Kifo cha Mbunge Regia si mapenzi ya Mungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo cha Mbunge Regia si mapenzi ya Mungu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by amkawewe, Jan 19, 2012.

 1. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Privatus Karugendo


  JANUARI 14, mwaka huu, ni siku ambayo ajali ya barabarani iliyakatisha maisha ya Regia Mtema, Mbunge wa Vitimaalumu kupitia CHADEMA, ilikuwa ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwangu nikiwa nimefikisha miaka 56.

  Ndugu, jamaa na marafiki walinitumia salaam za kunitakia heri, wengine walinipongeza kuvuka wastani wa kuishi wa Mtanzania, tunaambiwa kwamba miaka 43 ndiyo wastani wa kuishi wa Mtanzania?

  Mimi na wengine tuliovuka wastani wa kuishi wa Mtanzania tunawajibika kumshukuru Mungu, maana si kwa ubora wetu bali kwa neema yake; rafiki zangu wa mtandao wa facebook walitia fora maana hadi leo nilikuwa nimepokea ujumbe wa kunitakia heri ya "birthday" kutoka kwa watu 350.
  Kati ya hao, rafiki yangu kutoka Tabora alinitumia ujumbe ufuatao: "Karugendo, hongera kufikisha miaka 56 ya kuzaliwa, kumbuka kadiri miaka inavyoongezeka ndivyo unavyolikaribia kaburi.."

  Nami nikamjibu; "Asante kwa matashi mema. Zamani tulifikiri kulisogelea kaburi inaendana na umri mkubwa, ila siku hizi mambo ni tofauti. Vijana wanakufa kwa ajali, ukimwi na magonjwa mengine yanayosababishwa na kemikali zinazochanganywa kwenye vyakula, vinywaji na dawa bandia.."
  Kabla sijamaliza kusoma salaam zangu za "birthday" nilipata habari za kushitusha kuhusu kifo cha Regia Mtema, kijana ambaye kufuatana na mawazo ya rafiki yangu wa Tabora, umri wake wa miaka 32 ulikuwa si wa kulikaribia kaburi.

  Alikuwa bado mdogo, mwenye matumaini ya kuendelea kuishi miaka mingi mbele, wanaomfahamu vizuri wanasema alikuwa amepania mwaka huu uwe ni wa kuwahamasisha vijana kufanya kazi.

  Alitaka kuwashawishi vijana kuachana na tabia za kukaa vijiweni na kutegemea miujiza kutoka mbinguni. Maisha yake yamekatishwa na ajali ya barabarani. Inasikitisha taifa kumpoteza kijana aina ya Regia, ambaye alionyesha wazi kuwa ni hazina kubwa ya kuchangia maendeleo ya taifa.
  Mbali na kumfahamu Regia, kupitia kwenye vyombo vya habari na kushuhudia mchango wake wa mawazo katika matukio mbalimbali na hata bungeni, alikuwa rafiki yangu katika mtandao wa "facebook".

  Yeye ni kati ya watu walionitumia ujumbe wa heri wakati wa kukumbuka ya siku ya kuzaliwa kwangu. Ni imani yangu kwamba ujumbe huo aliuandika muda mfupi kabla ya kuanza safari yake hiyo iliyoyakatisha maisha yake.

  Aliniombea maisha marefu na kunihakikisha kwamba vijana wanafuata nyayo zetu sisi wazee katika harakati za kulijenga taifa. Wakati nikiusoma ujumbe wa Regia, kumbe yeye alikuwa akiaga dunia.

  Dk. Wilbroad Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA wakati akitoa rambirambi zake kuhusu kifo cha Regia alisema kimewasononesha na kuleta huzuni kwa taifa zima, lakini kwa vile ni mpango wa Mungu, hatuwezi kuhoji.

  Namheshimu Dk. Slaa na ninatambua vizuri uwezo wake wa kujenga hoja na kuzisimamia. Ninafahamu vizuri kwamba yeye ni mwanatheolojia aliyebobea.

  Bahati mbaya ni kwamba theolojia yake hii ya "Kazi ya Mungu haina makosa"... "Bwana ametoa, Bwana ametwaa" imepitwa na wakati! Kadiri siku zinavyosonga mbele, mwanadamu anakimbizana na maendeleo ya kasi ya sayansi na teknolojia na kwa hiyo, ni lazima tuwe na theolojia inayokwenda na wakati. Najua siku nikikutana na Dk. Slaa tutabishana juu ya hoja hii hadi kieleweke.

