Kigamboni haijauzwa acheni uzushi-JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kigamboni haijauzwa acheni uzushi-JK

Discussion in 'Major Projects in Tanzania' started by MziziMkavu, Jun 6, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Mkuu wa nchi amekanusha vikali uvumi uliozagaa Bongo kwamba serikali yake imepiga bei kwa wamarekani eneo la Kigamboni.

  Mkuu huyo alikanusha hayo jana wakati akizindua kivuko kipya cha MV Magogoni na kusema madai hayo kuwa hayana kichwa wala miguu.

  "Kuna watu waongo wanasema kigambini imeuzwa kwa Wamarekani, uongo wao umeaminika zaidi,Huu ni uvumi na uongo wa mchana hauna kichwa wala miguu, Wamarekani waje hapa wanatafuta nini?”Aliuliza.

  Alisema anachofahamu yeye ni kwamba Jiji kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wanampango wa kuboresha mazingira ya Kigamboni.

  Alieleza kuwa kinachofanyika ni kwamba wataalamu wa upimaji wanapima na kupanga vizuri mji huo na kamwe wenyeji wa eneo hilo hawatahamishwa bali watapewa maeneo yaliyopimwa, yatakayobaki watagawiwa wengine.

  “Ikitokea watendaji wakakiuka ahadi ya kutoa kipaumbele kwa wakazi wa Kigamboni, nipewe taarifa na hapo ndipo malalamiko yaanzie na si vinginevyo,”aliahidi Rais Kikwete.
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  MKUU WA NCHI AMELONGA HOJA INAKOSA WASEMAJI.......! WANAIPITA KAMA HAWAIONI.....!
  Kelele zote zimeishia wapi.....?
  HUREEEEEEEE....KIGAMBONI HAIJAUZWAAAAAAA.........!
  HAYA LETENI UZUSHI MWINGINE.................!
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  watu waongo wanasema kigambini imeuzwa kwa Wamarekani, uongo wao umeaminika zaidi,Huu ni uvumi na uongo wa mchana hauna kichwa wala miguu, Wamarekani waje hapa wanatafuta nini?”Aliuliza.

  [/QUOTE]

  duh! nakumbuka nilipokuwa mdogo nilikatazwa na hata kupigwa nikisikika nikisema "mtu muongo" au "anasema uongo" ..............leo hii rais wa nchi mbele ya hadhara ya watu ( watu wazima kwa watoto) ana tamka maneno hayo ....kweli tabia zimebadilika
   
