Kifo cha Magufuli, Tanzania ilipata hasara ya karne moja, maumivu yake yatawafikia hata walioshangilia

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,755
15,238
1.Miezi miwili tu baada ya hiyo tarehe kampuni ya symbion ililipwa zaidi ya billioni 349 na mafisadi kuachiwa licha ya bunge kutoa azimio symbion wasilipwe na waliohusika wafungwe.

2. Licha ya bandari ya Dares salaam kuboreshwa hadi kufikia meli kubwa ya mita 300 kuweza kutia nanga hapo lakini bado wakubwa serikalini hawalitangazi hilo maana tayari walishakula 10% na kuiuza kwa mwarabu.

3. Kesi zote sasa Tanzania lazima ishindwe na ilipe mabilioni ya pesa za walipa kodi masikini wa Tanzania maana wakubwa ndani ya serikali wanajilipa kupitia makampuni hayo.

4. Bunge , Serikali wamehongwa kwa kununuliwa pikipiki zenye nembo ya rais Samia ili waweze kufanyia kampeni za uchaguzi wa mwaka 2025 kwa gharama ya kuuza bandari zote za Tanganyika.

5. Tanzania ya kabla ya hiyo tarehe 17 ilikuwa Tanzania ya viwanda na vilionekana vikimea kila mahali na kuleta maelfu ya ajira kwa vijana hadi nchi ikaingia uchumi wa kati, Tanzania ya baada ya hiyo tarehe haieleweki inasimamia nini, kila kona vinajengwa vituo vya mafuta bila kuzingatia sheria ya mita 500 kutoka kituo hadi kituo na hakuna anayejali!

6. Tanzania iliyokuwa na uwezo wa kujenga miradi mikubwa kama bwawa la umeme ,reli ya umeme, sasa viongozi wake wanasema haijiwezi kwa lolote kabisa na kila kitu lazima waje waarabu kutuendeshea!.

My take.
Gharama za kumpoteza Magufuli zilikuwa kubwa ndiyo maana wenye akili za kuona mbali tulilia sana kwani tulijua fika Tanzania ilimhitaji Magufuli kuliko Magufuli alivyokuwa anaihitaji.
 
Dikteta ndo alifuta mikataba ya kampuni za madini kipuuzi sasa hivi tunalipishwa mabilioni na mahakama. Yeye na Profesa mpuuzi Mruma walitudanganya tunaidai Barric trilioni 495.. alitumia mabilioni ya Tsh kujijengea Airport kijijini kwake. Hata stendi ya Magufuli ilivyojengwa kibabe ni suala la muda tu itahamishwa tena.
 
Allah kampenda mja wake were ni nani uzungumze kwamba ni hasara kwa TAIFA,
MPANGO WA MUNGU MARA ZOTE NI WA HEKIMA NA BARAKA ZA KIPEKEE!,
ILIKUWA SIKU YA BARAKA ILIYO KUU,KWA SISI TUNAOMUAMINI MUNGU,NA NYIE WA MAMBO YA KIDUNIA MNAIITA SIKU YA HASARA.
 
Dikteta ndo alifuta mikataba ya kampuni za madini kipuuzi sasa hivi tunalipishwa mabilioni na mahakama. Yeye na Profesa mpuuzi Mruma walitudanganya tunaidai Barric trilioni 495.. alitumia mabilioni ya Tsh kujijengea Airport kijijini kwake. Hata stendi ya Magufuli ilivyojengwa kibabe ni suala la muda tu itahamishwa tena.Uhuru wa uchumi unagharama zake
Acha ujinga wewe!

Mikataba ya kijinga iliyoingiwa yote ni bora ikafutwa tukaanza upya, Ni aheri kuwalipa na tukafuta wawekezaji tukaingia mikataba yenye tija
 
Tarehe 17.03.2021 ilipotangazwa kifo cha Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Watanzania walipata hasara ya karne ambayo haiwezi kufidiwa,

Katikati ya mjadala mkubwa wa bandari za Tanganyika kuuzwa kwa Waarabu,malalamiko ya Wananchi lakini ndio kwanza tunaonyeshwa ndege ya Rais inatua Dubai na baadae kupelekea Saudi Arabia lakini tunaambiwa kila Weekend Rais uwa anakwenda Dubai yaani anafanya safari huko huko kwa tunaowalalamikia,Rais wetu hatujali kabisa. Hana uzalendo wala uchungu wa lolote lile.
 
Ubaya zaidi ni kutokana na uwezo waliopewa JWTZ kutetea yeyote alie madarakani haijalishi upstairs yupoje.
 
Radar inaonyesha uelekeo wa ndege yatu
 

Attachments

  • IMG-20230729-WA0200.jpg
    IMG-20230729-WA0200.jpg
    26.9 KB · Views: 12
  • IMG-20230729-WA0197.jpg
    IMG-20230729-WA0197.jpg
    60.5 KB · Views: 10
  • IMG-20230729-WA0197.jpg
    IMG-20230729-WA0197.jpg
    60.5 KB · Views: 11
  • IMG-20230729-WA0198.jpg
    IMG-20230729-WA0198.jpg
    47 KB · Views: 10
Tarehe 17.03.2021 ilipotangazwa kifo cha Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Watanzania walipata hasara ya karne ambayo haiwezi kufidiwa,

Katikati ya mjadala mkubwa wa bandari za Tanganyika kuuzwa kwa Waarabu,malalamiko ya Wananchi lakini ndio kwanza tunaonyeshwa ndege ya Rais inatua Dubai na baadae kupelekea Saudi Arabia lakini tunaambiwa kila Weekend Rais uwa anakwenda Dubai yaani anafanya safari huko huko kwa tunaowalalamikia,Rais wetu hatujali kabisa. Hana uzalendo wala uchungu wa lolote lile.
Ni hasara mno, miaka itaenda, watapita watawala wengi lakini trh 17.3.2021 itabaki kuwa hasara kwa ukombozi wa pili wa Tanzania baada ya ukombozi wa mwalimu Nyerere
 
Back
Top Bottom