Natanguliza pole zangu za dhati kwa familia, ndugu, jamaa na CHADEMA kwa kifo cha Mwanasiasa mkongwe hapa nchini Hayti Richard Tambwe Hizza. Hayati Tambwe alivutia kwa umahiri wake katika matumizi ya lugha ya ksiasa, uharaka wake wa kufikiri na kujibu na vionjo vyake vya kusema kisiasa hasa anapokuwa jukwaa la kisiasa. Richard Tambwe Hizza alikuwa tajiri wa maneno ya kisiasa. Alikuwa mahiri alipokuwa CUF, CCM na hata CHADEMA.
Siasa za Hayati Tambwe Hizza hazitofautiani hasa na za kada wa CCM Ndugu Livingstone Lusinde aka Kibajaji. Uzungumzaji wao wa kiutani na 'madongo' huku wakijibu au kumimina 'data' za kisiasa unawafananisha. Kama alivyo Lusinde, Tambwe Hizza hakuwahi kukosa jibu kwa swali lolote la kisiasa. Ingawa majibu au maelezo yake mengi yalionekana kuchekesha, majibu na maelezo hayo yalijaa 'data' za kuacha midomo wazi wasikilizaji wake.
Hadi kukutwa na umauti wake, Tambwe Hizza alikuwa mwanachama wa CHADEMA na alikuwa miongoni mwa wapiga kampeni wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Kinondoni. Hadi jana alishiriki katika kampeni na vikao vya CHADEMA vya kimkakati. Alikuwa akijibu na kuelezea kwa 'data' yale yanayomhusu mgombea wa CHADEMA Salum Mwalimu kuhusu 'Uzanzibari' wake. Alimtaja hata Dr. Hussein Mwinyi aliyewahi kuwa Mbunge wa Mkuranga na sasa Mbunge huko Zanzibar.
Katika ufanano wao, Mkuu
GENTAMYCINE, mmoja wa wanachama nguli wa JF, 'aliwafananisha' Tambwe Hizza na Livingstone:
Kati ya Livingstone Lusinde wa CCM na Tambwe Hiza wa CHADEMA nani anaongoza kwa madongo? Aliwapambanisha katika muktadha wa ufanano wao katika kufanya siasa zao na hata kuendana na vyama vyao vipya wanavyohamia. Tambwe alihama CUF na CCM. Lusinde alihama CCM na CHADEMA. Jana, ilikuwa kilele cha mpambano wao.
Katika kampeni za Ubunge Kinondoni hiyo jana, Tambwe Hizza alikuwa na CHADEMA. Ndugu Livingstone Lusinde alikuwa 'Mgeni Rasmi' kwenye kampeni za CCM katika Kata ya MAKUMBUSHO. Kila mmoja alikuwa akimnadi mgimbea wake. Tambwe alikuwa na Salum Mwalimu wa CHADEMA; Livingstone Lusinde alikuwa na Maulid Mtulia wa CCM. Na ni jana hiyo hiyo, Richard Hizza Tambwe alimaliza safari yake ya kimaisha hapa duniani. Was it a coincidence?
RIP Kamaradi Richard Hizza Tambwe!