 4. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Watz kwenye uchaguzi wa ubunge huko Busanda wameshuhudia utovu mkubwa wa nidhamu kisiasa pengine toka tz ipate huru,na ufisadi huo wa kisiasa uliasisiwa na kuenziwa na mawaziri wake waandamizi wawili askari George Mkuchika na waziri kijana William Ngeleja.
  Akiwa kata ya Katondo,sehemu inayochukuliwa kama ndiyo ngome kuu ya wapinzani hasa Chadema,askari Mkuchika aliwaambia waandishi wa habari kuwa "hata kama mnaishabikia Chadema,lkn CCM itashinda hasa kwa kura za vijijini kwani huko wakazi hawasomi magazeti na wala hawaoni TV kwani hamna umeme",alisema haya huku waziri wa nishati na madini kijana Ngeleja akiwa amekwisha ingia kwenye jimbo hilo kuipigia kampeni CCM,na ndiyo maana kwenye makala hii nitamchambua zaidi kijana Ngeleja zaidi kuliko propagandalist askari Mkuchika.
  Willima Ngeleja,mbunge wa Sengerema hakuwepo kwenye baraza la kwanza la mawaziri ktk serikali ya kwanza ya mzee JK,Kuteuliwa kwake kuwa waziri kamili mara baada ya mabadiliko makubwa ya serikali ya TZ kufuatia kashfa ya Richmond kulinifurahisha sana mimi kwani nilidhani kwa ujana wake atakuwa na mawazo mapana zaidi ya kuwatumikiaa watz kinidhamu na kujituma;kumbe nilikuwa najidanganya !
  Yote madudu aliyoyafanya kwenye wizara yake kwa miaka si zaidi ya 2 toka awe waziri wa Nishati na madini yanafahamika,toka zile kashfa za kutaka kununua mitambo chakavu ya Richmond,songombingo la songas,baadhi ya wilaya kutokuwa na umeme hadi leo,umeme usio na uhakika kwa mikoa mingi ya tz na kikubwa zaidi kutofaidika kwa sisi watz na mali asili zetu zitokanazo na madini kutokana na mikataba ya "carl peters'iliyosainiwa na vigogo kutoka ktk wizara ya Ngeleja.Kwa ufupi kama kuna waziri anatakiwa asibanduke hata dakika moja kwenye ofisi yake makao makuu kwa sababu yupo nyuma sana kwenye kufanikisha malengo yake kwa watz ni waziri wa nishati na madini Ngeleja,kinyume chake anakwenda hadi Busanda tena kuongea "pumba"tupu kwa niaba ya wizara yake!
  Waziri Ngelaja akiwa anawakilisha wizara ya Nishati na madini,akawasili Busanda kumnadi mgombea wa CCM mama Lorensia Bukwimba kwa kuwambia wananchi hasa wachimbaji wadogowadogo kuwa"CCM ndiyo yenye nchi na kati yenu yeyote atakayebainika hajatupa kura yake tutaituma TRA kuja kuangalia rekodi yake ya ulipaji kodi".Kinachonishtua hapo,je kulipa kodi si ni haki ya kila mtz anayeingiza mapato ili kuinua uchumi wa nchi yake?kumbe ukiwa mwana CCM usipo lipakodi hufuatiliwi sana na vyombo husika?uwezo mdogo wa kijana Ngeleja kwenye uongozi ulianza kudhihirika hapo!
  Kijana Ngeleja hakuishia hapo,kwa kutumia wizara yake ya Nishati wafanyakazi wa Tanesco wakaanza kutandaza nguzo eti sasa baada ya miaka zaidi 40 ya kuwepo wilaya ya Geita duniani ndipo watapeleka umeme,huo ni utapeli mwingine mkubwa wa kisiasa ulioasisiwa na kuongozwa na kijana Ngeleja!
  Ngeleja kaenda Busanda kupiga kampeni za kashfa na vitisho,lkn hajawaambia hadi leo watz mustakabali wa nchi yao juu ya uwizi mkubwa wa maliasili yetu ya madini unaofanywa na wenzake hasa kama ujangili wa mgodi wetu wa kiwira ambapo kuna tuhuma za wazi bwana mkubwa Mkapa na mwenzake Yona walijipa kwa bei poa.Hapo najiuliza tena na tena na maswali,lipi lingekuwa jambo la kutusaidia sisi walalahoi kati ya kwenda kudanganya walalahoi Busanda au kutusaidia kuturudishia mgodi wetu wa kiwira mikononi mwetu?
