Kigoma: Daktari feki aliyetibu kwa muda wa miaka 10 akamatwa

Jeshi la polisi mkoa wa Kigoma limemkamata daktari feki toka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilaya ya Kasulu ambaye amekuwa akifanya kazi za utabibu kwa zaidi ya miaka kumi katika Hosiptali mbalimbali hapa nchini.

Chanzo: Azam Tv
Huyu sio feki tena wamtunukie tu vyeti vyake
 
Itategemea na kujifanya kwake kulikuwa kwa mazingira gani.
Impersonating.JPG
 
Yaan miaka yote hawakutambua? Waangalie historia yake wajue nini chimbuko lake, inakuwaje atibu miaka yote bila kushtukiwa?

Ina maana ana ufahamu wa maswala ya afya?

Hatari sana
Huyo atakuwa ni mtu aliyesomea udaktari hadi kozi za mwisho. Ila huenda hakufanya mtihani wa mwisho au alifeli mtihani.
Huwezi kufanya chochote kwa usahihi kwa muda mrefu katika fani ya udaktari bila kupitia mafunzo ya Udaktari.
Ukweli ndio huo.
 
Miaka 10 kashindwa mara mbili, sio mbaya wamuache tu aendelee na kazi

Mbona hata madaktari binngwa wanafanyia watu operesheni, na wanakufa?!

Miaka 10 bila kushtukiwa ina maana mfumo wetu mzima wa kusimamia hii fani ni mbovu sana.
 
Ten years kashindwa mara mbili, wakati kuna madaktari sio fake lakini ndani ya mwaka tu washafanya makosa karibu 10 mara wamesahau mikasi, mara wamechanganya wagonjwa....

Ushauri kama huyu jamaa kazi anafanya nzuri ni bora wamuweke chini ya uwangalizi tu kila anapofanya kazi.
 
Huyo atakuwa ni mtu aliyesomea udaktari hadi kozi za mwisho. Ila huenda hakufanya mtihani wa mwisho au alifeli mtihani.
Huwezi kufanya chochote kwa usahihi kwa muda mrefu katika fani ya udaktari bila kupitia mafunzo ya Udaktari.
Ukweli ndio huo.
Nakuunga mkono, mtu ambaye hajawahi kupitia mafunzo ya udaktari uambiwe mgonjwa huyu hapa mfanyie operation sijui utaanzia wapi. Maana hata wale manesi wanaokusogezea vifaa watashangaa unaanza na kifaa sicho na haiwezekani. Alimaliza mafunzo ila mtihani wa makaratasi akafeli mwaka wa mwisho huyo.
 
Sijajua hii wizara kuna shida gani maana kazi zao ni nyeti ila magumashi wanakamatwa kila siku. Hawana mfumo mzuri wa utambuzi na ajara??? mimi ninadhani hata hospitali binafsi ni lazima serikali ihusike asilimia 100 kuhakikisha kweli wanaofanya kazi huko kweli wamesoma . Hawa madaktari wasifikiri ni kusoma tuu lakini lazima wajikite na wajue uongozi sio mtu anakuja na kujitambulisha kuwa dactari wewe unampokea tuu. Wasije wakawa bise kama yule " LE PROFFESER WA ZE COMEDY"
 
Nakuunga mkono, mtu ambaye hajawahi kupitia mafunzo ya udaktari uambiwe mgonjwa huyu hapa mfanyie operation sijui utaanzia wapi. Maana hata wale manesi wanaokusogezea vifaa watashangaa unaanza na kifaa sicho na haiwezekani. Alimaliza mafunzo ila mtihani wa makaratasi akafeli mwaka wa mwisho huyo.
Ni kweli
Na huko ni mbali sana, kuna Lugha ya Daktari ambayo unapozungumza tu Manesi wanajua huyu ni Daktari, kabla hata hujaanza kuwatuma wakuletee zana za kazi.
Hayo majina ya zana za kazi yote ni ya kitaalamu, usiyesomea hiyo fani huwezi hata kuyataja kwa majina.
 
Jeshi la polisi mkoa wa Kigoma limemkamata daktari feki toka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilaya ya Kasulu ambaye amekuwa akifanya kazi za utabibu kwa zaidi ya miaka kumi katika Hosiptali mbalimbali hapa nchini.

Kuna watu wana vyeti feki lakini tumeona wanafanya kazi nzuri ya kuongoza mikoa. Kwa hiyo sio tatizo katika nchi hi kama alikuwa akisaidia watu. Pia tumekuwa na mawaziri wenye feki PhD na MBA na wamechapa kazi safi kabisa.
 
Ni uongo huo,,,, kivipi ni dactari feki wakati anatibu watu na wanapona,,, acheni kutafanya ss mambulula
 
Back
Top Bottom