Kifo cha Richard Tambwe Hizza: Was it a coincidence?

Kifo cha Richard Tambwe Hizza: Was it a coincidence?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,347
Reaction score
26,153
Natanguliza pole zangu za dhati kwa familia, ndugu, jamaa na CHADEMA kwa kifo cha Mwanasiasa mkongwe hapa nchini Hayti Richard Tambwe Hizza. Hayati Tambwe alivutia kwa umahiri wake katika matumizi ya lugha ya ksiasa, uharaka wake wa kufikiri na kujibu na vionjo vyake vya kusema kisiasa hasa anapokuwa jukwaa la kisiasa. Richard Tambwe Hizza alikuwa tajiri wa maneno ya kisiasa. Alikuwa mahiri alipokuwa CUF, CCM na hata CHADEMA.

Siasa za Hayati Tambwe Hizza hazitofautiani hasa na za kada wa CCM Ndugu Livingstone Lusinde aka Kibajaji. Uzungumzaji wao wa kiutani na 'madongo' huku wakijibu au kumimina 'data' za kisiasa unawafananisha. Kama alivyo Lusinde, Tambwe Hizza hakuwahi kukosa jibu kwa swali lolote la kisiasa. Ingawa majibu au maelezo yake mengi yalionekana kuchekesha, majibu na maelezo hayo yalijaa 'data' za kuacha midomo wazi wasikilizaji wake.

Hadi kukutwa na umauti wake, Tambwe Hizza alikuwa mwanachama wa CHADEMA na alikuwa miongoni mwa wapiga kampeni wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Kinondoni. Hadi jana alishiriki katika kampeni na vikao vya CHADEMA vya kimkakati. Alikuwa akijibu na kuelezea kwa 'data' yale yanayomhusu mgombea wa CHADEMA Salum Mwalimu kuhusu 'Uzanzibari' wake. Alimtaja hata Dr. Hussein Mwinyi aliyewahi kuwa Mbunge wa Mkuranga na sasa Mbunge huko Zanzibar.

Katika ufanano wao, Mkuu GENTAMYCINE, mmoja wa wanachama nguli wa JF, 'aliwafananisha' Tambwe Hizza na Livingstone:Kati ya Livingstone Lusinde wa CCM na Tambwe Hiza wa CHADEMA nani anaongoza kwa madongo? Aliwapambanisha katika muktadha wa ufanano wao katika kufanya siasa zao na hata kuendana na vyama vyao vipya wanavyohamia. Tambwe alihama CUF na CCM. Lusinde alihama CCM na CHADEMA. Jana, ilikuwa kilele cha mpambano wao.

Katika kampeni za Ubunge Kinondoni hiyo jana, Tambwe Hizza alikuwa na CHADEMA. Ndugu Livingstone Lusinde alikuwa 'Mgeni Rasmi' kwenye kampeni za CCM katika Kata ya MAKUMBUSHO. Kila mmoja alikuwa akimnadi mgimbea wake. Tambwe alikuwa na Salum Mwalimu wa CHADEMA; Livingstone Lusinde alikuwa na Maulid Mtulia wa CCM. Na ni jana hiyo hiyo, Richard Hizza Tambwe alimaliza safari yake ya kimaisha hapa duniani. Was it a coincidence?

RIP Kamaradi Richard Hizza Tambwe!
 
Mambo ya vifo hayajadiliki kirahisi mkuu, Kila mtu ataondoka kwa style yake, Anza kuandika wosia mkuu kuhusu mali zako hata kama huna mali andikwa uzikwe kwa staili gani mkuu.

Hujui saa wala muda utakapochukuliwa, Yeye kachukuliwa akiwa kwenye siasa, Wengine huchukuliwa wakiwa na michepuko.
 
Coincidence gani sasa kwamfano.kwamba kuhutubia jana na kufariki usiku?....Wakatimwingine usikubali kushikiwa akili.
 
Nadhani natakiwa kutafuta mwalimu wa kunielewesha ni kwa namna gani hapo limeingia suala la coincidence manake pamoja na maelezo marefu; naona hiyo possible coincidence umeihusisha na Kibajaji pia kuwepo kwenye kampeni!

It doesn't add up though nakubali hilo neno nalo ni tamu sana sio tu kuliandika bali hata kulitamka!
 
Coincidence gani? Livingston Lusinde kuwa na Maulid Mtulia vs kidogo chake?

What do you exactly mean by coincidence?
.
Da! nilidhani niko peke yangu tu ambae sijaelewa. Nimerudia kusoma mada lakini sijaona coincidence
 
Nadhani natakiwa kutafuta mwalimu wa kunielewesha ni kwa namna gani hapo limeingia suala la coincidence manake pamoja na maelezo marefu; naona hiyo possible coincidence umeihusisha na Kibajaji pia kuwepo kwenye kampeni!

It doesn't add up though nakubali hilo neno nalo ni tamu sana sio tu kuliandika bali hata kulitamka!
Ni hiyo ya wafananao hao kukutana kwenye kampeni siku moja kabla ya kifo cha mmoja wao
 
Back
Top Bottom