Kigezo cha Umri kwenye mahusiano

Kigezo cha Umri kwenye mahusiano

ngoja waje waongee wengine, ila mimi mume wangu ni mkubwa kwangu kwa miaka 9 na sasa tuna miaka mitatu ya ndoa na tayari tuna watoto wawili wa kike(pacha) wana miezi 11, sijawahi kujuta na wala sijawa na wazo, jinsi anavyonilea nikifanya kitu utasikia no honey wewe bado mtoto acha nitafanya mimi kiukweli ni maelewano ya kwenda mbele, nilivyojifungua akaniambia miezi 9 uliyobeba mimba imekutosha sasa ni zamu yake kuhudumia watoto, na akitoka ofisini unaona masikio yamemsimama kama popo mgeni anawahi kufanya kazi nyumbani. kiukweli umri ni jambo la muhimu. nadhani ningekuwa na waumri wangu mambo yangekuwa mengine.

wow Mungu ambariki mumeo na wewe pia,sijui na mi ntapataga jamani kama huyo
 
Jamani mimi naona umri sio kigezo,wa kwangu mimi nimemzidi mwaka mzima lakini tunapendana sana, anajua nini ya thamani ya mwanamke na wala hatujafikisha miaka 30, hao waliozinidi umri waliishia kunisaliti tu.
 
Sijui kwa nini ila mi natamani mume wangu anizidi miaka ya kutosha hata kumi,inaongeza heshima,and atakuelekeza cha kufanya cos he is mature,..young boys hawa mhh sheeda,labda wakikua kama kakazao wataacha
 
Habarini

Natumai nyote mu wazima kabisa nami namshukuru Mungu nipo vyema!

Hebu tuligeukie suala hili la umri kwenye mahusiano yetu ya kimapenzi!
mimi sio mfanya utafiti ila naongea kwa ufahamu wangu tu

Utofauti wa umri je pia ni kigezo cha kujenga mahusiano bora? Namaanisha age difference maana nimekuwa nikiona vijana kwa vijana wanasumbuana mfano, kijana mwenye 25 akiwa na binti wa 22 yrs au juu yake kidogo kunakuwa na msuguano usioisha!

Au wao kwa wao kupishana ndani ya miaka mitano hadi saba hivi bado kunakuwa na fukuto lisiloisha la mara kwa mara!
lakini kwa watu waliopishana zaidi ya miaka kumi na kuendelea hali huwa shwari kidogo!

Je ni kweli kigezo cha Umri ni muhimu kwa wahusika kabla ya kuanza mahusiano?? Epuka kejeli na matusi pia.......nawasilisha

Asanteni

Haya mambo hayana fomula mm na mke wangu tuna mahusiano ya miaka kumi na nne na yalianzia chuoni.miaka saba ya mahusiano bila ndoa then nikaoa 2009, tumepishana miezi mm nimezaliwa mwezi wa nne yeye mwezi wa kwanza lakini mwaka mmoja we quarrel lkn tunasonga mbele. kwahiyo yawezekana ikasumbua au inaweza isisumbue ni nyinyi wenyewe jinsi ya kuendesha mahusiano,hayo ndio mawazo yangu mzee
 
ngoja waje waongee wengine, ila mimi mume wangu ni mkubwa kwangu kwa miaka 9 na sasa tuna miaka mitatu ya ndoa na tayari tuna watoto wawili wa kike(pacha) wana miezi 11, sijawahi kujuta na wala sijawa na wazo, jinsi anavyonilea nikifanya kitu utasikia no honey wewe bado mtoto acha nitafanya mimi kiukweli ni maelewano ya kwenda mbele, nilivyojifungua akaniambia miezi 9 uliyobeba mimba imekutosha sasa ni zamu yake kuhudumia watoto, na akitoka ofisini unaona masikio yamemsimama kama popo mgeni anawahi kufanya kazi nyumbani. kiukweli umri ni jambo la muhimu. nadhani ningekuwa na waumri wangu mambo yangekuwa mengine.

