Ngoja nijaribu kuchangia kwa kuanza kuweka sawa, maana ya tafsiri na ukalimani. Hizi dhana zinachanganywa sana;
Tafsiri (Translation) ni hali ya kuhaulisha (kubadilisha) mawazo yaliyopo katika maandishi kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine. Hivyo, tafsiri uhusisha lugha ya maandishi.
Ukalimani (Interpretation) ni hali ya kuhaulisha mawazo yaliyopo katika lugha ya mazungumzo, kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine. Hivyo, ukalimani uhusisha lugha ya mazungumzo.
Zipo kampuni ambazo zimetengeneza software mbalimbali, zinazoweza kutafsiri au kukalimani (Machine translation or interpretation), lakini si lugha zote zimeingizwa katika mfumo. Fahamu, kompyuta inafanya kazi kama ilivyoprogamiwa. Kompyuta inaelekezwa na binadamu nini cha kufanya.
Kuhusu Kiswahili na Jiwe; sina uhakika lakini kuna asilimia kubwa, huwa kuna binadamu (humani interpreters), wanaofanya ukalimani wakiwa ndani ya vyumba maalumu ambavyo havipitishi sauti ( Sound proof).
Kuna sababu za msingi kwa nini binadamu ataendelea kufanya ukalimanj au tafsiri;
Lugha humu duniani hutofautiana katika vipengele mbalimbali, hivyo kuifanya wakati mwingine mashine kushindwa au kupotosha ujumbe.
Kwa mfano, mashine inaweza kushindwa kutoa ujumbe sahihi pindi unapozungumza au kuchapa Kiswahili cha mtaani, kukosea matamshi, au miundo ya sentensi.
Binadamu ataendelea kukalimani vikao muhimu, mfano AU, SADC, UN etc.