  Ngelaja,dhambi uliyoichuma kule Busanda itakutafuna wewe milele!Geita ni wilaya tajiri sana iliyofunikwa na dhahabu lukuki,lkn ni wilaya masikini sana tz labda ikiizidi Bunda tu kwa utajiri.Tulitegemea waziri husika ungesimama na wana Busanda kuwaondolea kwenye lindo hili la umaskini hasa kwa kuatetea kuwa wafaidkie na dhahabu waliyonayo,kinyume chake wewe unazidi kuwaibia kisiasa!CCM ipo pale toka enzi za mbunge Donald Max lkn huduma muhimu za binadamu kama vile umeme,maji na shule hamna!leo hii unakuja Ngeleja kuwatapeli kwa kusimikia nguzo?
  Sio tu Busanda au Kyela au Hanang,matatizo ya huduma za jamii kwa watz ni yaleyale na wala CCM haipiganii kwa vyovyote kuyaondoa.Busanda hawana umeme,maji,shule,zahanati na tija kwa wafanyakazi hata wa serikali ipo chini sana;sawa tu na Biharamulo labda kama wamebahatika Biharamulo ni kupata umeme wa kubangaiza lkn kwa vyeyote vile huduma za maji,shule na huduma za kiusalama hawapo pazuri kama tu Busanda!
  Kwa mtaji huo basi,sisi tunamtegema tena Ngeleja aende Biharamulo kuokoa jahazi ili CCM ichaguliwe tena!lkn akumbuke pia Biharamulo sio Busanda na kule watu wanaangalia TV na kusoma magazeti kwa hiyo basi askari Mkuchika hawezi kwenda huko!
  Naam Ngelaja nenda tena kaambie wakazi kule kuwa umeme wao sasa utakuja kwa kutumia vinu vya nuklia na ikiwezekana nunua hata kinu kimoja cha mfano kawaonyeshe,na uchaguzi ukiisha ondoka zako,kama tu ambapo sasa hutaki hata kusikia habari za Busanda.
  Kwa vyovyote vile huenda CCM ikampeleka Biharamulo waziri mwingine kijana"Mkuu wa Vitambulisho"ambaye pia waziri kijana Lawrence Masha ambaye kuwa alikuwa kule Busanda eti kuangalia usalama wa raia.Hakika kweli serikali hii haijali,je waziri Masha na hali ya usalama kwa raia wa tz ilivyo hivi sasa mbapo albino wanakatwa mapanga,majambazi yanapora Dar hadi mchana,anastahili kuacha ofisi yake hata kwa dakika moja na kuja Busanda?kama Masha alikuwepo Busanda akiacha nchi kwenye usalama tete atashindwa vipi kujikongoja Biharamulo kuhaidi wakazi kule kama mkiichagua CCM mtaletewa kombania nzima ya polisi kila kijiji?hawa ndiyo mawazir wetu vijana!
  Imeniingia imani kwa Rais JK kuwa endapo atashinda 2010 ni bora awachague wazee akina Kingunge kuongoza wizara,ingawaje wamechoka lkn wanachagua la kusema!Ilikuwa kauli mbiu yetu zamani sisi vijana kuwa na sisi tupewa nafasi,lkn kumbe kama tukipewa nafasi tija ya kazi ndiyo hii kama ya akina Ngelaja ni heri mzee Malecela arudi wizarani!
  Liwalo na liwe,lzm tutashuhudia kauli zisizo za kistaarabu kutoka kwa wanasiasa wa tz kwenye uchaguzi wa Biharamulo hasa hawa vijana;nikisikia tena kauli kama hizo toka kwa vijana wetu akina Ngelaja sitashangaa kwani hamna mzee wa chama hata mmoja aliyewakemea,badala yake wazee akina Ndejembi wanawaita waandishi wa habari pale Maelezo kutuambia nahau zile zile za kila mwaka"ndani ya CCM hamna fisadi,na kama fisadi ni yeye sio chama" huwa nacheka sana nikisikia habari za akina Ndejembi,je kuna Chama bila watu?Na ndiyo kusema labda wazee hawa wamebariki yale waliyoyasema akina Ngeleja kule Busanda?mboina hawawakemei?
  lkn Ngelaja kumbuka kuwa Busanda sio Biharamulo na muulize kilichompata mbunge aliyeangushwa Anatory Chonya kwa mbunge aliyeshinda hayati Kabuye,nasisitiza tena Ngeleja usome alama za nyakati yasije yakakukuta kama ya Makamba Tarime
   
 5. k

  kela72 Senior Member

  #5
  Jun 6, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona ya nchi kuongozwa na Rostam hajibu??
   
 6. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2009
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  Du kibao kimeshageuka! Tuliambiwa wawekezaji ndo wanakuja leo imeshakuwa hivyo? Tumekwisha! Jiji na wizara ya ardhi, kichefuchefu kitupu. Nilitegemea milioni 200 kwenye kiploti changu.
   
Loading...