Kielelezo kingine cha udikteta aliouacha Hayati Magufuli ni kuua media kabisa

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,849
Kesho ni Katiba day na katiba hakuna mtu yeyote ambaye hana maslahi nayo.

Waandishi wa habari kama Mwangosi na Azory Gwanda waliuawa kwa sababu ya katiba mbovu na mpaka leo hatujawai kuona wanasiasa waliosababisha wakiwajibishwa.

Watu kama wakina Ngurumo wamekimbia nchi mpaka leo kwa sababu ya habari zao za kiuchunguzi kutotakiwa na tawala za ccm.

Awamu ya Magufuli waandishi mpaka walipigwa viboko na kuwekwa ndani

Utawala wa Magufuli vyombo vya habari vilifungwa na kupewa faini kubwa kubwa kwa sababu ya katiba na sheria mbovu.

Lakini leo watu wanaanzisha katiba movement Ila cha kushangaza hakuna hata media moja inayosaport movement hiyo!!.

Cha kushangaza siku Samia akitangaza kukubali katiba media zitaandika kumpongeza bila kuwapongeza walio anzisha movement hii

Bongo hatuna media kabisa.
 
Je, mtakubali maoni ya upande mwingine? Kilichoshindikana katika michakato iliyopita ni pande mbili kutokukubaliana, sidhani kama kitakuwa tofauti hivi sasa.
 
Je, mtakubali maoni ya upande mwingine? Kilichoshindikana katika michakato iliyopita ni pande mbili kutokukubaliana, sidhani kama kitakuwa tofauti hivi sasa.
Ndio maana ya national dialogue yaani tunataka kile wananchi walichosema kwa wingi ndio kitekelezwe
 
Ndio maana ya national dialogue yaani tunataka kile wananchi walichosema kwa wingi ndio kitekelezwe
Naamini unakumbuka mchakato uliopita kwamba walichosema wananchi sio kilichopendekezwa kwenye baraza la katiba. Hata ukirudi nyuma miaka ya 1990 wananchi walitaka nchi inedelee kiwa yachama kimoja, lakini mwisho wa siku marekebisho ya katiba yalifanyika na sasa tuna vyama vingi.

Makundi yanayoongizwa na vyama vya siasa ndio watakuwa wawakilishi wa wananchi kwenye baraza la katiba. Je kwa mfumo huo unadhani Chadema vs CCM itakwepeka? Na je, wanachosema Chadema ndio hicho watakachosema CCM au tutarudi hapa hapa kusema yameshidikana?
 
Tunza hii post yako, siku mama anakubali hoja ya katiba mpya lazima uje usifie kuwa ccm ni wasikivu. Wazee wa bendera fuata upepo. Kwa taarifa yako hoja ya katiba mpya ndio habari ya mjini, na hii ccm mtake msitake lazima muicheze hiyo ngoma.
Kabla ya kuingia kwenye mchakato wa katiba lazima kuwe na majadiliano na makubaliano ya awali(preminary discussions and agreement/ consensus on basic principles of ought to) kuhusu misingi ya kitaifa ambayo haiwezi kubadilishwa na katiba mpya maana yake unaua taifa la Tanzania i.e muundo wa muungano.

Haya mambo bila kupata makubaliano ya awali kitaifa hapo hapatakuwa na a way forward kwenye jambo hili. Tanzania ni tofauti na Kenya, Uganda, S.A na nchi nyingi za Afrika kimuundo, desturi, maslahi, na utamaduni wake, kwa namna yoyote lazima kuingia kwenye duru hii inahitaji umahiri na siyo porojo za wanasiasa wenye mlengo wa kusambaratisha taifa kiaina.
 
Tunza hii post yako, siku mama anakubali hoja ya katiba mpya lazima uje usifie kuwa ccm ni wasikivu. Wazee wa bendera fuata upepo. Kwa taarifa yako hoja ya katiba mpya ndio habari ya mjini, na hii ccm mtake msitake lazima muicheze hiyo ngoma.
Hakuna anayetaka katiba zaidi ya majuha wachache wa ufipa
 
Back
Top Bottom