Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 11,578
- 19,887
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Kigoma, imewaachia huru washtakiwa 11 waliokuwa wakikabiliwa na kosa la kuua kwa kukusudia askari wawili wa Jeshi la Polisi na kukata sehemu za siri za mmoja wa askari hao katika mapigano yaliyotokea wakati wa kuwaondoa wananchi waliovamia eneo la Hifadhi ya Ranchi za Taifa (NARCO), wilayani Uvinza.
Hukumu hiyo ilisomwa Ijumaa (Agosti 14), na kesi hiyo ilihusu tukio lililotokea Oktoba, mwaka 2018, wakati wananchi karibu 1,000 walipojiunga kupambana na askari wakiwa na silaha za jadi.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, Ilvi Mgeta, alisema sababu za kuwaachia huru ni ushahidi alioutoa daktari wa Kituo cha Afya cha Lugufu, aliye wahudumia baadhi ya washtakiwa na kueleza kuwa risasi walizopigwa zilipita juu ya ngozi wakati washtakiwa wana makovu makubwa yanayoonyesha risasi zilipita upande mmoja na kutokea mwingine tofauti na shahidi ulivyoeleza.
“Tunashindwa kuelewa kwa nini shahidi huyu alitoa ushahidi wenye nia ya kuidanganya mahakama wakati akiwa anajua ukweli ni ushahidi wa askari walioeleza kuwapo katika mapigano hayo.”
Ushahidi mwingine ulioelezwa kuwa dhaifu ni wa askari walioeleza kushiriki operesheni hiyo kuwa walipambana na wananchi hao uso kwa uso na kufanikiwa kuwapiga risasi wakati wa mapigano, wakati makovu ya risasi hizo kwa watu 10 kati ya 11 walioshtakiwa, yakionyesha kuwa walipigwa upande wa nyuma na kutokea mbele hivyo wapigaji wa risasi hizo hawakuweza kuwaona uso kwa uso washtakiwa.
Pia, Jaji alisema gwaride la utambuzi halikufuata misingi ya sheria kwa kuwa mmoja wa washtakiwa alieleza kuwekwa kwenye mstari akiwa peku na wengine wakiwa na nguo zilizo jaa damu kutokana na majeraha ya risasi, hivyo kurahisisha kutajwa kuwa walihusika na mauaji hayo.
Kadhalika, alisema ushahidi wa aliyeshuhudia gwaride la utambuzi kuiambia mahakama kuwa hakuwaona washtakiwa hao katika gwaride la utambuzi pamoja na maelezo ya onyo yaliyoelezwa kuandikwa na washtakiwa, ambayo wote waliyakana mahakamani kuwa sio yao pamoja na kukamatwa eneo tofauti na tukio lilipotokea katika maeneo tofauti.
Baada ya Jaji Mgeta kupitia uchambuzi wa hoja za pande zote mbili za upande wa Jamhuri uliowakilishwa na Happyness Mayunga, Shaban Masanja na Riziki Matitu na upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Sadick Aliki, Kagashe Rweyumamu na Eliuta Kiviylo, alisema kwa kuzingatia uhalisia wa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo kuonyesha kuwa na taarifa zinazopingana, ushahidi huo ni dhaifu na hauwezi kuwatia hatiani washtakiwa hao na mahakama hiyo imeamua kuwaachia huru washtakiwa wote 11.
Askari waliopoteza maisha kwenye tukio hilo ni Inspekta Ramadhani Mdimu na Koplo Mohamed Nzengohuku. Washtakiwa 11 waliochiwa huru ni Gelya Gisega, Jumanne Jackson, Nkono Mwandu, Shishi George, Masanja John, Hamis Masalu, Walwa Malongo, Makenzi Lukelesha, Masalu Inambali, Petro Bucheyeki na Charles Maduhu.
NIPASHE
------
Nimesoma taarifa za hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma iliyowaachia watuhumiwa wa mauaji ya askari wawili katika tukio lililotokea huko Kigoma Oktoba 2018.
Wakati Polisi walitoa ushahidi kwamba watuhimiwa walijeruhiwa wakiwa wanapambana na askari uso kwa uso, ushahidi kutokana na makovu ya majeraha ya risasi ya watuhumiwa 10 umeonesha kwamba walipigwa risasi nyuma, sio mbele, ikionyesha kwamba Polisi waliwapiga risasi watuhimiwa wakati wakikimbia kuondoka kwenye tukio (shot in the back). Kwa hiyo jambo jingine hapa ni kwamba tuna jeshi la Polisi lenye askari waongo, na ambao hawaoni aibu hata kusema uongo Mahakamani ili kukandamiza washitakiwa!
Baadhi tunakumbuka mauaji ya Sharpville Afrika Kusini yaliyofanywa na askari wa Makaburu kwa wanafunzi ambao walikuwa wakiwakimbia Polisi na kuuwawa au kujeruhiwa kwa kupigwa risasi za nyuma. Dunia nzima, pamojana Tanzania, ililaani kitendo hiki na kukiita ni cha uuaji, ukatili, kisichofuata haki za binadamu, kilichofanywa na polisi wahuni wenye kukosa mafunzo na waoga!
Leo hii kitendo hicho hicho kinafanywa na askari polisi wa Tanzania katika nchi ambayo ilikuwa mstari wa mbele kulaani kile kilichofanywa na askari wa Makaburu!
Ikumbukwe kwamba katika ugomvi kuvamiwa na majambazi ukampiga risasi aliyekuvamia na kumuua, huwezi kujitetea kwamba ilikuwa ni self defence kama ulimpiga huyo mtu risasi ya mgongoni!
Lakini Polisi wetu wanashambulia raia na kuwapiga risasi za migongoni na kujaribu kuidanganya Mahakama kwamba waliwajeruhi hao raia katika mapambano ya uso kwa uso!
Tunasikitika kwamba katika mgogoro huu huko Kigoma kuna Polisi wawili waliuwawa. Lakini hilo halihalalishi Polisi wetu kuanza kuwapiga raia wanaokimbia eneo la tukio risasi za migongoni.
Tungependa kuona serikali ikichukua hatua kali kwa askari wote waliohusika na tukio hili, na kuwawajibisha viongozi wote ambao kwa namna moja au nyingine wanawajibika na hili. Hatuwezi kuwa katika nchi huru ambayo Polisi inapiga raia wake risasi za migongoni na kuwaua au kuwajeruhi. Lazima tuonyenye kwamba nchi hii naendeshwa kwa sheria ambazo zinawahusu hasa askari wanaopewa silaha kwa lengo la kutunza usalama, sio kutumia silaha hizo kuua raia wanaokimbia tukio.
Tuelewe kwamba polisi waliwafyatulia risasi za nyuma kwa lengo la kuua raia wa Tanzania waliokuwa wanakimbia tukio, sio adui adui wa nchi ningine.
Source: Walioshtakiwa kuua askari waachiwa huru