Maisha ni stage 5: (1) Roho (2)kisha baadae unakuja katika tumbo la mama (3)Halafu unakuja katika dunia) (4) halafu utakwenda kaburini (5) halafu utafufuliwa siku hiyo ya hukumu.Binadamu ameumbwa kwa ajili ya kuishi milele,lakini hizi habari za kuzaliwa,kufa, ni kuondoka katika hali na kwenda katika hali nyengine yaani tunahama kutola katika stage kwenda stage nyengine lakini matokeo yake yote utaona bado tunaishi tu,Hapa tulipo kifo haimaanishi ndiyo kwamba kwisha kila kitu, hapana yale ni maisha mengine yale. Mungu anasema"Tunakuumbeni kutokana na hiyo dunia, na hiyo hiyo dunia mutarudi ndani yake,na baadae tutakutoeni kwa ajili ya maisha ya baadae".Kwa hiyo utaona sisi tunatoka katika hatua kwenda katika hatua nyengine.Ndiyo maisha hayo na baada ya hapo tukifufuliwa ni peponi na wengine motoni,(mungu asitujaalie wa motoni tu) Bado tunaishi tu na kule peponi na motoni watu hawafi,karne baada ya karne zile stage watu washazipitia