Kifo cha retired major generali James Luhanga

Mwenyezi Mungu amurehemu.
Hapo nilipo nukuu panatia shaka labda kama una maanisha alikuwa anapenda kazi yake. Mpenda vita n kama Rumsfeld au Bush au Osama

Luhanga alikuwa msomi bora wa kivita aliyependa vita kulipo pesa au mshahara au marupurupu.
Hivi Kamanda Kikwete jina lake lingine alilopewa kutokana na uhodari wake kikazi ni kamanda nani vile? Silikumbuki anayelikumbuka humu jamii forum anitajie nakumbuka la LUHANGA NA NYERERE naomba msaada mnitajie la Kikwete.
Anaitwa "The smiling Commander"
 
..Rest in Peace Major General James Luhanga.

..mwisho senior commanders wote wa vita ile watakwisha.

..Brig.Hemedi Kitete, Brig.Yussuf Himidi, Maj.Gen.Muhidin Kimario, Maj.General John Walden, Lt.Gen.Imran Kombe,Gen.Abdalah Twalipo, wote wamefariki.

..inasikitisha kwasababu sidhani kama makamanda wetu wametafutwa ili kuweza kupata mawazo na mitizamo yao kuhusu historia ya vita vya Kagera,Msumbiji, pamoja na jeshi letu kwa ujumla.

R.I.P Major General Luhanga.

General Kimario amefariki lini?
 
Last edited:
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Tunasuburi wote wamalizike ndio tuandike walikuwa kina nani? Ilivyo sasa, mashujaa wa kweli wa nchi hii kama hawa wamewekwa pembeni. Wadandiaji, wanaojiita wafanya biashara wakubwa ndio wameshika usukani. Meli yetu itaelea mpaka mwisho kweli?
 
R.I.P. Gen.Luhanga
...pamoja na taaluma nyingine za kijeshi,alikuwa rubani safi sana....huenda mwanae akafuata nyayo zake.
 
Huyu jamaa jeshi lilikuwa damuni sana utafikiri alikuwa mkurya, kumbe wapi ni mnyalukolo. R.I.P General luhanga!
 
na sasa hivi pale Lugalo hapitiki ma Generals wa kila namna wa[o kuuaga mwili kabla ya safari kuelekea Iringa

In short inabidi tuwe na separate thread ya kulijadili jeshi letu
 
By the way Mzee Kimario yuko hai haya mamabo ta FM kuua watu ilihali wako hai ni aibu

halafu mnataka mpewe nchi!
 
RIP General Luahanga!

Habari kutoka Iringa kuwa Rais Jakaya Kikwete atahudhiria mazishi yatakayo fanyika Kijiji cha Tanangozi Km 25 kutoka Iringa Mjini!
 
..wakuu niliteleza. samahani sana. Major General Muhidin Kimario yuko hai.
 
Makamanda wengi wa kijeshi tuliokuwa nao miaka ya sabini wanaonekana kuwa walikuwa wazuri sana kuliko leo kwa sababu kama ile ile tunayosema kuwa walimu wa miaka hiyo walikuwa wazuri, elimu ya miaka hiyo ilikuwa nzuri, na viongozi wa kisasa wa wakati huo walikuwa wazuri.

Ninadhani kuwa credit kubwa sana iende kwa viongozi wa juu wa kisiasa tuliokuwa nao wakati ule, kwani ndio waliokuwa kioo cha wengine wote. Hata leo hii tukifanikiwa kuwaondoa viongozi wabaya wote na kukata rushwa za aina yote ili watu waishi kwa kutegemea mishahara yao, na mishahara hiyo iwe mizuri, utaona mapolisi, waalimu wanajeshi na wataalamu wengine wanaouhudumia umma watafanya kazi zao vizuri sana. Sumu ya rushwa, tamaa ya mapato ya haraka haraka na maisha yasiyokuwa realistic ndivyo vilivyoleta matatzo yote haya.
 
