Kifaa cha kutambua mabomu (made in Tanzania)

Kifaa cha kutambua mabomu (made in Tanzania)

Transistor

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,061
Reaction score
1,639
SECURITY MASTER CIRCUIT


Hii ni Design yangu nyingine(home made circuit) ambayo ni mwendelezo wa ile sakiti ya Security,safari hii nime-design ili iwe na uwezo wa kufanya kazi tofauti tofauti za securnity kutegemeana na mahitaji ya husika.

Top view ya circuit inaonekana hivi
SAM_0096.JPG


Bottom view inaonekana hivi
SAM_0113.JPG
KAZI AMBAZO INAWEZA KUZIFANYA

1.Kutambua mabomu na siraha zozote za chuma mfano bunduki.



kifaa hiki kikifungwa mlangoni,au sehemu yeyote watu wanapo ingilia kitasaidia kugundua ubebaji wa siraha hizo hata kama zipo ndani ya mabegi au masanduku.


Vilevile kifaa hiki kinaweza kutengenezewa kigari kidogo(toy car) ambacho kitakua kinabeba sakiti hii ili kukagua mabomu maeneo ambako kunahisiwa bomu lipo,.


Hii itasaidia kupunguza hatari kwa mkaguzi binadamu kusogea eneo la hatari,hivyo badala ya binadamu kusogea eneo la hatari kifaa hiki kitapakiwa katika kijigari kinacho endeshwa na remote na kupelekwa eneo hilo linalohisiwa kuwa na bomu.
Endapo kifaa hiki kitagundua uwepo wa bomu kitatuma ujumbe kwa njia ya sms pia kitawasha king'ora kuashiria uwepo wa kitu cha hatari.

2.Unaweza kuitumia kama Door security guard.


Kazi nyingine inayoweza kufanywa na kifaa hiki ni kama door security ambapo kinafungwa katika mlango wako.
Mlango wa (gari,nyumba au chochote) utakapo funguliwa au kuvunjwa bila idhini yako,ndani ya sekunde 30 utapata ujumbe kwenye simu yako(Ujumbe huu utakutaarifu kuwa mlango wako umefunguliwa).Popote pale utakapokuwa.
Baada ya kukutumia ujumbe kifaa hiki kitaanza kupiga ALARM au KING'ORA chenye sauti kali ili kuwataarifu wale watakao kuwa jirani kuhusu uvamizi huo.


Unaweza kuitumia sakiti hii vilevile katika sehemu yeyote unayo hifadhi vitu vyako vya thamani ambapo usingependa pafunguliwe na mtu mwingine bila idhini yako.
NB
Ufanyaji wake wa kazi wa skiti hii unaweza ku-design-iwa katika hali tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya mteja.
(The design is not fixed)


3.Unaweza kuitumia kama Object ditecting.


Kifaa hiki unaweza ukakitumia kutambua kizuizi chochote ambacho kitakua kinasogelea mlango wako,dirisha lako aukuta wako n.k


Mfano kama mtu atakua anasogelea mlango wako kabla hajaufikia kifaa hiki kitagundua uwepo wake na kufanya maamuzi kutegemeana na wewe unataka kifanye nini kinapo hisi kizuizi.

Mfano;-

unaweza ukataka kikihisi kizuizi kiwashe taa(mfano ni usiku huna haja ya kuwasha security lamps muda wote taa zitajiwasha tu pale mtu au kitu chochote kinaposogelea nyumba yako.hii inasaidia kupunguza bili ya umeme).
Vile vile reaction za kifaa siyo fixed utapendekeza wewe unataka kifaa kifanye nini kinapo hisi kizuizi.

4.Touch detector

Pia kifaa hiki unweza ukakitumia kutambua mtu anapo gusa,kitasa cha mlango wako;reaction yake itategemeana na wewe utataka nini kifanyike pale mtu anapogusa kitasa cha mlango wako wa gari,nyumba n.k
Kazi hizi na nyingine nyingi zinaweza kufanywa na sakiti hii!

Kama utataka u-design-iwe kitu chocho te cha electronics wasiliana nasi tutajitahidi kadri tuwezavyo ili wazo lako liwe kitu harisi.

Tazama ufanyaji wake wa kazi YOUTUBE part 1 and YOUTUBE part 2


Kwa wale wanaopenda kujifunza design za electronics darasa limeanza tayari ingia HAPA


"IT IS ALWAYS IMPOSSIBLE UNTILL IT IS DONE "
 
Hongera ila boresha uchomaji

Asante kwa ushauri wako but kumbuka this is It is just home made circuit project.

Pia ni project ambayo ilikuwa inabuniwa(there is no clear layout) hivyo trial and error was inevitable.

It is hard to have clear work circuit if you dont have clear layout design!

Hii ni design ni kama vile fundi wa nguo anavyo buni aina fulani ya mshono nadhani nguo yake ya kubunia haita kuwa sawa na ile itakayo shonwa baada ya kupata picha kamili ya ubunifu wake.

Hata hizo circuit za wazungu wanavyo buni haziwi hivyo unavyo ziona huanzia kwenye circuit board kama hizi mwisho ndio wanaprint mchoro wao katika board na kuingiza on makert.

Hope umenielewa!
 
