mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 16,102
- 36,076
- Thread starter
- #61
Kwa hiyo kama ni muislam asiandikwe kwa mabaya yake acha fikra potofu,dini zimekuja tu na majahaziMkapa aliuza Nbc,TCC na TBL kwa bei ya kutupa huku mashirika hayo yakiwa yanatengeneza faida,ni yeye pia aliyeiingiza nchi katika mikataba mibovu ya uchimbaji wa madini,ni yeye pia ndiye aliyeleta kampuni kutoka Afrika Kusini(Net Group Solutions) kuja kuendesha shirika la umeme ambapo matatizo ya shirika la umeme tuliyonayo hivi sasa yalichangiwa pia na uamuzi huo maana jamaa wakati wakisimamia menejimenti ya shirika hawakuwahi kufanya uwekezaji wowote wa kuimarisha miundombinu ya uzalishaji umeme.
Lakini pia wakati wa mkapa ndiyo ililetwa kampuni ya wahindi kuja kusimamia menejimenti ya shirika la reli ambapo katika jitihada za kulinusuru shirika ilibidi itumike gharama kubwa ili kuvunja nao mkataba.
Je tuseme naye alikuwa Mzanzibari? Hata hivyo lengo lako kubwa lilikuwa ni Uislamu ila hiyo Wazanzibar umelitumia kama geresha tu.