Makamanda wengi wa kijeshi tuliokuwa nao miaka ya sabini wanaonekana kuwa walikuwa wazuri sana kuliko leo kwa sababu kama ile ile tunayosema kuwa walimu wa miaka hiyo walikuwa wazuri, elimu ya miaka hiyo ilikuwa nzuri, na viongozi wa kisasa wa wakati huo walikuwa wazuri.

Ninadhani kuwa credit kubwa sana iende kwa viongozi wa juu wa kisiasa tuliokuwa nao wakati ule, kwani ndio waliokuwa kioo cha wengine wote. Hata leo hii tukifanikiwa kuwaondoa viongozi wabaya wote na kukata rushwa za aina yote ili watu wasihi kwa kutegemea mishahara yao, na mishahara hiyo iwe mizuri, utaona mapolisi, waalimu wanajeshi na wataalamu wengine wanaouhudumia umma watafanya kazi zao vizuri sana. Sumu ya rushwa, mapato ya haraka haraka na maisha yasiyokuwa realistic ndivyo vilivyoleta matatzo yote haya.
Nakubaliana kabisa na wewe...leadership is everything.Sasa hivi tunawapiga soga na hadithi tu kila eneo.
 
Makamanda wengi wa kijeshi tuliokuwa nao miaka ya sabini wanaonekana kuwa walikuwa wazuri sana kuliko leo kwa sababu kama ile ile tunayosema kuwa walimu wa miaka hiyo walikuwa wazuri, elimu ya miaka hiyo ilikuwa nzuri, na viongozi wa kisasa wa wakati huo walikuwa wazuri...............

...sina hakika unawazungumzia akina nani in specific.....however, makamanda waliopo sasa wengi wao walikuwepo mika hiyo ya sabini lakini kwenye rank za chini (lutenis, kaptenis na majors).....na waliopo sasa ni matunda ya hao hao ambao umewasema hapo juu.........

RIP Luhanga
 
...sina hakika unawazungumzia akina nani in specific.....however, makamanda waliopo sasa wengi wao walikuwepo mika hiyo ya sabini lakini kwenye rank za chini (lutenis, kaptenis na majors).....na waliopo sasa ni matunda ya hao hao ambao umewasema hapo juu.........

RIP Luhanga

Ni kama ambavyo Kingunge na Mkapa walivyokuwa wanasiasa wazuri sana wakati huow akiwa hawana hata doa la ufisadi.
 
Kama mpiganaji wa porini nipo nikiwaza nchi itapata lini wapiganaji wazuri na ambao ni wazalendo kama mheshimiwa Luhanga aliyefariki jana ambaye alimfanya hadi Marehemu Raisi wa Msumbiji Samora Machel atembelee mkoa wa Iringa na atoe hotuba ndefu ya masaa matano kwenye uwanja uliopewa jina la Samora Kufuatia ziara ile.

Samora alimpenda sana Luhanga na alikuwa mshauri wake binafsi wa kivita lakini alipotaka amchukue moja kwa moja Luhanga alikataa.

Ziara yake ile ya Samora Iringa mojawapo ya agenda kuu zilizokuwa zimemleta alikuwa akitafuta uwezekano wa kumshawishi Luhanga kwa kupitia wazee Fulani wawili ahamie msumbiji.Angeshinda ajenda yake lakini kilichotibua ni kuwa Angola walikuwa na kambi yao kule Kijiji cha Mgagao Iringa na mkuu wa kule naye akatumwa kuwa Angola Akina Augustino Neto walikuwa wakimhitaji akawe mkuu wa kikosi vita cha Anga kule .Nyerere akapata Taarifa akamtuma mkuu moja wa usalama wa Taifa Mzena ambaye alikuwa ni wa Iringa amwambie Luhanga kuwa asikubali ombi la waangola na la Samora.Nyerere alichukia kitendo chao cha wao kwenda kumrubuni mtu moja kwa moja badala ya kuomba kupitia kwake.

Jeshini Tulizoea kumwita “Kamanda Ngumi.mkononi” kwani alikuwa na msemo kuwa silaha bora kuliko zote duniani ni ngumi ya mkononi.Alikuwa akipiga ngumi mtu lazima azimie haijalishi ni askari au ni raia.Alikuwa anajua kupigana ngumi kiwango ambacho sijamwona mtu wa namna hiyo maisha yangu yote.Nilifundishwa naye "one to one combat techniques "kwenye kozi moja.Alitufundisha jinsi ya kutumia pistol na ngumi akituonya tuepuke judo au karate tukiwa karibu na adui. Alitusihi tupende ngumi zaidi kwani ngumi ndiyo silaha ya uhakika ya kummaliza mtu kuliko judo au karate za wachina na wajapani kwenye mapigano ya ana kwa ana.Sikuamini kuwa yeye ni rubani wa ndege za kivita kwa jinsi alivyomudu somo lile.Kila mwanafunzi aliyefundisha naye toka wakati ule alipenda ngumi mno.Siku hizi askari wengi ngumi hawawezi sana wanajua kutumia virungu,mikanda na silaha na kidogo labda kuruka ruka vijudo na vikarate vya kubabaishia kama yule aliyerusha kamguu ka kikarate au kijudo ka kubabaishia Raisi Mwinyi alipolambwa kibao na kijana kwenye mkutano wa waislamu.

Luhanga alikuwa msomi bora wa kivita aliyependa vita kulipo pesa au mshahara au marupurupu.Jeshi lilikuwa kwenye damu si pesa si cheo.Alikuwa mzalendo hasa.Alipigana vita ya UGANDA na Tanzania na ilikuwa nusura ampige ngumi na kuua kiongozi dhaifu wa vita toka Zanzibar ambaye kutokana na ugoi goi wake aliongoza vibaya kikosi wengi wakateketezwa na adui.Baada ya wengi kuteteketea Luhanga alitoa pistol akafuata mnzazibari yule huku akiwa na ngumi mkononi tayari kwa one two one combat na mnzazibari yule aliyesababisha kushindwa kwa kikosi kile kivita mwazo kabisa wa vita ile.Nyerere nafikiri aliamuru arudishwe nyuma ya vita na akaamua ampe vyeo vya kisiasa asije akawabonda na ngumi zake makamanda wavivu wa kijeshi basi akaishia kuwa mkuu wa mikoa mbalimbali huku akijinywea pombe zake akiendelea kusubiria kufariki kwake hadi alipofariki kifo kilipomkuta hapo hapo kwao Iringa.

Huko unakoenda kaendelee kupigana. Ukikuta shetani Linalotaka kukupeleka motoni kama liko litandike ngumi usisahau one to one combat.

I salute you fellow fighter major general James Luhanga. I salute you again Kamanda Ngumi Mkononi.

Kwa waliobaki hivi hawa makamanda wa majeshi wanajulikana kama kamanda nani zaidi ya majina yao? Nawakumbuka akina kamanda mti mkavu n.k kwa jinsi walivyopewa majina kufuatana na uhodari wao katika mapambano.Walikuwa sit u na majina yao binafsi lakini pia walikuwa na majina yatokanayo na uhodari wa medani za mapambano.

Kamanda Nyerere alijulikana kama Mwalimu kutokana na uhodari wake katika maeneo kibao.

Hivi Kamanda Kikwete jina lake lingine alilopewa kutokana na uhodari wake kikazi ni kamanda nani vile? Silikumbuki anayelikumbuka humu jamii forum anitajie nakumbuka la LUHANGA NA NYERERE naomba msaada mnitajie la Kikwete.
God Bless His Heart this Great Tanzanian! My brother if you were taught by this grat man, it's very sad that this is all you can attribute to the great General the country ever produced. General Luhanga is a genttleman I know very well, as professional airforce fighter, a commandant, a Member of Parliament, A Board Chair of the then Air Tanzania, and A Chief Regional Executive, My God what a loss, He continued mentoring many of us unlike your assertion that he retired into drinking!
 
Back
Top Bottom