  Mbali na Dk. Slaa, ukisikiliza ujumbe unaotolewa redioni na kuandikwa kwenye magazeti ni ule ule wa "Kazi ya Mungu, haina makosa". Hivyo mawazo kama haya ninayoyatoa yanayoelekea kuhoji kazi ya Mungu, ni lazima yatapokewa kwa hisia tofauti.

  Ninalijua hili, lakini ni lazima awepo mtu wa kuanzisha mjadala. Na kwa kawaida, kuanzisha kitu si kazi nzuri wakati wote, maana kuna kutukanwa mambo yanapokwenda vibaya. Kitulizo ni kwamba kilichoandikwa kimeandikwa. Leo watatukana na kuweka pembeni, lakini kesho na keshokutwa watasoma na kufurahi.

  Mambo mengi yanayokatisha maisha ya watu hapa Tanzania, si mpango wa Mungu na wala si kazi ya Mungu, bali ni kazi yetu sisi wenyewe. Jambo hili ni lazima tulieleze bila kuogopa maana kinyume cha hapo ni kuendelea kuwapumbaza watu.

  Ajali kama hii iliyokatisha maisha ya Regia Mtema, si mpango wa Mungu. Ni dhambi kubwa kusema kwamba huu ni mpango wa Mungu. Kama barabara ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, ingekuwa ni ya njia nne, ajali kama hii ya Regia Mtema na nyingine nyingi zinazotokea kila wakati kwenye barabara hii zisingetokea.

  Wataalamu wanasema kutokana na wingi wa magari yanayotoka na kuingia Dar es Salaam kila siku ya Mungu, ni uzembe kuendelea kuwa na aina ya barabara tuliyonayo kwa sasa ya magari kupishana. Tutake-tusitake ni lazima ajali zitaendelea kutokea.

  Ajali zikitokea, tunasema Mpango wa Mungu hauna makosa? Na kwamba hatuwezi kuhoji kazi ya Mungu! Theolojia ya aina hii ni ya kuwekwa pembeni kabisa! Mungu anatuumba tuwe na uzima tena tuwe nao tele. Mpango wa Mungu ni uzima tele, kinyume cha hapo ni kutoka kwa yule mwovu.

  Tunaachia magari mengi yanaingizwa nchini, bila kuwa na mpango wa kupanua barabara, tunategemea nini? Kama si foleni, basi ni ajali za kila siku. Ni makosa makubwa kusema foleni na ajali zinazosababishwa na uzembe wetu wa kushindwa kupanua barabara zetu miaka 50 baada ya uhuru wetu, ni kazi ya Mungu na haina makosa.

  Namkumbusha Dk. Slaa, kitu anachokijua mwenyewe. Ni lazima tusimame na kuhoji ni kwa nini maisha ya Watanzania yanaendelea kupotea kwenye ajali za barabarani.

  Tukifanya hivyo, haina maana imani yetu imekwenda tenge, kuhoji kazi ya Mungu. Ni haki yetu kuhoji tena kwa ukali. Mungu amefanya yote, ameiumba Tanzania ikiwa na rasilimali nyingi, ametupatia akili ya kuzaliwa na kipaji cha kujifunza mambo mapya na kuwa wavumbuzi, ametupatia uwezo wa kuutiisha ulimwengu.

  Iweje leo hii tunashindwa kuwa na barabara nzuri, kubwa na pana zinazoweza kuruhusu magari kukimbia bila kukutana wala kugusana. Tatizo letu ni kupanga vipaumbele. Tukiyaweka maisha ya Watanzania kuwa kipaumbele namba moja, ni lazima ajali za barabarani zitakoma.

  Ni lazima tusimame na kuihoji Serikali yetu iliyo madarakani. Je, maisha ya Watanzania ni kipaumbele namba moja? Mtu akifa kwa ajali ni lazima tuhoji kwa ukali kabisa, albino akichinjwa ni lazima tusimame na kuhoji, hatuwezi kusema kwamba kuyakatisha maisha ya albino kwa imani za kishirikina ni kazi ya Mungu, mtu akifa kwa malaria ni lazima tuhoji kwa ukali, watoto wachanga wakipoteza maisha ni lazima tusimame na kuhoji kwa ukali, mwanamke akipoteza maisha wakati wa kujifungua ni lazima tusimame na kuuliza kwa ukali kabisa.

