Kigoma: Mahakama Kuu yatenda haki bila kuingiliwa na Serikali. Yamwachia huru Baba Levo, yasema kifungo alichoongezewa ni batili

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
754
3,097
Msanii wa Muziki na Diwani wa Mwanga Kaskazini, Clayton Chipando ‘Baba Levo’ ameachiwa huru leo baada ya kumaliza hukumu yake ya miezi mitano huku Mahakama ikijiridhisha kuwa kifungo alichoongezewa kilikuwa batili.

Baba levo alihukumiwa kwenda jela Miezi mitano Agosti 01, 2019 na Mahakama ya Mwanzo Mwandiga, Kigoma baada ya kupatikana na hatia ya kumshambulia Askari wa Usalama Barabarani, baadae alikata rufaa kupinga hukumu hiyo na akaongezewa tena miezi mingine.

Kupita mtandao wa Twitter, Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto ameandika

Nashukuru sana kuwa Diwani wetu @ACTwazalendo
amerudi uraiani. Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma imeona adhabu ya kuongeza kifungo mpaka mwaka na siku 2 haikuwa halali. Tutaendelea na hatua za kimahakama kufuta rekodi ya jinai ya Diwani wetu. @officialbabalev
karibu tuendelee na kazi

Pia soma


Baba+levo+pic.jpg
 
Hahahha eti haki bila kuingiliwa na serikali kisa mmeshinda. Ila mngeshindwa basi serikali ingekuwa imeingilia 🤣🤣
 
Niliskia kuwa ccm wanampango wa kumpa ubunge hivi kuna ukweli hapo?
 
Yaani haki ni kushinda kesi tu. Nyie watu sijui vichwa vyenu vina shida gani
Tatizo hamfuatilii mambo ya kimahakama vinginevyo mngesikia jinsi mahakimu na majaji wakilalamikia kupewa maelekezo ya kutoa hukumu na hili lilithibitishwa na Jaji Mkuu mstaafu alipolalamikia tabia hiyo.
 
Papaa Mobimba, Kufuta rekodi ya uhalifu? Mahakama kuu imesema kifungo alichoongezewa ni batili maana yake kifungo halisi cha miezi mitano ni halali
 
Mahakama inajitekenya na kucheka yenyewe

Inamna siku hizi mahakimu ni incompetent mpaka hukumu inakuwa batili
 
Back
Top Bottom