Kigamboni vs Mkuranga, Wapi Panafaa Kununua Kiwanja Kwa Ajili ya Asset?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,064
49,749
Nimeangalia Matokeo ya sensa nimeona Licha ya Kigamboni kuwa Dar ila Ina watu Wachache na wengi pia hawahamii tofauti na Mkuranga..

Sasa sijajua shida ni ipi ila nataka kuuliza,ni wapi Kati ya Mkuranga na Kigamboni naweza nunua kiwanja/viwanja Kwa Ajili ya kutunza kama asset Ili nije niuze baada ya miaka 10 kutanilipa zaidi?

Na bei za viwanja Wilaya hizo ikoje?
Screenshot_20230420-193037.jpg
Screenshot_20230420-193111.jpg
 
Nimeangalia Matokeo ya sensa nimeona Licha ya Kigamboni kuwa Dar ila Ina watu Wachache na wengi pia hawahamii tofauti na Mkuranga..

Sasa sijajua shida ni ipi ila nataka kuuliza,ni wapi Kati ya Mkuranga na Kigamboni naweza nunua kiwanja/viwanja Kwa Ajili ya kutunza kama asset Ili nije niuze baada ya miaka 10 kutanilipa zaidi?

Na bei za viwanja Wilaya hizo ikoje? View attachment 2594302View attachment 2594303
Mkranga pata mashamba sio viwanja kigamboni is over rated na madalali wa viwanja.
 
Mkuranga sasa hivi ni mashamba tu, tafuta sehemu nzuri nunua hekari zako kadhaa.
Kigamboni kuzuri ila uwe na pesa, au lah utapata kigamboni ya huko mbali mbali huko kimbiji, puna,buyuni huko,pemba mnazi.
Huko mbali mbali Kwa miaka 10 ijayo let say 2032 hakutanilipa? Shida yangu nije niuze tuu
 
Watu hawana Mpango kabisa na Kisarawe 😁😁.

Ndio Wilaya pekee licha ya kuwa jirani na Dar ila watu wamekupotezea kabisaa.
 
Mpaka wa Dar na Pwani Kwa wilaya ya Kisarawe una hifadhi ya msitu wa Pugu,sehemu nyingine kunapakana na Kambi ya jeshi alafu kinafuatiwa na hifadhi ya msitu wa Kazimzumbwi hivyo kuwa na ugumu wa kuwa na makazi ya watu Kwa kuwa maeneo hayo yamekatazwa kujenga makazi ya watu. Lengine wenyeji wamekuwa wagumu kuuza.
 
Nimeangalia Matokeo ya sensa nimeona Licha ya Kigamboni kuwa Dar ila Ina watu Wachache na wengi pia hawahamii tofauti na Mkuranga..

Sasa sijajua shida ni ipi ila nataka kuuliza,ni wapi Kati ya Mkuranga na Kigamboni naweza nunua kiwanja/viwanja Kwa Ajili ya kutunza kama asset Ili nije niuze baada ya miaka 10 kutanilipa zaidi?

Na bei za viwanja Wilaya hizo ikoje? View attachment 2594302View attachment 2594303
Kigamboni Ardhi saizi ni Ghari sana, sijui budget yako ila naamini utapata eneo dogo compared na lenye thamani kubwa compared na Mkuranga

Mkuranga utapata eneo kubwa sana kwa hiyo hiyo budget ya Kigamboni maana bado kule Ardhi sio Ghari kama Kigamboni

Kwa mradi wa muda mfupi nunua Kigamboni na kwa mradi wa muda mrefu nunua Mkuranga
 
Back
Top Bottom