Kifo cha Sheikh Yahya: Gwajima ameshinda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo cha Sheikh Yahya: Gwajima ameshinda?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Kaitaba, May 20, 2011.

 1. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Shekh yahya na Gwajima nani zaidi

  MCHUNGAJI AMPA MASHARTI SHEH YAHAYA-JANUARY 4 ,2010

  Siku chache baada ya mtabiri mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahaya Hussein wa Dar es Salaam kutangaza katika vyombo vya habari kuwa mwana CCM atakayejitokeza kuchuana na Rais Jakaya Kikwete katika kinyang'anyiro cha kugombea urais mwaka huu, atakufa ghafla, Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Glory of Christ Ubungo ametoa masharti matatu kwa mtabiri huyo vinginevyo naye atakufa ghafla.

  Katika mahubiri kanisani hapo jana, Mchungaji Kiongozi, Gwajima alisema demokrasia ya Tanzania imo hatarini endapo mtu mmoja ataachiwa kuamua hatma ya taifa kinyume na mapenzi ya Mungu asiyekuwa na upendeleo kwa mtu yeyote.

  "Baada ya kuendelea kutenda kazi zake zikiwa ni chukizo machoni mwa Mungu, leo ninatoa hukumu kutoka kwa Bwana, nanyi nyote mtachuja kuwa ni upi utabiri wa kweli kati ya Sheikh Yahaya na Mungu. Ninamwagiza Sheikh Yahaya afanye mambo matatu la sivyo naye atakufa ghafla kama alivyowatishia Watanzania wenzake," alisema.

  Sharti la kwanza alisema ni Sheikh Yahaya kwenda katika kanisa hilo la Glory of Christ na kuonana na mchungaji Gwajima yeye mwenyewe ili amwongoze kwa sala ya toba, kisha ampokee Yesu katika maisha yake.

  Sharti la pili, Sheikh Yahaya ameamriwa kuanzia sasa aachane na utabiri wake ambao kwa miaka mingi alisema umewaumiza watu wengine wasiokuwa na hatia na kuwafaidisha wengine wachache kwa njia za giza.

  Na sharti la tatu, Sheikh Yahaya ametakiwa, baada ya kuokoka, arudi katika vyombo vya habari kwa nguvu ileile aliyoitumia kutangaza utabiri wake wa mtu kufa ghafla na sasa awatangazie Watanzania mabaya yake yote aliyokwishayafanya kwa watu wa taifa hili hadi siku ya mwisho alipolazimika kuokoka.

  Akifafanua juu ya masharti hayo, Mchungaji Gwajima alisema kimsingi yeye anamkubali Rais Jakaya Kikwete kuwa kiongozi wa taifa hili ila kinachomkera ni Sheikh Yahaya kuwatisha watu wengine wasitumie haki yao ya msingi katika kuikuza demokrasia hapa nchini.

  Alipohojiwa kwa njia ya simu, Sheikh Yahaya ambaye alisema yuko nje ya jiji la Dar es Salaam kwa siku ya jana, alisema katika kipindi cha miaka 40 ya utabiri wake umekuwa sahihi siku zote na umaarufu wake ni wa kimataifa.

  "Kamwe sitakwenda katika kanisa hilo, pia siko tayari kufuata sharti hata moja kutoka kwa mchungaji huyo.

  Nimeanza utabiri kabla ya yeye kuwa shemasi wa kanisa hivyo endapo nitakufa najua ni siku zangu zimefikia mwisho wala si vinginevyo," Sheikh Yahaya alisema.

  Akitoa mifano ya utabiri wake ambao aliosisitiza kuwa sahihi mara zote, alitabiri msiba wa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa kwa maelezo kwamba taifa litapata msiba mkubwa. Pia alisema aliwahi kutabiri kifo cha kiongozi mashuhuri ambaye kifo chake kingewakutanisha watu wa mataifa mbalimbali, dini, rangi na vyama mbalimbali vya siasa na kwamba kiongozi huyo alikuwa hayati Mwalimu Nyerere.

  "Je, sikutabiri kuwa ndani ya CCM utazuka mtafaruku na kusababisha ufa ndani ya chama hicho kitu ambacho ninyi waandishi mmekishuhudia hivi karibuni?

  Mimi siwezi kuongea kashfa yoyote dhidi ya mchungaji huyo bali ninachosema akipenda apeleke malalamiko yake Ikulu, kwani nako huko wapo watu wa kumjibu waliozishuhudia kazi zangu kwa miaka yote," alitamba Sheikh Yahaya.