Sasa hii kazi naona ni nzuri na huyu jamaa kaumiza kichwa kuliko yule wa kaboti ka veta ongera sana.
 
Nnaona kuna simu hapo.jipange bado upo nyuma sana

MKUU upo ?? kimya sana.
jamaa yupo juu sana aisee uwepo wa simu hapo siyo ishu sanaaa nazani nikwaajili ya kutuma SMS tuu basi.

ila kazi zingine zote nazani hiyo circuirt inamaliza hapo.
tumpe hongera sana tungepata wabongo kama 10 hv humu jf wakawa wabunifu kama huyu MKUU nazani tungekuwa far sana .
wengi tumejaa porojo za mdomoni tuuu ufaham wa mdomo mwingii vitendo 0.
 
Watanzania tukiwa na akili ya ubunifu km hii tutafika mbali sana. Tuache mambo ya kuchuuza na tufanye ubunifu. Hongera sana
 
Nnaona kuna simu hapo.jipange bado upo nyuma sana

Kwanza usiseme niko nyuma,sema tuko nyuma kwasababu mimi ni mtanzania na wewe ni mtanzania

Pili naona hujui vizuri kuhusu ufanyaji kazi wa saketi hii!

Naomba nikuulize maswali yafuatayo

1.Je Simu inauwezo wa kutambua kama mlango uko wazi na ikajituma sms yenyewe?

2.Je Simu inauwezo wa kugundua kizuizi kinasogelea mlango wako na kutoa taarifa.

3.Je simu ina uwezo wa kutambua uwepo wa bomu na kujituma ujumbe?

4.Je simu ina uwezo wa kutambua mtu anapo gusa gari lako au kitasa cha nyumba yako na kujituma ujumbe?

Sakiti hii ndiyo yenye uwezo wa kutambua aina ya tukio na kuiamrisha simu itume ujumbe.

Hivyo simu hapo imetumika kama medium of communication na siyo detector!

Hata bila simu sakiti hiyo inaweza kufanya kazi kama kawaida kwa kutoa taarifa kwa njia ya sauti n.k

Tumeweka simu ili hata yule alie mbali aweze kupata taarifa ya tukio linapo tokea.

Vifaa vingi vinavyo tumia mfumo huu wa kutoa taarifa kwa njia ya sms zinakuwa na mfumo wa simu ndani yake lakini sema tu umbile lake linakuwa sio kama simu unayo shika mkononi.Hivyo hayta kifaa hicho cha mzungu kinacho fanya kazi kama hii kinamfumo wa simu ndani yake na kinatumia SIM CARD kama kawaida.

Kwa kuwa mfumo huo wa simu na saketi ya detector unakuwa katika package moja.Ndio maana unatakiwa uweke SIM CARD upate mawasiliano kokote utakapo kuwa pale detector itakapotambua tukio la kutolea taarifa.

Mzungu kwa kuwa hufungia vitu vyake ndani ndo mana hua hujui nini na nini kipo ndani.

Simu kama simu huhitaji second part kuiendesha ikikaa peke yake haita fanya chochote;hivyo mfumo huu wa saketi yangu licha ya kuwa ni detector vilevile ni robotic circuit inayo chapa sms na kuituma.

Ubunifu sio jambo dogo hata hicho nilicho kifanya mimi chapaswa kupewa japo a single like!

Nakukaribisha katika ubunifu;sio lazima wa electronics wowote ule nahisi ukiingia ngomani utajua kwa nini hadi leo we are still being buyers of technology and not producers!
 
Big up broo! At least ume think big.
Ila naomba ufanye video kuonyesha inavyotuma ujumbe pale mlango unapofunguliwa plus na alarm yake.
 
ingekuwa KENYA ingesha sikika ila Tanzania hii yetu ni fitina tu mwanzo mwisho iliyopo kwenye serikali yetu. bado sijajua kwa nini inashidwa kuwasaidia watu kama hawa.....HONGERA MKUU
 
Hongera sana kwa kazi nzuri. Ubaya ni kwamba serikali yetu inawapuuza sana wabunifu wa hapa nyumbani
 
Wabongo tumeelekezea akil zetu kwenye ujinga video jamaa ame upload ila waliotazama ni wa5 ila ikitoka video ya loyal uko majuu had mnapigina sim pambav kabisa
 
Hongera sana...

Bahati nzuri au mbaya upo katika nchi isiyojali sana wavumbuzi na wagunduzi wa mifumo na teknolijia mbalimbali...

Lakini hili haliwezi kuwa kikwazo endapo tu utaboresha kile unachokifanya na kukigeuza kuwa suala la kibiashara...

Pia usione vibaya kuiga designs za wale waliotutangulia kiteknologia haswa kwenye suala la kuzifanya models zako ziwe simplified zaidi...

Usisite kuonesha kazi zako kwa watu ili ukosolewe na kwa namna hii utaziboresha zaidi, kila la kheri mkuu!!!

NOTE:
Kuna kitu kimoja nilikuwa nataka kujua toka kwako, hivi hizi components za kieletroniki kama resista, tansista, dayodi, OPAMP n.k huwa zinapatikana wapi kwa Dar es Salaam ikiwa mtu anataka kununua?

Na vipi kuhusu circuit boards za tests (zile ambazo huwa na vitundu kama sega la asali la nyuki) pia zipo madukani?
 
Back
Top Bottom