  Katika dunia hii ya maendeleo ya sayansi na teknolojia mwanamke kupoteza maisha wakati wa kujifungua si kazi ya Mungu, ni kazi yetu sisi. Ni lazima tuijutie na kupiga magoti kuomba toba kwa muumba wetu.

  Tunaachia dawa bandia zinaingizwa nchini. Watu wanazitumia dawa hizi, matokeo yake wanaugua saratani pamoja na magonjwa mengine hatari. Wakifa, tuseme ni mpango wa Mungu, hauna makosa na haturuhusiwi kuhoji?

  Baadhi ya vyakula tunavyonunua madukani vimejaa kemikali za hatari. Hatuna mpango imara wa kudhibiti vyakula hivi, ili kuhakikisha ni salama kwa matumizi ya binadamu. Wale wanaohusika na kupima vyakula hivi wakihongwa ‘vijisenti' kidogo wanaachia vinapita na kusambaa nchi nzima. Samaki wa mionzi kutoka Japan walifika hadi Morogoro. Kesho na keshokutwa vyakula hivi vikisababisha vifo tuseme ni mpango wa Mungu, kwamba bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe milele!

  Theolojia hii ni ya kutupwa kabisa na isionekane tena hapa duniani. Sina lengo la kupinga nguvu za Mwenyezi Mungu. Ninafahamu kwamba yeye ni Muumba wa Mbingu na nchi, ambaye anaumba vinavyoonekana na visivyoonekana. Hoja yangu ni kwamba hata yale ambayo Mungu ameyaweka kwenye himaya yetu, tukishindwa kuyatekeleza kwa uzembe wetu, tunayasukuma kwake.

  Tunaruhusu matairi bandia yanaingizwa nchini. Matairi haya yakipasuka, magari yakapinduka na watu wakafa, tuomboleze kwa kusema ni mpango wa Mungu: Bwana ametoa, bwana ametwaa? Kusema kweli ajali na vifo vingi hapa Tanzania ni vya kujitakia na wala si mpango wa Mungu. Tunamsingizia Mungu kwa uzembe wetu na kukwepa wajibu wetu wa kuzipanua barabara zetu. Tunamsingizia Mungu kwa uzembe wetu wa kushindwa kudhibiti bidhaa bandia.

  Tunashabikia magari ya mitumba na kununua vitu chakavu. Wabunge walijadili na kupitisha sheria ya kununua vifaa vichakavu. Wanataka tununue magari ya mitumba, meli za mitumba ndege za mitumba.

  Vitu hivi vichakavu vikileta hatari na kusababisha maisha ya Watanzania kupotea, tuseme ni kazi ya Mungu haina makosa? Ni kukwepa wajibu wetu na kumbebesha Mungu huyu mizigo isiyokuwa ya kwake.

  Kifo cha Regia Mtema, kimetusikitisha na kutuletea majonzi makubwa. Kama alivyosema Kabwe Zitto, huyu alikuwa mbunge kijana ambaye ni mara yake ya kwanza kuingia bungeni. Alikuwa na mpango wa kufanya mambo mengi, lakini maisha yake yamekatishwa kwa ajali ya barabarani.
  Wale wanaofuatilia mambo ya siasa za Tanzania, watakubaliana nami kwamba Regia Mtema, alikuwa hafungwi na mipaka ya chama chake. Ni mbunge aliyekuwa akitetea haki za walemavu, vijana na wanawake wote wa Tanzania, bila kuangalia chama.

  Rais Jakaya Kikwete pamoja na viongozi wengine wa Serikali na vyama vya siasa wamemsifia Regia Mtema, kuwa miongoni mwa wazalendo wa Tanzania wenye jitihada binafsi za kuleta umoja na mshikamano katika taifa.

  Wazalendo wanaolitanguliza taifa mbele kabla ya kitu chochote kile. Wanatanguliza taifa kabla ya chama chao cha siasa, wanatanguliza taifa kabla ya tumbo lao na familia zao.

  Hivyo wakati tunamlilia Regia Mtema, tuache utamaduni huu wa Kazi ya Mungu haina makosa. Tukubali makosa yetu, tukubali kwamba kwa namna mmoja ama nyingine tumechangia kifo cha kijana huyu na wengine wanaokufa kwa vifo vinavyoweza kuzuilika.

