Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 59,009
- 103,398
Kabla ya kuingia kwenye mchakato wa katiba lazima kuwe na majadiliano na makubaliano ya awali(preminary discussions and agreement/ consensus on basic principles of ought to) kuhusu misingi ya kitaifa ambayo haiwezi kubadilishwa na katiba mpya maana yake unaua taifa la Tanzania i.e muundo wa muungano. Haya mambo bila kupata makubaliano ya awali kitaifa hapo hapatakuwa na a way forward kwenye jambo hili. Tanzania ni tofauti na Kenya, Uganda, S.A na nchi nyingi za Afrika kimuundo, desturi, maslahi, na utamaduni wake, kwa namna yoyote lazima kuingia kwenye duru hii inahitaji umahiri na siyo porojo za wanasiasa wenye mlengo wa kusambaratisha taifa kiaina.
Hayo yanaweza kubakia kama yana maana kwa hivyo, lakini katiba mpya ni lazima. Na hakuna mjadala wowote wa maana utafanyika kwenye hilo, maana hakuna uwanja wa mijadala ya hivyo kwenye nchi hii, zaidi ya vikao vya vyama vya siasa. Ni hivi mjadala wa katiba mpya ni wawana siasa, hizi porojo za wananchi wote, sijui mjadala ya kitaifa ni porojo tu.