Unebarikiwa kuliko wanawake wote. Mko wachache. Mama Furaha njoo ujiunge JF uungane na huyu binti kuwaambia umma kuwa wapo wanaume wanaojali. Nakumbuka enzi zetu mke wangu akijifunga ile miezi 3 ya uzazi nilikuwa nampikia kabla ya kwenda kazini. Na nikirudi usiku mtoto nilikuwa nabadilisha mimi nepi maana hatukuwa na dusposable na pia kama zingekuwepo kwa mshahara ule tusingeweza. Nimemzidi miaka 5. Cha msingi pendaneni na msiangalie pembeni wanasema nini. Mama alikuja kumtunza mama Furaha alipojifungua alichoshangaa ni kuamka asubuhi na kukuta nimeshachemsha supu!!! Tulijifunza kwa mume wake (baba) na alifurahi. Kitunze kidumu na kila siku kinakuwa kipya.
 
hongera jamani,vijana wa sikuhizi hata kupika uji wanajua kweli?
 
Nina 24 charminglady wangu ana 28, maisha yanaenda. Mwakani ndoa
 
Last edited by a moderator:
wapo wanaojua ila wanaona ni kwanini wafanye hivyo kwakuwa wewe umeolewa basi kila kitu ni chako.
 
kiukweli unakuwa unamuongezea miaka mke kwa furaha anayokuwa nayo.
 
umri ni muhim mume kuwa mkubwa kuliko mke walau kwa 5yrs more hii si kwa ajili ya kusumbuana ni kwamba mke huanza kupoteza mvuto ktk umri wa above 32 so kama uko na mtu mliye sawa likely atataman wanawake wengine!!! maana umri wa mvuto wa mwanamke ni hiyo 17 to 32
 
Mimi napenda wa kunizidi miaka 10 nina sababu zangu. Mwanaume angalau awe na 35 na kuendelea huko chini ya hapo kwangu ni janga.
 
kwa mtazamo wangu umri unachukuliwa kama kigezo kutokana na ...
1.mwanamke anawai kupevuka sana kiakili kuliko mwanaume.hivyo wapenzi wa umri sawa mf 24.mwanamke atakuwa na uwezo mkubwa wa kufikili kuliko mwanaume..hivyo inapendeza kama mwanaume akamzidi miaka kidoo mpenzi/mke wake ili uelewa wake ukue.
2.kimaumbile mwanaume anachelewa sana kuzeeka kuliko mwanamke.hasa baada ya kujifungua mwili wa mwanamke unachoka halaka..xo ili kuepusha utofauti wao ni vema mwanaume akamzidi kidogo mwanamke ili waweze kwenda sawa...
3.heshima..mwanamme akimzidi umri mwezake heshima inakuwepo kwani atakuwa na uelewa mkubwa sana wa jinsi ya kuiongoza familia yake.na mwanamke atamuheshimu..mtazamo tuuu..

Aisee, mbona kama nakuwa disappointed vile, Girlfriend wangu ananizid miezi kadhaa na ndio wife to be...
 
ila nimeona wengi wakuu mmeongelea kuhusu mwanamme kumzidi mwanamke..je mwanamke kukuzidi mwanaume nayo ni mbaya kama kakuzidi miaka kumi chukulia una 35 mwanamama ana 48 ina kaaje.napia katika kitabu changu tukufu....mtume muhamadi aliowa mwanamke mkubwa kwake ki umri sana.na hakuna katika kitabu cha dini walicho ongelea kwamba ni haramu kumuowa mtu alie kuzidi umri....kama ipo niambie.nimtazamo tu
 
umri ndo nini ?point kichwani una KNOWLEDGE bby sac
 
Last edited by a moderator:
Hakuna formula ya hili kwani unapoanza mahusiano umri huwa si kigezo muhimu na ukishajenga mahusiano yenyewe inakuwa si busara kuvunja mahusuano hayo kwa sababu ya tafauti ya umri.
 
Back
Top Bottom