Kifungo cha miaka 30 au Kudharirika..... USHAURI Tafadhari

Kifungo cha miaka 30 au Kudharirika..... USHAURI Tafadhari

Pilot_In_Command

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2013
Posts
2,507
Reaction score
3,459
Kama kawa... wakuu leo nimeona niseme tu..

Kuna vitoto vya kike.. na sometimes wakiume wanapenda sana kuja ninapoishi na wanaingia hadi Chumbani kwangu..

kwa kuwa mie sio Mkali,na wala sina roho mbaya sasa wamenizoea sana.. kiasi kwamba wakiamka tu asbuh wanakuja kugonga geti niwafungulie..

hali hiyo imechochewa na mie kuwapa Video games wacheze, kuwapa Pc waangalie katuni na kuwapikia misosi.. sasa wamenogewa sana hadi usiku wa saa nne wanatoroka makwao wanakuja kwangu.. Kuwafukuza siwezi..

HALI IMEKUWA MBAYA ZAIDI.

mama zao nao, wamefuata tabia za watoto wao... unakuta anakuja kumchukua mwanae badala amchukue aondoke nae.. na yeye anabaki hapo hapo.. kama ni chumbani basi na yeye anakaa kitandani.. wakati ni mke wa mtu.

hivyo hivyo hadi usiku .. wanakuja mama zao.. kuulizia kama watoto wao wamesahau viatu.. au masweta kwangu.. na jambo hilo linaleta sintofahamu kwa majirani wa kiume.. kwani wao huwa sina mazoea nao sana zaidi ya wake zao...

hata mtu huwezi kukaa faragha na mpenzi wako if akija.. huwez kuenjoy nae.. ni mwendo wa kengele tu kila saa... muda wote.. hodii.. hodii....

napata hasira mamaeeee... ipo siku naweza kusingiziwa nimebaka mtoto wa mtu.. nikafungwa bure.. maana siku hizi kusingiziwa nje nje

jana usiku..nimetoka zangu kupiga mazoezi.. nikaingia ndani.. kuoga.. ile natoka kuoga nashangaa mtu anagonga mlango.. nikaenda kufungua nikamkuta mdada.. ambaye ni jirani yangu kahamia mtaa huu hata wiki haijaisha.. anaanza kuniuliza maswali yasioeleweka.. na nilikuwa nimevaa kitaulo... nikamwambia ingia ndani.. akaingia.. nikampa kiti akakaa.. ile anataka kuongea na mimi nini shida yake.. mumewe akawa amerudi na kuanza kupiga honi katika nyumba yake.. huyu dada akili zake zikamtuma awahi kumfungulia mumewe ndipo alipokutana nae uso kwa uso akitokea katika mlango wangu... maana jamaa alishuka akafungue geti lake mwenyewe maana alikaa sana nje bila kufunguliwa geti..

nikasikia jamaa anamfokea yule dada huku majirani wengine wakitoka nje.. nikaona sio ustaarabu nikatoka na nje kwenda kuyamaliza... kumbe nilikuwa nimekosea... maana nilitoka na kitaulo.. jamaa akajenga picha tofauti.. na akahamia kunifokea mimi...

kwakuwa sipendi upuuzi.. niliingia ndani.. na kuyaacha yale mambo yaendelee bila ya mie kuyasikia...

sasa nimetafakari... nimeona.. hapa kuna mawili.. JELA AU GESTI...
 
Achana na wake za watu mkuu, mueleze ukweli jamaa kisha umuombe msamaha halafu toweka gheto kama mwezi ukirudi addiction yao ishaisha.
jamaa sijabahatika kuonana nae leo.. mke wake kasema jamaa amemuelewa so yameisha..

kuhusu kutoweka hapa .. mwezi wa 8 wote nilikuwa songea kikazi... nimerudi tar 10 mwez huu.. ndio kama nimechochea.. kila saa hodii tumekumithi.... mara oh.. zawadi.. wananiona kama BABU KRISMASS
 
jamaa sijabahatika kuonana nae leo.. mke wake kasema jamaa amemuelewa so yameisha..

kuhusu kutoweka hapa .. mwezi wa 8 wote nilikuwa songea kikazi... nimerudi tar 10 mwez huu.. ndio kama nimechochea.. kila saa hodii tumekumithi.... mara oh.. zawadi.. wananiona kama BABU KRISMASS
Kwani huwezi kuhama mkuu? unaweza kujitwalia matatizo makubwa sana chief
 
Back
Top Bottom