bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 1,113
- 2,718
Unazinduka katikati ya usiku wa manane.
Huwezi kusogeza kiungo hata kimoja. Kifua chako unahisi kizito sana, kama kuna kitu kikubwa kimekukaa. Unajaribu kupiga kelele lakini sauti haitoki. Unahisi uwepo wa kiumbe fulani chumbani kwako kitu ambacho hakipaswi kuwepo hapo.
Muda mfupi baadaye, hali hiyo inapita. Unakaa kitandani, uko peke yako, lakini mwili mzima unatetemeka kwa hofu.
Kwa karne nyingi, watu waliokumbana na hali hii walisema jambo moja: Shetani alimtembelea usiku.
Shetani wa kiume aliitwa Incubus, na wa kike aliitwa Succubus. Na historia yao ni ngeni na ya kutisha kuliko unavyofikiria.
wanatheolojia wa Kanisa walilichukulia jambo hili kwa uzito mkubwa.
Thomas Aquinas, mmoja wa wanafalsafa wakubwa wa Kanisa, aliandika kuhusu viumbe hawa. Nadharia yake ilikuwa ya ajabu: Alidai kuwa Incubus na Succubus ni shetani yule yule anayegeuza umbo. Kwanza humtokea mwanamume kama Succubus na kuchukua mbegu zake za uzazi, kisha hugeuka kuwa Incubus na kwenda kumpachika mimba mwanamke!
Stori za kale zinasema hata mchawi mashuhuri Merlin alizaliwa kwa njia hii akiwa mtoto wa Incubus na mwanamke wa kibinadamu.
Kitu cha kusisimua ni kwamba tukio hili halikutokea Ulaya pekee. Tamaduni mbalimbali duniani kote zilizungumzia tukio hili hili la kutisha lakini kwa majina tofauti:
Zanzibar / Afrika Mashariki: Aliitwa Popo Bawa kiumbe mwenye umbo la popo anayewashambulia watu usiku.
Canada Alijulikana kama "Old Hag" (Bibi Kizee).
St. Lucia: Aliitwa Kokma mizimu ya watoto waliokufa bila kubatizwa inayorukia kifuani na kukukaba.
Hungary: Aliitwa Lidérc shetani anayetokea kama moto unaoruka.
Amerika ya Kusini: Waliamini samaki aina ya Amazon river dolphin hugeuka kuwa mwanamume mtanashati usiku na kutongoza wanawake.
Tamaduni tofauti, majina tofauti, lakini uzoefu ule ule!
NB. Miaka ya nyuma Tanzania popobawa aliwahi kusumbua sana.