Kifo cha kampuni ya Business Times Ltd | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo cha kampuni ya Business Times Ltd

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Maimai, Apr 15, 2011.

 1. M

  Maimai Senior Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu hali mbaya ya kiuchumi inaonyemelea kampuni tanzu ya Business Times Limited. Taarifa za ndani zinasema kwamba wafanyakazi wake hawajalipwa tangu mwezi wa kwanza mpaka leo. Kisa family interference into operations. Kwa mujibu wa mfanyakazi huo chama cha wafanyakazi tayari kimetangaza mgogoro na mwajili huyo. This is the shame nakumbuka majira miaka hiyo na Business Times miaka ile. Du kweli la kuvunda halina ubani.....Correspondent wenyewe hawajalipwa kwa miezi mitano.. je tunaelekea wapi......
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwani mzee (mmiliki) si alishafariki...at that time alikuwa ni mbunge wa kulee, labda kaondoka na mali zake.
   
 3. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Labda ina undungu na CCM. Shina likifa, lazima matawi yanyauke.
   
 4. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni aibu kwa kampuni ya wazawa kuelekea kaburini, ikibidi waende kwa RA wakusanye nguvu na Habari Corporation Ltd
   
 5. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawawezi kukikwepa hicho kitanzi maana wanaandikaga habari kwa uwazi sana. kwa vyovyote vile watakuwa wamefanyiwa umafia na mafisadi.
   
 6. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nani ni mmiliki wake baada ya kifo cha mbunge ... ?

  What farmily conflict ... we can assist ..on the dispute.... just be open and loud!!!

   
 7. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #7
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asilimia kubwa ya makampuni ya kibongo (blacks) akifa mmiliki tu yanasambaratika vibaya, hii inatokana na sababu nyingi lakini mojawapo ni kuwa wabongo wengi wakishakuwa na hela wanakuwa na familia nyingi, mtu ana mke mmoja ila watoto wa nje 20 kwa akina mama tofauti. Hawa sasa ndio wanaoanza vurugu mechi ya kudai mali alizoacha marehemu maana wengi wao wakati mdingi yupo hai walikuwa wanawekwa mbali na hizo mali. Wewe fanya uchunguzi utaligundua hili.
   
 8. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Partners wakubwa wawili walikuwa Richard Nyaulawa (marehemu) na Rashid Mbuguni. Inaonekana something is not OK kwa vile mrithi wa richard Nyaulawa ni mwanaye wa kiume ambaye ameamua ku concetrate na biashara yake binafsi ya Times FM ambayo ameihamishia nyumbani kwao karibu na Kawe Beach. BTL iko chini ya mwanae na Rashid Mbuguni, sasa hapa ndiyo penye matatizo, dogo anahitaji kusaidiwa
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Duh, inaweza kuwa kweli manake gazeti huru la kila siku yaani Majira limepoteza nuru hata halimhamasishi mtu kulisoma! Majira limetutoa mbali laki ndio hivyo tena limezaliwa, likakua na halina budi kuonja umauti!!
   
 10. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  makampuni mengi yanakufa kwa sababu wenye makampuni hawashirikishi familia zao. Imagine mtu akifa ndiyo wanaanza kutafuta jinsi kazi ilifanyika.

  Sorry for them men, lazima ife. Na wewe kama hulipwi miezi yote hiyo unasubiri nini kufukuzwa au? Waondoke waende kwingine.
   
 11. a

  artist Member

  #11
  Apr 15, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Siamini kwanza kama majira bado lipo, sijaliona siku nyingi na mara ya mwisho nililiona limechooooooooka.
   
 12. h

  hoyce JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135

  Meneja ni mtoto
   
 13. Kimori

  Kimori JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2011
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama vipi wauze HISA! Ili kuwe na usimamizi nje ya familia.
   
 14. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  NI bora wauze hisa kwaq daily nation au chadema
   
 15. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  What is wrong with dogo aliyebaki BTL?

  Dogo anatatizo la ki taaluma?

  Or what is wrong with dogo?
   
 16. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Sisi kwetu katika uislamu,hilo wala haliwi tatizo kwa sababu watoto halali wenye kurithi ni hao wa mke wa ndoa tu.Na mirathi ni kitu kinachotakiwa kufanyika haraka mara baada ya kifo.Jukumu la kuwa na vimada wengi atabeba mwenyewe marehemu.
   
