Kifo cha kampuni ya Business Times Ltd

Sisi kwetu katika uislamu,hilo wala haliwi tatizo kwa sababu watoto halali wenye kurithi ni hao wa mke wa ndoa tu.Na mirathi ni kitu kinachotakiwa kufanyika haraka mara baada ya kifo.Jukumu la kuwa na vimada wengi atabeba mwenyewe marehemu.

analibebaje wakati kashakufa?
 
Inasikitisha kuona gazeti kama Majira lina-disappear mtaani. Hata hivyo lilikuwa limeshuka kiwango sana. Enzi hizo hata Mwananchi ilikuwa haoni ndani. Ilikuwa kama hujasoma Majira, then hajasoma gazeti. Business Times pia ilikuwa na forum kama mnaikumbuka.
 
Dah!!Hii Kampuni ndio inaelekea shimoni hivyo jamani hakuna bail out yoyote ile
 
1.biashara ya vyombo vya habari,idara ya matangazo ni muhimu sana.
2.kusipokuwa na matangazo ya kutosha,na ufuatiliji makini wa madeni.......kampuni au chombo hicho cha habari lazima kife.
 
source wangu pale majira anasema restructuring imefanyika..baba na mwana kama kawaida. Mhariri wake anaitwa Mapinduzi kakimbia
 
Ni kweli Bwana Mapinduzi ameondoka? Yaani yule aliyekuwa anakaimu uhariri mkuu wa Majira? Nakumbuka utabiri huu uliotolewa miezi miwili iliyopita. Hapa nanukuu, "...Kuna siku mhariri mkuu wa majira atakuwa mtoto wa mwenye kampuni, na kisha magazeti mengine kama spoti starehe na business times lenyewe. sasa wameanza na darleo, mengine yatafuata. sishangai kila nikisoma majira nakuta halina mhariri bali lina kaimu wake. anayekaimu nafasi hiyo ni John Mapinduzi. Yeye asubiri mhariri mkuu wa Majira atakapokuja kutoka familia ya mwenye kampuni. Nikifikiria hayo hata nikiambiwa nirudi business times nitakataa. Na tangu nilipoondoka 2006 sijajuta. Hiyo ni kazi ya familia. Kama bado kampuni itakuwepo mabadiliko yake yatakuwa hivi: Mkurugenzi wa Business Times Ltd, Baba Mbuguni. Meneja Mkuu, Mtoto Mbuguni, Mhariri Mkuu Majira, Family3 Mbuguni. Mhariri Mkuu Darleo, Family4 Mbuguni, Mhariri Spotistarehe, Family5 Mbuguni, Mhariri Mkuu Business Times, Family6 Mbuguni. Meneja Mkuukiwanda cha uchapaji, Mr1 Mbuguni, nk, nk. Vikao vyote vya utawala vitafanyika nyumbani na maamuzi kufanyika huko huko. Halafu mnashangaa kampuni isife!!!!!!!!!!!!!!!!????????????"
 
Back
Top Bottom