tu na zimeisha! Ukibahatika kupata tiketi basi namba za siti zimegonganishwa kwa watu wengine wawili (na mtajuana wenyewe)na ni juu yenu kupangiana zamu ya kukaa! Ikiwa unataka kusafiri siku unayotaka inakupasa kulipa shilingi 45,000/- ili uweze pata tiketi ya kwenda Dar es Salaam nauli ambayo walipa wasafiri wa Kanda ya Ziwa kutoka Dar kupitia nchi jirani (Kenya na Uganda).