Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,191
PONGEZI SANA NDUGU 'MATUKUTA JUNIOR' KWA MOYO HUO WA UJASIRI JUU YA MATUMAINI YA CCM HATA IWEJE
Ndugu zangu wana-JF,
Nichukue nafasi hii kumpongeza sana tena sana huyu mtani wetu wa kijani, Ndg Mutakuta Jr, kwa ujasiri wa hali ya juu kuendelea kutetea kile anachokipenda hata darini kama hivi juu ya chama chake cha CCM.
Nasema haimpi mtu yeyote faraja kuja kusikia kwamba 2015 CHADEMA tumeshinda uchaguzi dhidi ya CCM kilicho dhaifu kwa kipindi chote, CCM kilichokata tamaa na CCM kinachoona aibu kujinadi mbele za watu kama alivyofanya hapa huyu mwenzetu Junior??????????
Binafsi, kwangu mimi naamini na kusema hapa kwamba nafarijika sana tena sana ninapogundua kwamba watani wetu wa huko CCM WANAENDELEA KUJIPA RAHA NA MATUMAINI MOYONI HAKIKA NDIKO UTAMU WENYEWE WA SIASA ZA USHINDANI UNAPOPATA NGUVU YAKE - na huo ndio msimamo wangu ulivyo.
Na ninakuhakikishia hapa kwamba nitatetea HAKI YAKO YA KUSEMA CHOCHOTE HAPA JUKWANI hata kama ninao uhakika ya kwamba kile unachokisema kweli ni upuuzi mtupu na kwamba pengine ni kule katika kujitafutia faraja tu ya muda mfupi moyoni.
Hilo ninalosema nakuhakikishia nitakutetea kwa kila hatua utakapojaliwa pumsi ya kunena zaidi na zaidi mbele ya umati huu wote uliofurika mote hapa jukwaani hata kama mtazamo wako ni kinyume kabisa na cha kwangu huku CHADEMA.
Naam, na hayo ulioyasema nayo ni maneno ya kutumainika maana huna sababu yoyote kujitangazia umauti CCM hadi pale ambapo waheshimiwa wapiga kura watakapotoa maelekezo sahihi kwa muda murua zaidi.

Mtakufa ninyi na CCM itabakia daima kama Chama Dola!!