  Uchungu tulionao utusukume kuanza kufanya uamuzi wa kulijenga taifa kwa viwango vinavyostahili. Mungu amlaze mahali pema peponi ndugu yetu, rafiki yetu, mwanaharakati na mzalendo wa kweli wa Tanzania, Regia Mtema.

  Amina.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  japo umeandika ndefu sana ki ukweli nitasoma baadae......
  kwa sasa nideal na kichwa cha habari.....
  Tumuache Regia apumzike kwa amani......tumuombee......na sisi tujiandae kwa sababu ni njia ya wote.....
  si wakati wa kutafuta mchawi ni nani....
   
 3. b

  bakene Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Well said, mr karugendo.
   
 4. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  well said Preta!
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Preta,

  Utakaporudi isome hadi mwisho, nina uhakika ukiimaliza uta edit hii comment yako kama si kuifuta kabisa.
   
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  ZD,

  Na wewe mama hujamsoma Padre Karugendo. Jitahidi umsome kuna maneno mazito sana ya busara.
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  ndio maana nikatanguliza kusema......nadeal na kichwa cha habari pekee.....
  nitarudi kusoma habari yenyewe na nitacomment vilevile.....
  heshima yako sana mkuu.....
   
 8. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  sawa dady.Ila nimesoma baadhi ya mistari kama "matairi ya kichina" nikaelewa kiasi.Nitajitahidi niisome yote.Btw...mbona ulinidanganya?
   
 9. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,016
  Trophy Points: 280
  he is completely wrong, ajari zipo hata ktk nchi zenye barabara 6 na maxmum 24x7 traffic wakiwa na vifaa vyote.
  Princess diana alikufa kwa ajari, sokoine, chacha n.k kwa juzi kati mapadre wa kiitaliano nao walikufa.
  Kumsingizia regia kwamba ni uzembe ni injustice na hayupo kusema exctly whats happened mimi na wewe hatukuwepo
   
 10. M

  Masuke JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Nakushauri usome habari yote halafu ndo uweke comment yako.
   
 11. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #11
  Jan 19, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Busara zilizo jaa humu zimeniacha nakuna kichwa. Kapumzike kwa amani Regia kifo chako sio bahati mbaya, kimepangwa.
   
 12. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  ur wrong..damn wrong! sababu hujawahi pata ajali au?
   
 13. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,116
  Trophy Points: 280
  Well said, lakini maneno hayo ya busara kwa aina ya viongozi tulionao ni bora hata kumpigia mbuzi gitaaa.
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Fanyeni some editing basi...
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Umesoma heading tu na kukimbilia kusonga mbele ku comment.
  Soma content yake utamuelewa Padre Karugendo.
   
 16. +255

  +255 JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Rudi uisome hy post, sio kusoma title na kukimbia
   
 17. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mama kamalizie palipobaki.

  Btw, Daddy hadanganyi, unatakiwa kuomba msamaha kwa kumdanganya Daddy!
   
 19. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Preta,
  Heshima mbele kama tai.

  Unaniangusha rafiki, jitahidi kusoma content, vichwa vya habari bongo ni utata, na ukizingatia ametajwa Mungu, unaweza kujikuta unachangia kitu tofauti.
   
 20. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe kabisa! Ila natofautiana na wewe kwenye kuhoji pale kinapotokea kifo. Mimi nadhani badala ya kuhoji, tuwajibike kwa nafasi zetu na kuchukua hatua. Mwenye dhamana ya usalama barabarani na ujenzi wa barabarani wanapoonekana wameshindwa kuwa wabunifu na watekelezaji wa mambo yanayotuhakikishia usalama, wakae pembeni, tuwaweke wengine hadi pale tutakapopata best fit. Na sisi wananchi tukiona tatizo ni serikali, basi tuwajibike kwa kukiwajibisha chama kinachoiunda hiyo serikali kwa kuweka chama mbadala kitakachounda serikali makini.

  Na mtazamo wangu ni kwamba, tutaendelea kutaabika na kufa hovyo hadi pale tutakapoiwajibisha serikali ya ccm kwa kuiweka pembeni maana imeshindwa kabisa kuwalinda raia wake.

  Tuwatoe, tuijaribu cdm!
   
Loading...