Kigogo amegeuka chinjachinja kwa ukwimwi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigogo amegeuka chinjachinja kwa ukwimwi.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tabutupu, Dec 25, 2010.

 1. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,409
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  KIGOGO AMEGEUKA CHINJACHINJA KWA UKWIMWI.


  Waziri wa chi ofisi ya Rais, Hawa Ghasia amewatakahadharisha vijana wa kike wanao ajiriwa serikalini kuwa makini kutokana na kuwepo kwa kigogo anayewaambukiza ukimwi kwa makusudi.

  Waziri amesema, kila mtumishi mpya anyeajiriwa anamdaka na anajua kabisa ameathirika na anaamua kuwa chinjachinja.

  Amekuwa mtu wa kuwadaka wasichana wageni wanaoajiriwa,na kuwaambukiza ukimwi. Dada zetu Jihadharini na huyu chinjachinja, bado tunawahitaji.
  Source: Mwananchi 23th dece 2010 ,ukurasa wa 15.
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,118
  Trophy Points: 280
  Huyu naye ni mropokaji tu kama sophy, hivi akiulizwa athibitishe ataweza? na kwa nafasi yake kama waziri anaweza kweli kutamka upupu kama huu? inawezekana ni kweli wapo but i dont kama ni fair ku-declare publicly namna hio au na yeye alipitiwa na huyo kigogo? basi tutaoa waathirika tupu au kaona keki yake inanyemelewa na vibinti vichanga...sasa yeye ameshakua zilipendwa bana, mwanamm gani atatoka na mwamk kajitanda namna ile? mmmh
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Heeeey,MMU siku hizi ni sehemu ya udaku na picha za kijeshi?
  kweli pame vamiwa huku
   
 4. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  uhhh ...nilidhani ni my Kigogo ambaye mpaka saa hii bado yupo jela......sasa huyu waziri akishitakiwa kwa kunyanyapaa atamlaumu nani.....mbona anakuwa kama hajaenda skuli
   
 5. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,409
  Trophy Points: 280
  hawa ndoo viongozi wetu
   
 6. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  sasa kama anamjua,kwanini asimtaje?so it means naye anamkingia kifua?!ndivyo viongozi wetu wa kweli wanavyotujali???
   
 7. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,409
  Trophy Points: 280
  Wanaoleta udaku ndio wamevamia. hapa tunaongea mambo ya msingi yanayo jenga jamii katika usawa, haki, na maadili. Ukitaka udaku ipo sehemu yake.
   
 8. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #8
  Dec 25, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135


  .........hapo kwenye red mmmhhhhh!!!!!!!
   
 9. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #9
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hawa ndio wale mawaziri wanaoteuliwa kwashinikizo la mke wa mkulu na sio kwa uwezo. Kuwabebabeba huku ndio kunawafanya wawe wanalopoka hovyo mambo hata yasiyo na maana ili mradi nao waonekane wapo!! Kama anamjua huyu chinjachinja kwanini asimtaje ili hao wasichana anaotaka kuwalinda wamfahamu badala ya ya kumficha, hao walengwa watamjuaje?
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180


  Anajiumauma nini si amtaje watu tumjue? Au keshamchakachua na yeye ndiyo maana hataki kumsema?
  Hizo promotion wanaopewa wenyewe sijui kama walipona.
   
 11. Lisa Rina

  Lisa Rina JF-Expert Member

  #11
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 1,770
  Likes Received: 2,037
  Trophy Points: 280
  Crap!
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Dec 25, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kwani ile sheria ya makosa ya kuambukiza HIV kwa kusudi si ilishapitishwa? kwanini wasichukue hatua badala ya kuwa kama mamba asiye na meno?
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180

  Hawakuipitisha kwa sababu na wao ingewabana. Mwenye VVU lini kapitisha sheria inayomshtaki mwenyewe?
   
 14. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #14
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ina maana Mzee Mkapa alikuwa na nyumba ndogo huko Ntwala? Maana huyu uwaziri wake ulianzia enzi za Che Nkapa? Nkwele kamsili tu.
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ama kweli, kiswahili ni lugha yetu ya Taifa lakini wengi bado wanafikiri kwa lugha zao za kikabila au lugha "mama".

  Hawa Ghasia, hakumlenga mtu fulani. Hasha, ila kaongelea kinasaha na kuwa-asa kina dada wajichunge na "kigogo".

  Sidhani kama hilo lina mjadala.
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Sheria ilishapitishwa toka 2008 kinachosubiriwa ni Regulations za kuitekeleza hiyo sheria.Regulations hizo zinaandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wadau wengine... kama kuna mtu wa Wizara basi atoe updates wamefikia wapi.
   
 17. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,409
  Trophy Points: 280
  Kumbuka kuwa Hawa Ghasia ni kiongozi tena waziri. Hatuwezi kuwa na mawaziri wasio wawajibikaji namna hii.Hakuwa na sababu ya kusema kitu kama hicho bila kutoa suluhisho. Ama sivyo angemtaja ili watu wajue ni nani wamwepuke. Pili inawezekana si habari ya kweli alitaka tuu kupata credit eti ni mfatiliaji wa mambo yanayo wahusu wafanyakazi wa sirikali lakini kachemka kwa hiyo strategy.
   
 18. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  "Waziri wa chi ofisi ya Rais, Hawa Ghasia amewatakahadharisha vijana wa kike wanao ajiriwa serikalini kuwa makini kutokana na kuwepo kwa kigogo anayewaambukiza ukimwi kwa makusudi. Waziri amesema, kila mtumishi mpya anyeajiriwa anamdaka na anajua kabisa ameathirika na anaamua kuwa chinjachinja."

  Hapo ni nani hajui kiswahili, sisi, walioandika kiswahili, Hawa Ghasia au wewe?????
   
 19. Atoti

  Atoti Senior Member

  #19
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 118
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Siyo wote wanaoenda skuli wanaelimika..
   
 20. smati

  smati Senior Member

  #20
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sijawaelewa bado???
   
Loading...