Kifo cha Mbunge Regia si mapenzi ya Mungu

Kifo cha Mbunge Regia si mapenzi ya Mungu

Kuboresha barabara kunapunguza tu ajali but hakuzuii ajali!
 
japo umeandika ndefu sana ki ukweli nitasoma baadae......
kwa sasa nideal na kichwa cha habari.....
Tumuache Regia apumzike kwa amani......tumuombee......na sisi tujiandae kwa sababu ni njia ya wote.....
si wakati wa kutafuta mchawi ni nani....

badala ya kujihoji na yeye ataagwa karimjee ama kule kwa mfuga mbwa na umati kiasi gani
anaanza kumjadili dada wa watu ambae anacheza karata za albastini na malaika sasa hivi
hope asikii wanachojadili
 
Asilimia 70 ya vifo vya afrika sio vya Mungu ni human error!
 
Well said rev.fr.karugendo, umenifungua macho wana jf naomba from this thread tuchukue hatua madhubuti juu ya hyo barabara
 
Kifo ni kifo tu kiwe ajali au kurogwa yes kuna mambo mengi ya msingi ya kuhoji iwe kabla ama baada ya kifo,mfano mzuri zaidi ni kwa vifo vivyotokana na ajali za barabarani ninavyoelewa ajali hizi nyingi. Kama si zote husababishwa na ama uwajibikaji wa moja kwa moja wa watendaji au watumiaji wa barabara ama chombo cha usafiri kilichohusika na ajali hiyo au kutowajibika kwa namna moja au ingine na pande hizo mbili. Watendaji kwa maana ya serikali,taasisi,na umma kwa ujumla wake,ikiwa ni case ya utengenezaji mbovu wa barabara,uingizwaji wa gurudumu hafifu au vyombo chakavu hapo ni lazima kundi hili likubali uhusika wa moja kwa moja kufanikisha ajali au kifo husika ila kama ni ubovu wa barabara kushindwa kudhibiti mwenendo wa vyombo vya usafiri,hapo kosa ni kushindwa kuwajibika ila hakuna unafiki unaofariji na kukutenga mbali na dhambi yako ama ya kuwajibika ama kutowajibika kama kumbebesha MUNGU kile ambacho kwa binaadamu kimeisha kuwa juu ya uwezo, MUNGU awarehemu wote waliopoteza uhai wao kwenye mzunguko huo ambao bado hatujui hatma yake
 
Priva,
mimi huwa navavaa kofia 1 kati ya 2 nilizonazo, 1. kiimani 2. ya kisayansi. Na hizi kofia ndio zilizotupelekea kupata kanisa katoliki na orthodox. Kuna hoja nzito huwa zinajadiliwa Radio maria kuhusu utoaji mimba mfano yaani hata kama mama ana mimba ya miezi 4 akapata ajali/ugonjwa ambapo ili kumnusuru maisha yake madaktari wanashuri ni lazima mimba itolewe, msimamo wa kanisa ni kwamba mwenye kutoa uhai ni mungu pekee na kile kiumbe cha miezi 4 na mama wote ni sawa kwa mungu... na hivyo ukitoa uhai wa mmmoja wapo utakuwa umevunja amri ya 5. Sasa hapa mama akifa tena tutasema ni mipango ya mungu!

Nadhani sasa ni wakati wa kuingiza sayansi katika imani zetu.
 
Mkuu,

Una point nzuri sana na muhimu. Sidhani kama kulikuwa na haja ya kuihusisha na kifo cha Regia.

Tulisjaijadili sana hii habari za vifo kwa ajali. Kuna makala nyingi za barabara na ajali na nini kifanyike humu ndani.

Juzi juzi nimepata habari School Mate wangu, Mhandisi wa Ujenzi kupitia UDSM, Cornelius Bukuru amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo hapo Dar. Alikuwa ni mhandisi wa wilaya huko Karagwe. Alipouguwa na kupelekwa Hospital, akakuta vifaa vya kumhudumia vimewekwa Store na mwenye funguo hayupo. Walipomtafuta hadi kumpata na akaja kufungua, mtu akawa ameshaondoka.

Tutalaumu vifo vya barabarani tu lakini wa ujumla, vifo vya kizembe Tanzania ni vingi sana.

Inabidi mjadala uwe mpana zaidi na usiishe ajali tu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Speed ,kupiga overtake sehemu ambayo huoni nini kinakuja au kujaribu kuliwahi gari linalokuja mbele,ubora wa gari,haswa kwenye matairi ,mafunZo ya udereva na kujua sheria na nidhamu kwenye uendeshaji , hayo ndio mambo makubwa yanayo changia kusababisha ajali nyingi. Suala la barabara sita nane , linaweza lisiwe tatizo kama uzingatiaji wa hayo niliyo sema.
 
Back
Top Bottom