  Alisema alitarajia kiongozi huyo wa kanisa aempe mwaliko rasmi waonane mahali popote siyo hapo kanisani ili waelezane masula ya nyota kwa undani badala ya ‘kumtisha'.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 524
  Trophy Points: 280
  Neno la Mungu litasimama milele yote.
  Tawala za majini, mapepo na mashetani lazima zianguke, kusambaratika na kupotea kabisa
   
 3. Wisdom

  Wisdom JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 473
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunasikitika kusikia kifo cha mnajimu maarufu wa Afrika Mashariki, Sheikh Yahya Hussein kilichotokea leo asubuhi, kabla ya kifo chake makundi mbalimbali ya Kikristo tuliomba na kukemea nguvu za giza zilizokua zinatumika na sheikh Yahya Hussein! na moja wa watumishi wa Mungu waliosema wazi kwamba aachane na nguvu hizo ni Mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la Glory of Christ hapa ni nukuu ya baadhi ya masharti aliyompa marehemu kabla ya uhai wake!

  “Baada ya kuendelea kutenda kazi zake zikiwa ni chukizo machoni mwa Mungu, leo ninatoa hukumu kutoka kwa Bwana, nanyi nyote mtachuja kuwa ni upi utabiri wa kweli kati ya Sheikh Yahaya na Mungu. Ninamwagiza Sheikh Yahaya afanye mambo matatu la sivyo naye atakufa ghafla kama alivyowatishia Watanzania wenzake,” alisema.

  Sharti la kwanza alisema ni Sheikh Yahaya kwenda katika kanisa hilo la Glory of Christ na kuonana na mchungaji Gwajima yeye mwenyewe ili amwongoze kwa sala ya toba, kisha ampokee Yesu katika maisha yake.

  Sharti la pili, Sheikh Yahaya ameamriwa kuanzia sasa aachane na utabiri wake ambao kwa miaka mingi alisema umewaumiza watu wengine wasiokuwa na hatia na kuwafaidisha wengine wachache kwa njia za giza.

  Na sharti la tatu, Sheikh Yahaya ametakiwa, baada ya kuokoka, arudi katika vyombo vya habari kwa nguvu ileile aliyoitumia kutangaza utabiri wake wa mtu kufa ghafla na sasa awatangazie Watanzania mabaya yake yote aliyokwishayafanya kwa watu wa taifa hili hadi siku ya mwisho alipolazimika kuokoka“

  Je, unabii huu umetimia? ama kifo kimesababishwa na matatizo ya kiafya aliyokua nayo muda mrefu?
   
 4. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2011
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,984
  Likes Received: 1,554
  Trophy Points: 280

  watu waliozoea kutapeliwa ndio hukubali haya maneno . Huyu yahaya hussein hana utabiri ila ALIKUWA ni shushushu mkubwa .
  Wajinga ndio waliwao
   
 5. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Haki yako lazima nikupe gavana!
  nasema THANKS, Thanks!
  Kumbe kuna wakati unapembua vyema gavana!
  Nilikwambia wee ni ticha mzuri tatizo ni ibilisi kakufunga ameona akikuachia huru nondo atakazo pata ni za kiukweli kiukweli!
   
 6. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  naweza sema ni utabiri umetimia-alikuwa mzee mshirikina-naamini ni pigo kwa washirikina wengi
   
 7. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Shehe kesha tangulia kwa Sheik Osama. Hivi alishindwa kujinajimu?
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,407
  Trophy Points: 280
  wadau hii imekaaje? i guess haina anya relation na kifo cha Sheikh Yahaya
   
 9. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #9
  May 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kweli kazi ipo....
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  at 81 years old

  na kuugua na kufanyiwa operesheni india...

  kuja kufa ndo gwajima ale ujiko sio?????????
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  kama alivyotabiri ( Mchungaji Gwajima ) Kuhusu kifo cha Sheikh Yahaya kifo cha Gafla na yeye huyo (
  Mchungaji Gwajima) atakufa kifo cha Gafla.
   
 12. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,610
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nawasikiliza tu.
   
 13. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,610
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  sijui na majini yake yamekufa ooh maskini.
   
 14. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,610
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndoa ndoano, bado umeninunia kwani.
   
 15. myao wa tunduru

  myao wa tunduru JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2011
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 613
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  sawa na kuusifu utabiri wa abunuwasi katika hekaya zake!
   
 16. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ushindwe kwa jina la Yesu!!!
   
 17. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tena sio kazi ndogo, maana mengi yatasemwa
   
 18. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Labda kuna waliokuwa wanafikiria ataishi milele
   
 19. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 512
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Hapo kwenye red.
  Kumbe Mzee huyu aliweka imani yake kwa wale watakao shuhudia kazi zake. Hakujua malalamiko yanatakiwa yaelekezwe sehenu gani. Lakini ni dhahili utabiri wake kwa wale aliosema wafuatwe ikulu kuulizwa ulianza muda mrefu kama alivyonukuliwa.
   
 20. STREET SMART

  STREET SMART JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2011
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 666
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  Gwajima huyu si ndo yule mchungaji mwenye skendo ya misukule feki...
   
Loading...