Au ukaunda joint vventure na vijana wenzio mnajikusanya nguvu tena wengine unawafundisha itakuwa better ni vema wazo alilo litoa mkuu lakini ukitaka kutunza legacy na heshima yako hebu panga wewe ndo uwe na kiwanda hata kama utaanza na chumba chako trust me sometimes hizi company kubwa zinakutumia afu zinakuja kuku dump kama takataka once wakiku exploit basi hata heshima yako juu ya uvumbuzi wako itatupwa. Watu wengi hatuna uthubutu wa kusema tutasimama wenyewe. Achana na serikali achana na makampuni simama wewe kama wewe kutetea kichwa chako. Umeweza kufanya jambo ambalo mabilioni hatuwezi sasa uje ushindwa kuzalisha vitu hivyo kwa wingi. Mkuu nakushauri wakomboe vijana wenzio
Nafurahi kuona unanipa mawazo chanya mkuu.
Mimi natamani sana kuona napata wafuasi katika aina hii ya elecronics(kuunda kitu chako na sio ufundi wa kurekebisha vitu vilivyotengenezwa na wenzetu).
Tatizo watu wanaona designing ya electronics ni kitu kigumu sana kujifunza,kumbe hawajui ni kitu kinacho wezekana endapo tuu unapata ufaham wa kanuni na sheria za electronics.
Tena ni kazi rahisi kuliko kuwa fundi wa TV au RADIO.Kwani ukiwa designer hata kitu chako kikiharibika kwakuwa unakijua vizuri utakirekebisha kiurahisi kuliko ambavyo TV ikiharibika kwani aliyebuni mchoro wa TV hiyo sio wewe hivyo hata urekebishaji wake unakuwa mgumu.
Mi nadhani vijana wa kielectronics wajue raha ya kuwa ma-designer;kwani wengi kwa sasa wamekuwa wanaunda vitu kwa michoro (layouts) za kukariri kama vile Inverters na amplifere.Wengi hawajui namna ya kubuni michoro yao na hilo ndio tatizo linapo anzia.
Kwa sasa mtu akikuona unasuka circuit kwenye board moja kwa moja atakuuliza "unasuka jnverter?" au "Unasuka amplifere?" ukimjibu hapana atakushangaa sasa unafanya nini?
Minadhani vijana wenzangu wakubali kuana kuwaza zaidi ya inverter na amplifere,tutizame matatizo ya jamii na kuona namnagani tutayatatua kupitia elecronics.
Kwa sasa nimefanya design nyingi kidogo na uzuri unavyo buni kitu chako na kikaonekana kuifaa jamii mara nyingi utapata kipato,na pia utajihakikishia uhakika wa ajira kwani kikiharibika hakuna mtu mwingine atakaye weza kukirekebisha ila ni wewe pekee.
Mimi nawakaribisha wanaotaka kujifunza designing za electronics waje pale napo fundishia au wanaweza kuwafundisha theory online na tukawa tunakutana siku za pactical tu.
Pia wanaweza kuwa wanatembelea blog yangu
HAPA kujifunza mambo mbalimbali ya electronics.
Pia hua nafanya workshop(semina) ya kiufundi kwa ajiri ya kutoa mafudisho kwa vijana wa electronics hua tunajifunza na kudesign vitu mbalimbali practically.Semina ya kwanzailifanyika June safari hii itaanza September 13,itakuwa inafanyka siku za weekend tu kwa muda wa siku sita.Hivyo kwa wale watakao penda kuhudhuria semina hiyo wajiandikishe mapema ili wapewe Designs zitakazo fanyika siku hizo waanze kujiandaa yeyote yule anakaribishwa chamsingi awe anajua kusoma na kuandika.