Kigoma: Askari Polisi wamepigwa mawe na Wananchi

Kulupango

JF-Expert Member
Mar 19, 2020
288
534
Polisi Mkoani Kigoma wamelazimika kutumia mabomu ya machozi pamoja na kupiga risasi hewani kutawanya Wananchi wenye hasira ambao wamevamia nyumba ya mkazi wa Mtaa wa Yusuph Kata ya Mwanga Kusini, Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuharibu milango na madirisha kwa kutumia mawe.

Katika vurugu hizo Wananchi wengine wamepora baadhi ya vitu ndani ya nyumba hiyo wakimhusisha mtu huyo na kupotea (kumteka) kijana aliyetajwa kwa jina la Philipo Hussein baada ya kutoonekana kwa siku saba na inadaiwa alimchukua kijana huyo akiwa na watu wawili akisema kuwa ni Polisi wanaenda kumhoji kijana huyo katika Kituo cha Polisi.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Kigoma amesema mtu huyo anaedaiwa kumteka Philipo ni mwandishi wa habari nao wao wanalichunguza tukio.

Millard Ayo

Embu onyesha picha askari wakipigwa mawe.
Maana heading na habari vimefarakana.
 
Polisi Mkoani Kigoma wamelazimika kutumia mabomu ya machozi pamoja na kupiga risasi hewani kutawanya Wananchi wenye hasira ambao wamevamia nyumba ya mkazi wa Mtaa wa Yusuph Kata ya Mwanga Kusini, Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuharibu milango na madirisha kwa kutumia mawe.

Katika vurugu hizo Wananchi wengine wamepora baadhi ya vitu ndani ya nyumba hiyo wakimhusisha mtu huyo na kupotea (kumteka) kijana aliyetajwa kwa jina la Philipo Hussein baada ya kutoonekana kwa siku saba na inadaiwa alimchukua kijana huyo akiwa na watu wawili akisema kuwa ni Polisi wanaenda kumhoji kijana huyo katika Kituo cha Polisi.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Kigoma amesema mtu huyo anaedaiwa kumteka Philipo ni mwandishi wa habari nao wao wanalichunguza tukio.

Millard Ayo

Labda tuanze kujiuliza kijana aliyetekwa Philipo Hussein alikuwa muumini wa chama gani na aliyemteka naye ni wa Chama gani
 
Labda tuanze kujiuliza kijana aliyetekwa Philipo Hussein alikuwa muumini wa chama gani na aliyemteka naye ni wa Chama gani
Vyama vinahusiana nini na utekaji? Philipo ni Kijana wa kawaida mstaarabu anayejituma na hana makuu, pia anajua kuendesha piki piki, Mtekaji anaitwa Masanja umri miaka 45, ni Msukuma, pia Mchungaji na Mwandishi wa Habari wa Kujitegemea Pia Ana Shutumiwa Kwa Ujambazi, Ana maisha mazuri Pesa anayo ya Wastan, Ana gari la kutembelea na Nyumba Nzuri ya wastan hiyo uliyoona Inavunjwa madirisha.. Ana majivuno na mbwembe kiasi..

kuna kipindi Aliwahi kumtuhumu Philipo kuwa Amemlawiti mtoto wake na kumfungulia mashitaka na hivyo Philipo kukamatwa Baada ya uchunguzi wa kipolice na madakatari Alibainika hana hatia na mtoto Hajalawitiwa hivyo Bifu lilikuwepo kati yao na kuahidi kumkomesha.

Ndipo week iyopita walipofika watu usiku kama saa 5_6 na kujitambulisha kuwa police na kumkamata Akiwepo pia Mchungaji Masanja yaani Hasimu wake Akiwa miongoni mwao.. kesho yake ndg zake wakaanza kufuatilia Police lakini wakawa wanapigwa dana dana tu..imechukua siku 8 toka Philipo atoweke lakini police wakawa wanajibu tu kuwa wanafuatilia na huku Mtuhumiwa yaani Mchungaji Masanja Yupo mtaani na Anaendelea na maisha ndipo ndg na Raia wa mtaa wa Yusufu na KWAMCHAGA Walipoamua kuchukua sheria mkononi, walitaka kumuua ndipo Akaokolewa na police.

JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom