Kifo cha CCM kimetimia

hakuna chama cha upinzani kitaweza kuiua CCM bali Ccm itajimaliza yenyewe!!
 
Mtashinda humu jf mkisema ccm itakufa, bila shaka utaiacha km uamini kwamba wewe utaicha subiri
 
Msamiati utaanza kuolewa wewe tena leo hii hii itakapotimia saa mbili usiku,halafu utaolewa na wengi kweli.nonsense.
 
Sijui ni kwanini CDM wanajiaminisha wataishinda CCM 2015!
Nakiona CDM kikishindwa kama wenzao wa Zimbabwe MDC cha Morgan Tshangilai!
 
Sijui ni kwanini CDM wanajiaminisha wataishinda CCM 2015!
Nakiona CDM kikishindwa kama wenzao wa Zimbabwe MDC cha Morgan Tshangilai!

Arusha 4-0 Bukoba mmesepa ingekuwa 8-0. 2015 usisepe matokeo ya uchaguzi uje hivi hivi bila kubadiri ID
 
Ni mapema mno kukisomea buriani chama tawala. Sioni utayari wa chama kingine cha siasa nchini kuking'oa madarakani chama tawala hasa kwa kutumia mbinu wanazozitumia sasa. Bado kuna kazi kubwa wanatakiwa kufanya kama kweli wapinzania wanahitaji kufikia lengo lao la kushika dola. Wajue kuwa wanapambana na chama dola na kimeshaonesha mara nyingi kiwa hakisiti kutumia dola kubaki madarakani. Haya ni maoni ya mtu huru asiye na mfungamano na chama chochote cha siasa.
 
Sijui ni kwanini CDM wanajiaminisha wataishinda CCM 2015!
Nakiona CDM kikishindwa kama wenzao wa Zimbabwe MDC cha Morgan Tshangilai!

Hicho ndicho kitakachowaangusha CDM. Huwezi ukashinda kwa kura kwenye uchaguzi ambao mshindani wako anaudhibiti wa mchakato mzima. Yaani yeye ndiye mwenye daftari la wapiga kura, ndiye anaamua nani aandikishwe kwenye daftari na wakati gani zoezi hilo lifanyike, anateua Tume ya Uchaguzi, anatoa ulinzi wa vituo na masanduku ya kura, anaamua wakati gani, wapi na nini uhutubie na yeye ndiye finally anatangaza nani kashinda. Kushinda katika mazingira haya haiwezekani yaani ni "Mission Impossible!!
 
Niliwahi kuwa kiongozi wa juu wa moja ya Tasisi muhimu sana Ndani ya CCM, hali kadhalika niliwahi kushiriki vikao vya juu vya kiongozi Ndani ya CCM, hivyo naweza nikawa ninaifahamu zaidi CCM, hata kuliko viongozi wangu wakuu wa Chadema, CCM inapaswa kupigwa vita hata zaidi ya Ukimwi, Agenda kubwa kwenye Mikutano ya Ccm ni kujadili uhai wa chama na kuwapora watanzania Ardhi, kuna kitu kinaitwa uwekezaji uliyomaliza Ardhi ya watanzania tuipige vita kwa nguvu zetu zote, na tuipige vita ccm, tuipige vita ufisadi, tuipende nchi yetu, tuiunge mkono Chadema.
 

tushirikiane kufunga kwa maombi kumtanguliza mungu awaondoshe hawa madalali wa Ardhi ya watanzania.
 

Kutamani CCM ife tu, hakutaiua CCM tunapaswa kuwaendea wananchi na kuwaambia kwa vinywa vyetu uovu wa CCM na kuwashawishi wainyime kura!
 

Tunakuamini, tumekutuma Simanjiro!
 
ccm ata wakitumia trilion kwenye uchaguz ujao, kamwe awawezi shindwa.
 

Maneno yako yame nichoma kama mkuki wenye sumu.....kiukweli ccm ni tatizo tanzania
 

propaganda ndio zina ipa pumzi ccm kwa sasa, lakini kumbuka watz walio wengi wana elewa kila kitu, bila kusahau ugumu wa maisha na bom la ajira...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…