 17. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Hakuna lolote jamaa waliobaki hawana management vision wanapata hela na kwenda kufanya mambo ya familia Mzee Nyaulawa alikuwa anajua uongozi na hakuwahi kuwacheleweshea mishahara wafanyakazi wake ila sasa kuna watoto wa mashareholders ndio mabosi na watotro hao walitoro0ka shule so i dont think kutakuwa na jipya tena its going down na wanadaiwa kodi ya mapato kwa zaidi ya miaka nane watu wa TRA wanakwenda kuvuta tu
   
 18. w

  wakuwaza JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Hata mimi sishangai kusikia Business Times ina hali mbaya. Nina muda mrefu tangu nilipojiondoa katika kampuni hiyo. Lakini nasikia sasa mambo hayaendeshwi kitaalamu. Ukishakuwa mtoto wa mwenye kampuni inatosha kupata nafasi ya kazi. Ukiacha GM ambaye baadhi tu ya wafanyakazi wanasema ana busara na msikivu, kuna mwingine ambaye wafanyakazi wenzake wanadai hawamwelewi kwa sababu haeleweki. Nasikia ingawa huyo mwingine wanayemwita Immma hana taaluma yoyote ya uandishi na wala hajawahi kuandika makala au habari yoyote, yeye sasa ni mhariri mkuu wa gazeti la Darleo. Mtu mmoja akaniambia anahudhuria pia vikao vya jukwaa la wahariri. na sijui kama wahariri wanaokutana wanaulizana taaluma zao. kama yote hayo ni ya kweli, kwanini nishangae ninaposikia BTL iko taabani wakati inaendeshwa na watu wasiojua wanachokifanya? kama ninayosikia ni ya kweli, kuna siku mhariri mkuu wa majira atakuwa mtoto wa mwenye kampuni, na kisha magazeti mengine kama spoti starehe na business times lenyewe. sasa wameanza na darleo, mengine yatafuata. sishangai kila nikisoma majira nakuta halina mhariri bali lina kaimu wake. anayekaimu nafasi hiyo ni John Mapinduzi. Yeye asubiri mhariri mkuu wa Majira atakapokuja kutoka familia ya mwenye kampuni. Nikifikiria hayo hata nikiambiwa nirudi business times nitakataa. Na tangu nilipoondoka 2006 sijajuta. Hiyo ni kazi ya familia. Kama bado kampuni itakuwepo mabadiliko yake yatakuwa hivi: Mkurugenzi wa Business Times Ltd, Baba Mbuguni. Meneja Mkuu, Mtoto Mbuguni, Mhariri Mkuu Majira, Family3 Mbuguni. Mhariri Mkuu Darleo, Family4 Mbuguni, Mhariri Spotistarehe, Family5 Mbuguni, Mhariri Mkuu Business Times, Family6 Mbuguni. Meneja Mkuukiwanda cha uchapaji, Mr1 Mbuguni, nk, nk. Vikao vyote vya utawala vitafanyika nyumbani na maamuzi kufanyika huko huko. Halafu mnashangaa kampuni isife!!!!!!!!!!!!!!!!????????????
   
 19. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Limetoka Mbali sana, tutalikumbuka DAIMA
   
 20. k

  kibananhukhu JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha sana habari hii. Hii ilikuwa ni moja ya makampuni yenye kuletea wazawa heshima kubwa. Tuwaenzi waanzilishi kwa kuwasaidia. Nawashukuru sana mliotua taarifa hii ya kusikitisha. Mchangu wangu kama mtaalam mshauri wa biashara.

  Kwanza kuna tatizo la governance au uongozi. Siyo siri kwanza watanzania wengi wetu hatuna mchakato wa kurithishana biashara na mambo wa maana kitaalam. Pili hatuna uwezo wa kujua ni kitu gani cha msingi katika mambo yetu. Tunapenda sifa kuliko kufaidi mambo ya maana. Kwani kuna tatizo gani mtoto wa Tajiri akapata chake na akawa nje ya ofisi.

  Nashauri ili yasitokee mambo kama ya Kwacha Transport, Zainabs bus service, Scandinavia, Milo Construction, na wale jamaa wa ujenzi wakina LUKUWI Waliohusika sana na PPF Towers na miradi mingi ya waswahili iliyokuta wafanye mambo yafuatayo. Wenye kuwajua wana familia ya Business times wawaunganishe nami ili kwanza tuwape tiba ya kisaikologia, pili tuweoneshe faida za kampuni kuendeshwa kitaalam, tatu tuwapange ili wafanye kazi kitaalam.

  Kwa bahati mumewahi kabla hawajafilisika kabisa. Washauri wenzangu tuwasiline tuwasaidie wazalendo la sivyo hakutakuwa na faida ya JF. Watafanikiwa kwa kufuata kanuni za bishara na kushirikisha wataalam tu. Mbona Mzee Mfugale na Hoteli zake anaonekana anafanya vizuri? Naamini, anafanya kazi na wataalam.
   
Loading...