Kigaila: Mbowe amekula chakula ambacho hajui nani amekileta

"Ukitaka kujua nia ovu iliyopo, kwa mujibu wa sheria mtuhumiwa akikamatwa na Polisi akapelekwa kituo cha Polisi ana haki ya kutembelewa na ndugu zake, kupelekewa chakula na kutembelewa na Mawakili. Mwenyekiti akiwa Oysterbay Polisi walikataza kuonana na familia yake."

"Familia inapeleka chakula, Polisi wanapokea, familia haimwoni mwenyekiti. Polisi wanampelekea chakula mwenyekiti bila yeye kujua nani ameleta, maana yake usalama wa mwenyekiti wetu tutaudai mikononi mwa Jeshi la Polisi."

"Mwenyekiti amekula chakula ambacho hajui nani amekileta. Kwa mujibu wa sheria za Polisi na Magereza kama mtu ameletwa chakula lazima aliyeleta aonekane na aonje mbele ya Polisi na mbele ya mtu aliyeletewa, kuwa kipo salama. Wamezuia ndugu, anayeonja chakula ni nani?

"Watu waliokamatwa wapo Mburahati, Buguruni, Sarenda, Polisi Kati na maeneo mbalimbali wamekataza ndugu zao na mawakili wasiwaone na ndugu zao wakipeleka chakula wanapokea Polisi na kuwapa chakula, tunajuaje usalama wa chakula ambacho kinabaki mikononi mwa Polisi?"" - Benson Kigaila
Huyo ng'ombe wenu wa kulimia kaua wengi sana. Asiogope kufa.
 
Siwamuue tu nchi ipate maendeleo , maana nchi hii Mbowe ndio kaifikisha hapa hata tozo kaleta yeye gaidi yule , tangu uhuru anatusumbua tu aaaghhhhhh
 
Back
Top Bottom