Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,715
- 218,260
Akifundisha somo la Katiba Mpya kwenye jimbo la Buhigwe, ambalo Mbunge wake alikuwa Phillipo Mpango, kwenye Mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Umati wa Wananchi, Tundu Lissu amedai kwamba, mkoa huo ulitelekezwa kwa miaka mingi kwenye ujenzi wa barabara.
Hata hivyo mara baada ya Dr Mpango kuwa Makamu wa Rais barabara za Kigoma zinajengwa kwa kasi, akiendelea kusema Lissu amedai kwamba hana shida na wana Kigoma kujengewa barabara, maana ni haki yao kabisa, lakini ameshangazwa na ujenzi ambao umesubiri kwa miaka zaidi ya 50 ili Kigoma ipate kiongozi wa Juu ndio ijengewe barabara.
Lissu amesisitiza Umuhimu wa Katiba Mpya kwa vile haitasubiri mtu fulani awe kiongozi ili maendeleo yapelekwe kwao, kwamba Katiba Mpya itaweka haki kwa hata yale maeneo yasiyotoa viongozi ili yapate maendeleo.
Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app