Kigoma: Daktari feki aliyetibu kwa muda wa miaka 10 akamatwa

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,241
2,000
Jeshi la polisi mkoa wa Kigoma limemkamata daktari feki toka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilaya ya Kasulu ambaye amekuwa akifanya kazi za utabibu kwa zaidi ya miaka kumi katika Hosiptali mbalimbali hapa nchini.

Kamanda wa Polisi wa Kigoma Martin, amesema wamemkamata Daktari feki kutoka kambi ya Wakimbizi ya Nyalugusu Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma,ambaye anatuhumiwa kufanya kazi hiyo asio na taaluma nayo kwa muda wa mika kumi katika Hospital mbalimbali hapa nchini Tanzania.

Daktari huyo feki amekamatwa akiwa na cheti cha kugushi cha Udaktari, amekamatwa na cheti cha kugushi cha mazoezi ya vitendo (internship) vilevile amekamatwa na cheti cha kugushi cha Usajili wa baraza la Madiktari la Tanganyika.

Ameshawa kufanya kazi katika Hospital ya St. Mary's iliyopo Karagwe mkoani Kagera 2007 - 2008, Hospitali Ndanda mission, Hospitali ya Feza, Hospitali ya maria stoppers Mwenge Dar Es Salaam. Baade akaajiriwa na Shirika la Redcross kuanzia mwaka 2016 July hadi alipokamatwa Mwaka 2018.

Imefahamika alishawafanyia Upasuaji watu wawili mmoja ilikuwa Upasuaji wa kujifungua na mwingine Upasuaji wa bandama. Wote hao Walipoteza Maisha.


Chanzo: Azam Tv
 

hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
42,712
2,000
hahaaa sasa kama mtu alikuwa anafanya kazi yake vyema siwamuache tu ..mtu kesha Fanya kazi miaka yote hiyo ." nyinyi wenyew hamuoni aibu kutuhabarisha kuhusu hiyo habari. .yaani mtu kafnya kazi kwa muda wa miaka yote hiyo huku vyombo vyenu husika vya ukaguzi vikiwepo ...CCM bwana "" hahaaaa "hawajamaa wanacheza mnoo na maisha ya watanzania ..mmeshajua ni idadi ya watu wangapi waliowahi kupatwa na matatizo makubwa mpka kufikwa na umauti baada ya kutibiwa na huyo mtumishi wenu '"?
 

Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,275
2,000
Jeshi la polisi mkoa wa Kigoma limemkamata daktari feki toka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilaya ya Kasulu ambaye amekuwa akifanya kazi za utabibu kwa zaidi ya miaka kumi katika Hosiptali mbalimbali hapa nchini.


Chanzo: Azam Tv
Watanzania tunaamini katika makaratasi na si vitendo; hao waliowatibu kwa miaka 10 walipona au walifariki? Maana inaelekea tunaweza kumwona Dr Shika kuwa ni daktari mzuri kwa kuwa na vyeti vingi wakati hajawahi kuingia wodini.

Practice makes better
 

Sir_Mimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2013
6,917
2,000
Huyo siyo fake tena wamwajiri tu aendelee na kazi yake,miaka kumi afanye kazi kisha leo mje mseme ni fake?haingii akilini!
 

TsafuRD

JF-Expert Member
Sep 29, 2013
1,940
2,000
apelekwe Chuoni kufundishwa taratibu za kazi na haiba ya kazi yake kwa muda mfupi tu then aendelree na kazi kuziba pengo la uhaba wa madaktari. hamna sababu ya kumfunga maana ameshakuwa experienced Doctor.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
58,974
2,000
Jeshi la polisi mkoa wa Kigoma limemkamata daktari feki toka kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Wilaya ya Kasulu ambaye amekuwa akifanya kazi za utabibu kwa zaidi ya miaka kumi katika Hosiptali mbalimbali hapa nchini.


Chanzo: Azam Tv
Kwa muda wote huo ameshakuwa daktari Bingwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom