Kifo cha Mkulima

Tamu3

Member
Feb 17, 2023
25
16
KIFO CHA MKULIMA

1.
Hadithi nawaletea, sikiliza kwa makini,
Zamani kulitokea, porini kundi la nyani,
Mitini walirukia, mara juu mara chini,
Nyani walifurahia, kwa kifo cha mkulima.

2.
Waliposikia njaa, lienda huko shambani,
Mahindi wakachukua, kurudi nayo porini,
Wakanywa na maji pia, kwenye mti kivulini,
Nyani walifurahia, kwa kifo cha mkulima.

3.
Mkulima alijua, wafanyacho hawo nyani,
Aliapa kuwaua, akashikwa na huzini,
Mitego akanunua, akafukia shambani,
Nyani walifurahia, kwa kifo cha mkulima.

4.
Nyani aliwachukia, wizi mahindi shambani,
Kisasi aliapia, wote kuangamizeni,
Mitego alifukia, shamba lake ardhini,
Nyani walifurahia, kwa kifo cha mkulima.

5.
Nyani wapatao saba, walinaswa mtegoni,
Shingoni ikawakaba, walikatwa mikiani,
Wakawa wenye jazba, hawendi tena shambani,
Nyani walifurahia, kwa kifo cha mkulima.

6.
Wakawa kule porini, hawendi tena shambani,
Kila matunda porini, japo hawayatamani,
Mahindi shindwa kuleni, mkulima hana dini,
Nyani walifurahia, kwa kifo cha mkulima.

7.
Wiki mbili zikapita, alikufa mkulima,
Nyoka wa miraba sita, alikuwa memuuma,
Nyani wote lijiita, shambani kwa mkulima,
Nyani walifurahia, kwa kifo cha mkulima.

8.
Mahindi walikuleni, pasipo kipingamizi,
Lishinda mule shambani, kwa uhuru na uwazi,
Ilipofika jioni, lipanda kwenye minazi,
Nyani walifurahia, kwa kifo cha mkulima.

9.
Mwaka mwingine lipita, tangu kifo kutokea,
Chakula hawakupata, nyani wote walilia,
Kila pori walifwata, mahindi wakihemea,
Nyani walifurahia, kwa kifo cha mkulima.

10.
Wakawa wanajutia, kwa kifo cha mkulima,
Wakaanza kutambua, kumbe anayo heshima,
Ujumbe wakautoa, kumpenda mkulima,
Nyani walifurahia, kwa kifo cha mkulima.

Denny Jeremias Kitumbika
Mtunzi wa mashairi na ngano za Kiafrika
Mufindi Tanzania 8.7.2023

1710780378202.jpg
 
WENGI WANAFURAHI MAHINDI KUSHUKA BEI HADI 18ALFU KWA GUNIA DEBE 2500 HAWAJUI KWAMBA MKULIMA ANAKATA MTAJI NA ATAPUNGUZA KULIMA WENGNE KUACHA KABISA KULIMA WENGNE KUBDILI AINA YA MAZAO YA KULIMA NA C MAHNDI TENA
 
Back
Top Bottom