Kigezo cha Umri kwenye mahusiano

Kigezo cha Umri kwenye mahusiano

Hakuna formula ya hili kwani unapoanza mahusiano umri huwa si kigezo muhimu na ukishajenga mahusiano yenyewe inakuwa si busara kuvunja mahusuano hayo kwa sababu ya tafauti ya umri.

nice age is just a symbol umekuwa but intellect,commitment ndo mpango
 
Mimi napenda wa kunizidi miaka 10 nina sababu zangu. Mwanaume angalau awe na 35 na kuendelea huko chini ya hapo kwangu ni janga.

so you are 25yrs mamyii?!" ............. am 35yrs naomba nikuoe.
 
ngoja waje waongee wengine,
ila mimi mume wangu ni mkubwa kwangu kwa miaka 9 na sasa tuna miaka
mitatu ya ndoa na tayari tuna watoto wawili wa kike(pacha) wana miezi
11, sijawahi kujuta na wala sijawa na wazo, jinsi anavyonilea nikifanya
kitu utasikia no honey wewe bado mtoto acha nitafanya mimi kiukweli ni
maelewano ya kwenda mbele, nilivyojifungua akaniambia miezi 9 uliyobeba
mimba imekutosha sasa ni zamu yake kuhudumia watoto, na akitoka ofisini
unaona masikio yamemsimama kama popo mgeni anawahi kufanya kazi
nyumbani. kiukweli umri ni jambo la muhimu. nadhani ningekuwa na waumri
wangu mambo yangekuwa mengine.

Hongera, natamani na mimi nipate mwanaume aliye nizidi umri sana.
 
hii ni bahati tuu, ila unachokiomba unakipata.
 
aisee, mbona kama nakuwa disappointed vile, girlfriend wangu ananizid miezi kadhaa na ndio wife to be...

usiogope mkuu..maelewano ndo muhimu kati yenu.upendo utawale.
 
Habarini

Natumai nyote mu wazima kabisa nami namshukuru Mungu nipo vyema!

Hebu tuligeukie suala hili la umri kwenye mahusiano yetu ya kimapenzi!
mimi sio mfanya utafiti ila naongea kwa ufahamu wangu tu

Utofauti wa umri je pia ni kigezo cha kujenga mahusiano bora? Namaanisha age difference maana nimekuwa nikiona vijana kwa vijana wanasumbuana mfano, kijana mwenye 25 akiwa na binti wa 22 yrs au juu yake kidogo kunakuwa na msuguano usioisha!

Au wao kwa wao kupishana ndani ya miaka mitano hadi saba hivi bado kunakuwa na fukuto lisiloisha la mara kwa mara!
lakini kwa watu waliopishana zaidi ya miaka kumi na kuendelea hali huwa shwari kidogo!

Je ni kweli kigezo cha Umri ni muhimu kwa wahusika kabla ya kuanza mahusiano? Epuka kejeli na matusi pia.......nawasilisha


Asanteni

age is just a number.!
 
Unebarikiwa kuliko wanawake wote. Mko wachache. Mama Furaha njoo ujiunge JF uungane na huyu binti kuwaambia umma kuwa wapo wanaume wanaojali. Nakumbuka enzi zetu mke wangu akijifunga ile miezi 3 ya uzazi nilikuwa nampikia kabla ya kwenda kazini. Na nikirudi usiku mtoto nilikuwa nabadilisha mimi nepi maana hatukuwa na dusposable na pia kama zingekuwepo kwa mshahara ule tusingeweza. Nimemzidi miaka 5. Cha msingi pendaneni na msiangalie pembeni wanasema nini. Mama alikuja kumtunza mama Furaha alipojifungua alichoshangaa ni kuamka asubuhi na kukuta nimeshachemsha supu!!! Tulijifunza kwa mume wake (baba) na alifurahi. Kitunze kidumu na kila siku kinakuwa kipya.
wewe ni mmoja kati ya wanaume wachache wanaojitambua big up!!@zogwale
 
Jamani mimi naona umri sio kigezo,wa kwangu mimi nimemzidi mwaka mzima lakini tunapendana sana, anajua nini ya thamani ya mwanamke na wala hatujafikisha miaka 30, hao waliozinidi umri waliishia kunisaliti tu.
hongera mama@halati88
 
Sijui kwa nini ila mi natamani mume wangu anizidi miaka ya kutosha hata kumi,inaongeza heshima,and atakuelekeza cha kufanya cos he is mature,..young boys hawa mhh sheeda,labda wakikua kama kakazao wataacha
Usemalo pia lina ukweli mama! badiebey
 
Last edited by a moderator:
Sijui kwa nini ila mi natamani mume wangu anizidi miaka ya kutosha hata kumi,inaongeza heshima,and atakuelekeza cha kufanya cos he is mature,..young boys hawa mhh sheeda,labda wakikua kama kakazao wataacha
Usemalo pia lina ukweli mama! badiebey
 
Last edited by a moderator:
ngoja waje waongee wengine, ila mimi mume wangu ni mkubwa kwangu kwa miaka 9 na sasa tuna miaka mitatu ya ndoa na tayari tuna watoto wawili wa kike(pacha) wana miezi 11, sijawahi kujuta na wala sijawa na wazo, jinsi anavyonilea nikifanya kitu utasikia no honey wewe bado mtoto acha nitafanya mimi kiukweli ni maelewano ya kwenda mbele, nilivyojifungua akaniambia miezi 9 uliyobeba mimba imekutosha sasa ni zamu yake kuhudumia watoto, na akitoka ofisini unaona masikio yamemsimama kama popo mgeni anawahi kufanya kazi nyumbani. kiukweli umri ni jambo la muhimu. nadhani ningekuwa na waumri wangu mambo yangekuwa mengine.

nimeipenda na nimetamani pia
 
ngoja waje waongee wengine, ila mimi mume wangu ni mkubwa kwangu kwa miaka 9 na sasa tuna miaka mitatu ya ndoa na tayari tuna watoto wawili wa kike(pacha) wana miezi 11, sijawahi kujuta na wala sijawa na wazo, jinsi anavyonilea nikifanya kitu utasikia no honey wewe bado mtoto acha nitafanya mimi kiukweli ni maelewano ya kwenda mbele, nilivyojifungua akaniambia miezi 9 uliyobeba mimba imekutosha sasa ni zamu yake kuhudumia watoto, na akitoka ofisini unaona masikio yamemsimama kama popo mgeni anawahi kufanya kazi nyumbani. kiukweli umri ni jambo la muhimu. nadhani ningekuwa na waumri wangu mambo yangekuwa mengine.
Hongera sana sana..nakupa hongera ww kwa sababu wewe unaonekana mtu wa ku-appriciate na ndo unafanya mshkaji akupeende na kukuthamini..wanawake wengi ambao akili haijatulia wakipendwa na kuthaminiwa kama wewe wanajisau na kuona jamaa ni bushoke...kusema kweli hata ss wengine tunaomba mungu tupate wanawake ambao ni mature na akili ya MAISHA inacharge sawa sawa
 
Wanawake wengi wanaopenda wanaume waliowazidi umri !

Mara nyingi huwa ni Tegemezi !

My personal views !
 
Back
Top Bottom